NA ASIFIWE GEORGE
SHINDANO jipya la ‘Graph Game’ litakalochezwa kwa kutumia simu za
mkononi kwa lengo la kuleta tija na mabadiliko na maendeleo katika jamii
kwa vizazi vijavyo limezinduliwa nchini.
Shindano hilo litakalowashirikisha watoto kuanzia chekechea hadi shule ya msingi, mwisho wa usajili wake ni Oktoba 22 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya simu ya Tigo, Diego Gutierez, ambao ndio
waandaaji wa shindano hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya Reach for
Change, alisema lengo la shindano hilo ni kuwasaidia na kuinua vipaji
kwa vijana wenye mawazo bunifu yanayolenga kuboresha maisha ya watoto.
Naye Mkurugenzi wa Reach for Change, Peter Nyanda, alisema shindano
hilo pia litasaidia kupata wajasiriamali watakaowapatia dola 20 kwa
ajili ya kutengeneza miradi yao.
Created by Gazeti la Mwananchi.
Tuesday, 29 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment