Wednesday, 16 September 2015

Tagged Under:

Kapuya, Mkumba watikisa mkutano wa Dkt. Magufuli

By: Unknown On: 09:50
  • Share The Gag
  • MGOMBEA ubunge Jimbo Kaliua Mjini, mkoani Tabora (CCM), Profesa  Athumani Kapuya, amekanusha madai dhidi yake kuwa mchana anampigia debe mgombea urais wa CCM, Dkt. Magufuli na usiku huhamia kwa mgombea urais wa CHADEMA na UKAWA, Edward Lowassa.

    Alisema yeye ni mfuasi wa CCM anayempigia debe ni Dkt. Magufuli na kuwataka wananchi wa jimbo hilo kumpigia kura mgombea wa CCM.

    Prof. Kapuya aliyasema hayo Mjini Kaliua, mkoani Tabora jana katika mkutano wa hadhara na kuongeza kuwa, uzushi huo  hauna ukweli wowote bali Dkt. Magufuli ni ndugu yake wa damu.

    Alimwomba Dkt. Magufuli baada ya kuapishwa na kuanza kazi ya urais, amsaidie kutatua kilio cha wananchi wake juu ya tatizo la upatikanaji wa huduma za maji, umeme katika baadhi ya vijiji na barabara.

    Naye Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM Taifa, Alhaj Abdallah Bulembo, aliwaomba wananchi kumchagua Dkt. Magufuli kwani nimtu mwadilifu na mchapakazi mwenye msimamo.

    Aliwakumbusha CHADEMA  kupitia aliyekuwa Katibu Mkuu wao, Dkt. Wilbrod Slaa, kuwa  mwaka 2007 walitaja orodha ya mafisadi na kusema wataiadhimisha siku hiyo kila mwaka lakini kwa sasa hawanajipya kwa sababu ya kuiondoa ajenda ya ufisadi.

    Kwa upande wake, Dkt. Magufuli aliwaomba wananchi wamchague ili aweze kutatua kero mbalimbali jimboni hapo. 

    Mkumba awa kivutio Sikonge
    Aliyekuwa mbunge wa Sikonge, mkoani Tabora, Said Mkumba (CCM), ambaye alihamia CHADEMA na kurudi tena CCM, jana alikuwa kivutio kwenye mkutano wa kampeni za mgombea urais wa chama hicho, Dkt. John Magufuli,katika uliofanyika Mjini Sikonge.

    Katika mkutano huo, Mkumba alimwambia Dkt. Magufuli kuwa alikwenda CHADEMA kuwasalimia watani zake na kuamua kurudinyumbani akiwa tayari kutumika popote atakapohitajika akiwataka waliomfuata CHADEMA warudi CCM.

    Dkt. Magufuli amwomba kadi
    Dkt. Magufuli alimtaka Mkumba amkabidhi kadi ya CHADEMA iliaamini kama amerudi CCM lakini kada huyo hakuwanayo hivyo aliifuata nyumbani na kumkabidhi mbele ya hadhara.

    Baada ya tukio hilo, Dkt. Magufuli aliwaomba wananchi kumsamehe na kuongeza kuwa, vitabu vitakatifu vya Mungu vimeandika samehe saba mara sabini hivyo asamehewe kwani alihama kwa hasira.

    Aliwaomba wananchi wamchague awe rais wao ili apandishe bei ya zao la tumbaku ambayo hivi sasa iko chini ukilinganisha na miaka ya nyuma pamoja na ujenzi wa Uwanja cha Sigara. 

    Katika sekta ya barabara, alisema itajengwa kwa kiwango cha lami kutoka Sikonge hadi Mpanda na tayari Makandarasi wameanza ujenzi huo, hivyo aliwaomba wananchi waendelee kuiamini CCM.

    Awali Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM Taifa, Alhaj Abdallah Bulembo, alimtaka Mkumba aache kutangatanga baada ya kupata taarifa za kuwapigia kampeni za chini chini wagombea wa ACT-Wazalendo.

    Ziara ya Dkt. Magufuli Kagera Katika hatua nyingine, ziara ya Dkt. Magufuli iliyokuwa ianze leo mkoani Kagera, imeahirishwa kutokana na sababu mbalimbaliikiwemo ya kuingiliana na shughuli za kiserikali. 

    Katibu wa CCM mkoani humo, Idd Ame aliyasema hayo jana wakatiakizungumza na waandishi wa habari juu ya mabadiliko hayo na kuongeza, hali hiyo imetokana na Dkt. Magufuli kuwa na shughuli za kiserikali mkoani Kigoma kama Waziri wa Ujenzi. 

    "Hadi sasa hatujapewa ratiba kamili kutoka Makao Makuu ya CCM juu ya tarehe rasmi ambayo ataanza ziara akisema walijiandaa kumpokeana kusikiliza sera zake hivyo watendelea kumsubiri," alisema

    Created by Gazeti la Majira

    0 comments:

    Post a Comment