Monday, 21 September 2015

Tagged Under:

Lowassa apania makubwa

By: Unknown On: 05:05
  • Share The Gag

  • Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, Edward Lowassa akihutubia umati wa wananchi katika kampeni zake zinazoendelea.

    MGOMBEA urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema anayebeba pia jahazi la vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi na NLD chini ya mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa ameahidi kushughulikia kero za wananchi kwa haraka pindi akiingia madarakani.
    Akizungumza katika Kata ya Chanika, Jimbo la Ukonga katika Manispaa ya Ilala, Lowassa alisema nia yake ya kugombea urais ni kutaka kushughulikia kero za wananchi. Ameendelea kusisitiza azma yake ya kupambana na umasikini kwa kuinua kipato cha wananchi, kuboresha kilimo na kuondoa ushuru na tozo zenye kero kwa wananchi.
    Alisema pia atawajengea mazingira mazuri ya kufanyia biashara, waendesha bodaboda, mama ntilie na wamachinga ili kuwaondolea kero ya kufukuzwa na mgambo. Lowassa alisisitiza kuwa atatoa elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu na kuboresha huduma ya afya.
    Aidha, aliwataka wananchi ambao wanataka mabadiliko pamoja naye, kujipanga na kuwa tayari kufanyakazi kwa bidii. Naye Mwenyekiti wa Chadema – Taifa, Freeman Mbowe amemtangaza Mwita Waitara kuwa mgombea ubunge jimbo la Ukonga na kusisitiza kuwa vyama vinavyounda Ukawa havitasita kuwatimua wanachama wanaopinga maamuzi ya kusimamisha mgombea mmoja.
    “Vikao vimempitisha mgombea wa Chadema kwa sababu ana vigezo, sasa kama huyo wa Cuf (hakumtaja jina) anaendelea kuzunguka huko muache aendelee ila ni nje ya Ukawa.
    Ila vyama havitasita kumtimua anayepinga maamuzi ya kusimamisha mgombea mmoja kwani hatuko tayari kugawa kura. Kuhusu nafasi za udiwani, Mbowe akimtaka Waitara kukaa na viongozi wa vyama vya Ukawa ngazi ya jimbo ili kupitisha mgombea mmoja mmoja katika kila kata.
    Aliagiza ndani ya saa 48 zijazwe kwa kila Kata kuwa na mgombea mmoja kutoka vyama vya Ukawa.

    Created by Gazeti Leo.

    0 comments:

    Post a Comment