Rais
mstaafu, Benjamin Mkapa ameponda kauli ya vyama vya upinzani kuwa
vitaleta mabadiliko, akisema kazi hiyo tayari imefanywa na CCM.
Akizungumza
kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Bukoba wakati wa uzinduzi wa kampeini za
wagombea wa chama hicho mkoani Kagera, Mkapa alisema chama pekee
kilichobobea katika ukombozi ni CCM na Serikali zake zilizotangulia.
Kiongozi
huyo wa Serikali ya Awamu ya Tatu alisema kuwa lengo la vyama vya
upinzani ni kuing’oa CCM na lengo la chama hicho tawala ni kuendelea
kushika dola, hivyo upinzani unatakiwa kujifunza hadi baada ya miaka 50.
Alitaja
miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa kwa awamu tofauti kuwa
ndiyo aina ya mabadiliko ya maendeleo wanayohitaji wananchi, akitaja
uwanja wa ndege wa Bukoba na barabara za lami.
“Hayo ndiyo mabadiliko
ya maisha ya Watanzania huwezi kuleta ajira kwa kutamka tu, tulianzisha
wilaya na mikoa mipya ili kuchochea maendeleo ya wananchi na maisha yao
hayo ndiyo mabadiliko,’’ alisema Mkapa.
Jana, alionekana kuzungumza kwa tahadhari kwa kile alichodai akiwaeleza wapinzani ukweli wanadai ana jeuri.
Hata hivyo, katika hotuba yake alishindwa kujizuia na kutamka neno mbumbumbu na kusema hataki kuwazungumzia.
Kabla
ya kumkaribisha Mkapa kuhutubia, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera,
Costancia Buhiye alisema wagombea wote wamepita kwenye mchujo sahihi na
kutamba kwamba chama hicho kimejipanga kupata ushindi.
Created by Gazeti la Mwananchi
Wednesday, 9 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment