NEW YORK, MAREKANI
KUNDI
la muziki kutoka nchini Kenya, Sauti Sol, wamefanikiwa kuingia Ikulu ya
nchini Marekani na kufanya onyesho la muziki wao kwa Rais Barack Obama.
Wasanii
hao walifika Ikulu hiyo kwa mwaliko wa rais huyo, baada ya mazungumzo
yao walisimama na kuimba, jambo ambalo lilimnyanyua Obama, akashirikiana
na wasanii hao kucheza wimbo waliokuwa wakiuimba.
Wasanii
hao wanaweka historia yao ya kuingia ikulu za marais mbalimbali ambapo
awali walishaingia Ikulu ya Kenya, walikutana na Rais Uhuru Kenyatta,
naye pia walimuimbia.
Wasanii hao bado wapo nchini Marekani kwa ajili ya kazi zao za kimuziki za ushirikiano na mwanamuziki John Legend.
Created by Gazeti la Mwananchi
Wednesday, 16 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment