Mgombe Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mkono
wananchi alipokuwa akiwasili katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa
Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora jana.
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli,
ametangaza mbinu mbalimbali zitakazoleta neema nchini, endapo
atachaguliwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Pia, Magufuli ameeleza mbinu ya kuondoa ukosefu wa madawati katika
shule mbalimbali nchini, kwamba ni kuwalazimisha wakurugenzi wa
halmashauri zenye shule hizo kukaa chini maofisini mwao.
Akizungumza katika mkutano uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa
Tabora katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi jana jioni, Dk Magufuli
alisema atapitia upya utaratibu wa kuwataka wahitimu wa vyuo mbalimbali
kuwa na uzoefu, kabla ya kuajiriwa katika nafasi mbalimbali za kazi,
zinazotangazwa katika utumishi wa umma.
Huku akishangiliwa na wananchi, alisema serikali yake itashusha bei
ya vifaa vya ujenzi hasa saruji, mabati na misumari, ili wananchi
wanaofanya kazi wajenge nyumba bora. Alisema atataka kila anayefanya
kazi apate kipato kizuri kitakachomsaidia kukabiliana na mahitaji ya
maisha yake, ikiwemo kujenga nyumba bora kutokana na kushushwa kwa bei
za bidhaa za ujenzi.
Katika kuongeza idadi ya Watanzania wanaofanya kazi za kujiajiri, Dk
Magufuli alisema katika kila mtaa na kijiji, Serikali yake itatoa Sh
milioni 50 kwa ajili ya kuanzisha na kukuza biashara ndogo za wanawake
na vijana.
Aidha, Dk Magufuli alisema nchi ina misitu ya kutosha, hivyo
haiwezekani wanafunzi wakae chini huku wakurugenzi wakifurahia kiyoyozi
ofisini kwao. Alisema kwamba atawalazimisha wakurugenzi wa halmashauri
zenye shule zisizo na madawati, kukaa chini maofisini mwao.
Mbali na kutoa mikopo hiyo izunguke katika ngazi ya kijiji na mtaa,
Dk Magufuli alisema Serikali yake itazuia usumbufu unaofanywa kwa
wafanyabiashara hao, ikiwemo kukamatwa kwa madereva wa bodaboda na mama
lishe.
Kwa wakulima, alisema atahakikisha pembejeo sahihi, zinatolewa kwa
wakati na mazao yatakayovunwa, na itakuwa marufuku kwa Serikali kukopa
mazao yao. Aliahidi kuondoa ushuru unaosumbua wafanyabiashara wadogo na
hasa wakulima.
Katika elimu, aliahidi kuhakikisha kuanzia mwakani, wanafunzi kutoka
darasa la awali mpaka kidato cha nne, wanasoma bila kulipa ada ili
kuondolea wazazi usumbufu wa watoto wao kurudishwa nyumbani kwa kukosa
ada.
Kauli ya Kinana
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alisema alipita katika Mkoa
wa Tabora na kukuta Hospitali ya Mkoa imetelekezwa haijajengwa kwa miaka
miwili, wakati mkandarasi ameshalipwa, akapiga kelele mkandarasi huyo
akaondolewa na sasa inajengwa.
AlisemaTabora wanalima tumbaku, lakini kati ya mkulima na mnunuzi
kuna watu wengi wa kati, ikiwemo ushirika, Bodi ya Tumbaku na Apex na
kuhoji huyo mkulima lini ataondokana na umasikini?
Mbali na wakulima, Kinana alisema pia kuna vijana wanatafuta riziki
kwa kuchimba madini, lakini hawana maeneo ya kuchimba wakati kuna watu
wameshika maeneo makubwa, lakini hawachimbi madini na vijana hao
wakienda kuchimba wanakamatwa.
Katibu Mkuu huyo alisema kama Dk Magufuli alishughulikia makandarasi
wazembe na wakati huo kulikuwa na mtu juu yake akimtuma, akiwa yeye
ndiye Rais, atakuwa kiboko ya kero hizo zote ;na kuomba wananchi
wamuamini na kumpa kura nyingi.
“Mchagueni Magufuli…Ni mzalendo, hodari, mchapakazi, haogopi mtu na
hapendelei mtu” alisema Kinana, akiowaomba wakazi hao wa Tabora,
kumpigia kura nyingi Dk Magufuli siku ya kupiga kura.
Sitta naye Spika mstaafu, Samuel Sitta akizungumza katika Uwanja wa
Ali Hassan Mwinyi, Tabora Mjini jana alisema kumpata rais si suala la
ushabiki, ni la kutafakari na kufikiria kwa makini kwa kuwa wananchi
wakikosea, wanaweza kutumbukiza nchi pabaya.
Alisema CCM ina utaratibu mzuri wa kumpata mgombea urais na mgombea
akipita katika utaratibu huo, wengine wote humuunga mkono na kumkubali
kuwa ndiye waliyeletwa na Mungu.
Alisema baada ya kumpata Dk Magufuli, hata yeye aliyewania kuteuliwa
kugombea urais, wameridhia kuwa ndiye waliyeteuliwa na Mungu, isipokuwa
mmoja wao, Edward Lowassa, ambaye alipata ghadhabu na kuondoka.
Kwa mujibu wa Sitta, Lowassa hakutosha katika vigezo kama ilivyokuwa
kwa wengine na kueleza kuwa wanalazimika kumchambua kwa kuwa anawania
nafasi kubwa ya urais wa nchi na kuongeza kuwa, hata mtu anapochumbia
ama kuchumbiwa,Watanzania hutazama tabia ya mchumba na anakotoka.
Katika uchambuzi wake, alibainisha kuwa yeye Sitta mwaka 1995 Lowassa
alipogombea urais ndani ya CCM, alimtetea lakini baadaye aliitwa na
Mwalimu Nyerere na kuelezwa kuwa hafai, kwa kuwa alipewa vyeo miaka
miwili tu akapata mali nyingi, ikiwemo majumba aliyokodishia Wajapani
mkoani Arusha.
Sitta alisema hata Rais Kikwete alimjaribu kwa kumpa uwaziri mkuu,
lakini katika miaka miwili tu aliharibu akakunjua makucha na kumkumbusha
usemi wa wahenga uliosema kuwa, ukitaka kumfahamu mtu mpe fedha au cheo
Created by gazeti la Habari leo
Wednesday, 16 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment