NA CHRISTOPHER MSEKENA
UCHAGUZI mkuu wa rais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika
Oktoba 25, umepunguza kasi ya wasanii wa sanaa mbalimbali kutoa kazi zao
kutokana na upepo wa kisiasa kuchukua nafasi kubwa.
Msanii kutoka Singida, Cyrill Kamikaze, ni mmoja wao licha ya
kukamilisha uandaaji wa wimbo wake mpya, lakini anashindwa kuutoa kwa
sasa kutokana na harakati za siasa zilivyopamba moto.
“Sio mimi tu, wasanii wengi wapo kimya kwa sababu ya uchaguzi, kwa
upande wangu nasubiri uchaguzi upite ndiyo niachie wimbo mpya, nadhani
utakuwa muda sahihi na wimbo utafanya vizuri kwa kuwa harakati za
kisiasa zitakuwa zimepita,” alisema Cyrill, ambaye ni mkali wa
‘Nikikuona’.
Wednesday, 16 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment