Thursday, 24 September 2015
Tagged Under:
NA SARAH MOSSI, KOROGWE
MGOMBEA mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan amesema alama ya ‘V’ haijawahi kushika dola duniani kote.
Samia, alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi katika eneo la Mombo akiwa njiani kuelekea wilayani Lushoto.
“Sasa hivi vurugu tupu, utawala wa nchi si wa kujaribu, wapeni wenye uthabiti, waliosimama imara na uwezo ndugu zangu, sumu haionjwi,”alisema Samia.
Mapema akiwahutubia wananchi wa Korogwe mjini katika viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi, Samia alisema Serikali inafanya mapitio ya uwiano wa mishahara kwa watumishi wa umma ili viandane na halisi ya maisha.
Alisema Serikali inatambua malalamiko ya watumishi wake, wakiwamo walimu madaktari na wauguzi.
Alisema kama wakichaguliwa watahakikisha wanshughulikia matatizo hayo haraka iwezekanavyo bila kinyongo.
Akizungumzia tatizo la maji wilayani Korogwe, alisema mradi mkubwa wa maji wilayani humo mapendekezo yake yamefikishwa kwa rais.
“Sifurahishwi kuona wanawake wanatembea umbali mrefu kutafuta maji nawaahidi awamu ya tano itauchukua mradi huo na kuukamilisha,” alisema Samia
Created by Gazeti la tanzania
Samia alia na alama ‘V’
By:
Unknown
On: 02:55

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment