MKUU wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Majid Mwanga amewataka
wananchi kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama juu ya watu wanaochukua
vitambulisho vya kupigia kura kwani ni matapeli.
Alisema hayo alipokuwa akielezea hali ya ulinzi na usalama kwa
wananchi wa kata ya Kibindu, ambayo hivi karibuni ilivamiwa na watu
waliosababisha vurugu na kusababisha madhara makubwa ikiwemo kifo.
Mwanga alisema kuwa licha ya eneo hilo kuwa na utulivu huku kampeni
nazo zikiendelea kwa utulivu, kumeibuka baadhi ya watu wanaochukua kadi
za wapigakura, jambo ambalo ni kosa kisheria.
“Mnapaswa kutoa taarifa kwenye vyombo vinavyohusika kwani ni kosa
kisheria mtu kuchukua kadi ya mtu ya kupigia kura, msikubali kuwapa na
mnapaswa kutoa taarifa sehemu husika ili hatua za kisheria ziweze
kuchukuliwa dhidi yao,” alisema Mwanga.
Alisema yeye akiwa ni Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya, hadi
sasa hakuna tatizo lililojitokeza tangu kuanza kampeni za uchaguzi.
Created by Gazeti la Habari leo
Sunday, 20 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment