ALIYEKUWA mpenzi wa msanii wa hip hop nchini Marekani, Lil Wayne,
Christina Milian, amesema bado ana mawasiliano mazuri na mpenzi wake wa
zamani. Wawili hao walikuwa na uhusiano tangu mwaka jana, lakini Agosti
waliachana. “
Mimi na Lil Wayne bado tunawasiliana lakini hatuna uhusiano wa
kimapenzi tena kama ilivyo miezi michache iliyopita, kwa sasa tumekuwa
na urafiki mkubwa na watu wanadhani kama tuna uhusiano mpya,” alisema
Christina. Wawili hao wanatarajia kufanya video ya wimbo mpya wa mrembo
huyo aliomshirikisha Lil Wayne.
Created by Gazeti la Mwananchi.
Tuesday, 29 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment