Na Mwandishi Wetu, Meatu
WANAWAKE wilayani Meatu mkoani Simiyu wamelalamikia kitendo cha
kuuziwa kadi za kliniki Sh 3,000, wanapokwenda kupata huduma ya kupimwa.
Hali hiyo, imesababisha wajawazito wengi washindwe kuhudhuria kniliki
kwa sababu ya kukosa fedha. Wakizungumza kwa masikitiko mbele ya mke wa
mgombea urais kwa wa Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Edward
Lowassa,mama Regina Lowassa, akina mama hao walisema wanashindwa kuanza
kliniki kutokana na gharama kubwa.
Walisema baadhi ya wauguzi katika hospitali za serikali mkoani
Simiyu, wamekuwa wakidai fdeha ili wawapime . Mmoja wa akina mama hao,
Fatuma Selmani alisema kuna baadhi ya akina mama amepoteza maisha
kutokana na kutokuhudhuria kliniki, kwa sababu wengi wao wanajifungulia
majumbani Walisema kero nyingen, walisema wamekuwa wakizuiwa na mabwana
shamba wasilime kilimo cha mseto kwa kuchanganya mahindi na pamba.
Alisema kutokana na ukame, wanalazimika kulima kilimo cha kuchanganya
mazao ili waweze kujikinga na njaa Naye Teresia Edward mkazi wa kijiji
cha Miringi,alisema wamechoshwa na uonevu huo.
Kwa upande wake, mama Regina alisema kuna haja ya Serikali kusikia
kilio cha akina mama hao, kwani kwa wajawazito ni muhimu ndiyo maana
kadi hutolewa bure.
Kuhusu elimu, alisema kila mtoto atasoma bure kwa sababu Ukawa
wamedhamiria kuondoa tatizo la watoto kukosa shule. “Wanawake wenzangu
naomba mwaka huu msiniangushe Oktoba 25, mpeni kura za ndiyo Lowassa ili
apate ridhaa ya kuongoza,”alisema
Created by Gazeti la Mtanzania
Friday, 18 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment