Tandahimba. Mgombea wa ubunge
Jimbo la Tandahimba kwa tiketi ya CUF, Katani Katani amesema
akichaguliwa atahakikisha bei ya zao la korosho inaboreshwa ili kilimo
chao kiwe na tija.
Katani alitoa ahadi hiyo jana wakati wa ufunguzi wa kampeni za ubunge wa jimbo katika eneo la Mnyoma, Kata ya Mdimba.
Alisema
wananchi wa wilaya hiyo wamekua wakiongoza kwa kilimo cha korosho,
lakini ni maskini huku baadhi ya watu wakinufaika kupitia wakulima.
Katani alisema chanzo cha kudorora kwa kilimo hicho ni wakulima kukopwa,
uhaba wa pembejeo na kupangiwa bei
Kutokana na hali
hiyo aliwaomba wananchi kumpa ridhaa ya kuwaongoza na kusema kuwa
anatambua matatizo ya wakulima, hivyo atasimamia kero hizo.
“Wananchi
wa Tandahimba kipaumbele changu cha kwanza ni kuhakikisha mnapata bei
bora ya korosho kwani ndiyo zao kubwa mnalolitegemea na changamoto
mnazokumbana nazo nazijua zinatatulika,” alisema KataniCreated by By Haika Kimaro Gazeti la mwananchi
0 comments:
Post a Comment