Friday, 11 September 2015
Tagged Under:
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
WAZANZIBAR 504,133, wanatarajia kutoa uamuzi kwa kupiga kura ya kuamua nani awe rais wa Zanzibar kati ya wagombea 14 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake Maisara jana, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Salum Kassim Ali, alisema idadi hiyo imepatikana baada ya kukamilika kazi ya uandikishaji wapigakura wapya pamoja na uhakiki wa kuwaondoa watu waliofariki dunia.
Alisema kazi ya kuhakiki daftari la kudumu la wapigakura imekamilika, na hatua inayoendelea hivi sasa ni ya kampeni pamoja na kutoa elimu ya uraia kwa wananchi.
“Tuna wapigakura 504,133 watakaoshiriki uchaguzi wa mwaka huu, baada ya kukamilika kazi ya kuhakiki daftari la kudumu la wapigakura,” alisema Ali.
Alisema majina ya watu 5,995 yamefutwa baada ya kuthibitishwa wamefariki dunia.
Ali alisema ZEC imejipanga vizuri kufanikisha shughuli za uchaguzi.
Aliwataja wagombea walioteuliwa na tume na tayari wameanza kampeni kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu, kuwa ni Rais Dk. Ali Mohamed Shein (CCM), Kassim Bakari Ali (Jahazi Asilia), Hafidh Hassan Suleiman (TLP), Said Soud Said (AFP), Maalim Seif Sharif Hamad (CUF) na Tabu Mussa Juma (Demokrasia Makini).
Wengine ni Mohammed Masoud Rashid (CHAUMA), Issa Mohammed Longa (SAU), Juma Ali Khatib (TADEA), Ali Khatib Ali (CCK), Khamis Iddi Lila (ACT-Wazalendo), Abdalla Kombo Khamis (DP), Hamad Rashid Mohammed (ADC) na Seif Ali Iddi (NRA
Created by Gazeti la Mwananchi
Wapigakura 504,133 kuamua Rais wa Z’bar
By:
Unknown
On: 00:43

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment