Afrika Kusini huenda ikajiondoa kutoka kwa mahakama ya kimataifa ya ICC.
Kauli
hiyo iliafikiwa katika kongamano la sera la chama tawala nchini Afrika
Kusini, ANC (African National Congress) huko Johannesburg.Mkutano huo unaoishauri chama kuhusiana na maswala ya diplomasia na mahusiano ya nje lilipitisha mswada utakaoweka msingi wa taifa hilo kujiondoa kutoka kwa ushirikiano na mkataba uliounda mahakama ya kimataifa ya jinai ICC yenye makao yake makuu huko Hague Uholanzi.
Akizungumza baada ya kufikia kauli hiyo , Obed Bapela, ambaye ni mwenyekiti wa jopo la maswala ya uhusiano wa kimataifa inayoshirikiana na mahakama hiyo amesema kuwa mahakama hiyo imepoteza mwelekeo.
Serikali kuu ya Afrika Kusini ililaumiwa sana na mahakama hiyo ya uhalifu wa kivita kwa kukataa kumkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir alipoenda huko kuhudhuria mkutano wa kila mwaka wa marais wa Afrika chini ya nembo ya Umoja wa mataifa ya Afrika AU mwezi juni.
Rais huyo wa Sudan anatuhumiwa kwa kuendesha makosa ya uhalifu wa kivita dhidi ya watu weusi katika jimbo la darfur wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Aidha Omar al-Bashir anakabiliwa na shtaka la mauaji ya kimbari.
Created by BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment