Wednesday, 16 September 2015
Tagged Under:
*Lissu amjibu JK, asema Lowassa hahusiki na Richmond
Na Waandishi Wetu, Morogoro
MWANASHERIA mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amemkingia kifua mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa akisema hahusiki na sakata la Richmond.
Lissu ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kunukuliwa na gazeti moja akisema kuwa muhusika wa Richmond ni yule anayetembea na Lissu katika kampeni huku akimtaka amtaje kabla Rais Kikwete hajafanya hivyo.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro jana, Lissu alimtaja kwa jina kigogo wa serikali akisema ndiye muhusika mkuu wa wa Richmond na si Lowassa.
Kauli hiyo ya Lissu haitofautiani na ile ya Lowassa aliyoitoa alipokuwa akijiunga na Chadema ambapo alisema katika moja ya vikao vya serikali vya kujadili sakata hilo, kiongozi mmoja alisema amepata amri kutoka ngazi za juu kwamba asaini mkataba wa kampuni hiyo.
Lissu alisema ni vema Watanzania kutambua kuwa mmiliki halali wa Richmond ambayo imebadilishwa majina kutoka Dowans hadi Symbion kwa sasa yupo ngazi za juu serikalini.
‘’Huyu mzee wa watu wameshampaka matope vya kutosha na wala hajatoka mbele za watu kulalamika, anatumia busara zaidi.
‘’Tunaishangaa serikali kuendelea kuwadanganya wananchi bila ya huruma kwa kudai kampuni hizo zote zinamilikiwa na Lowassa, kama kungekuwa na ukweli wowote, kwanini wanaendelea kulipa hayo madeni ya mabilioni ya fedha?
“Ni lazima Watanzania watambue kuwa Richmond ilijadiliwa bungeni ikiwa chini ya mwenyekiti wake Dk. Harisson Mwakyembe ambaye alikuwa kwenye kamati ya Bunge iliyochunguza mkataba wa Kampuni ya Richmond na mwishowe kuja kuibuka kashfa ya mafisadi ambao walikuwa 11,” alisema na kuongeza.
“Katika mlolongo wa mafisadi waliotajwa namba tisa alitajwa Lowassa wakati akiwa waziri mkuu, lakini hakuhusika moja moja na suala hilo,” alisema.
Lissu alisema katika orodha hiyo namba 10 alitajwa kiongozi mmoja mstaafu na baadae akataja tena jina la kigogo mwingine ambaye alisema huyo ndiye mmiliki wa kampuni hiyo.
Alisema Lowassa ambaye anatembea naye katika kampeni zake hahusiki hata kidogo na suala hilo ila aliwajibika kisiasa ili kuiokoa serikali, kwa kuwa alikuwa msimamizi wa serikali hiyo.
Lissu alisema ili kuondoa mfumo mbovu ni lazima wahakikishe wanaing’oa serikali iliyopo madarakani kwa kipindi cha muda mrefu, kwani hiyo ndio chanzo kikuu cha umaskini.
Lowassa: na wakulima
Kwa upande wake Lowassa, alisema serikali yake itakuwa rafiki kwa wakulima na wafugaji na kuwa atatoa elimu bora bila malipo yoyote.
“Hakutakuwa na mambo ya michango ya ajabu ajabu, tutatoa elimu ya bure lakini iliyo bora,” alisema.
Kuhusu suala la viwanda vya miwa, alisema atahakikisha viwanda vinavyowezekana vitarudishwa mikononi mwa serikali.
Alisema pia kuwa, wafanyabiashara ndogo ndogo wakiwamo mama lishe na bodaboda, atawahakikisha wanaendelea kuwa rafiki zake.
Sumaye: CCM inahukumiwa kwa uongo wake
Waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, alisema kwa sasa CCM inahukumiwa kwa kusema uongo kwa kipindi cha miaka 50 tangu taifa lipate uhuru.
Alisema katika kipindi hicho, chama hicho kimeshindwa kukidhi mahitaji muhimu ya Watanzania, hivyo wananchi wamechoka kudanganywa .
Aidha Sumaye alidai Watanzania bado wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu na yenye shida pamoja na CCM kuja na sera yake ya uongo ya maisha bora kwa kila Mtanzania .
“Ni wazi hakuna ubishi kama Watanzania sasa wamechoshwa na uongo wa CCM, ndio maana wametuunga mkono kwa asilimia 100 katika mikutano yote ya Ukawa pasipo kuletwa na magari kama ilivyo katika mikutano yao”alisema Sumaye .
Alisema uongo wa CCM unajionesha wazi wazi kwenye sekta ya kilimo, afya , miundombinu, elimu na kudai kuwa hayo ni maeneo ambayo yanawatesa kwa kiasi kikubwa na kuyaona maisha kuwa magumu.
Alisema kuwa dalili za Watanzania kuunga mkono ukawa ni dalili tosha kuonesha wanahitaji mabadiliko ndani ya taifa , pasipo kushawishika na pesa .
“Hapa mmekuja kwa upendo wenu na taifa lenu hamjaletwa kwa magari kama ilivyo katika mikutano yao (CCM),” aliongeza Sumaye .
Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kanda ya Kati wa Chadema, Mathew Likwina akizungumza na wanachama wa chama hicho alisema kuwa lengo la UKAWA ni kufanya mabadiliko ya kimfumo.
Alisema kuwa kuondoa mfumo sio kubadilisha kiongozi mmoja wa ccm , bali ni kuondoa uongozi wote wa CCM usio na mfumo mzuri katika kuleta maendeleo ya taifa na watu wake .
Aidha alidai kuwa kama Watanzania wataiondoa CCM taifa linauhakika mkubwa wa kuwa na mfumo mzuri Wenye kujali maslahi ya wananchi badala ya sasa CCM imekuwa na mifumo ya kujali watu wachache na familia zao .
Habari hii imeandaliwa na Lilian Justice, Ashura Kazinja na Ramadhan Libenanga, Morogoro
Hapatoshi
By:
Unknown
On: 02:19

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment