NA CHRISTOPHER MSEKENA
RAPA na prodyuza wa muziki duniani, Kasseem Dean maarufu kwa jina la
Swizz Beat, ameonekana kuvutiwa na nyimbo mbili za msanii, Diamond
Platnumz.
Staa huyo anayeishi Marekani ameweka vipande vya video katika kurasa
zake za mitandao ya kijamii ikimuonyesha akisikiliza na kucheza nyimbo
za Diamond ‘Nataka Kulewa’ na ‘Nana’ huku akiandika ujumbe kwamba
anafurahia midundo ya Afrika.
Hii siyo mara ya kwanza kwa prodyuza huyo wa muziki kusikiliza nyimbo
za Afrika, ameshaonekana akisikiliza na kucheza wimbo wa msanii wa
Nigeria, Wizkid huku ujumbe wake ukiwa ni kwamba anapenda midundo ya
Afrika ndiyo maana anasikiliza.
Created by Gazeti la Mwananchi.
Tuesday, 29 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment