NA CHRISTOPHER MSEKENA
SHEREHE za watoto wa mastaa katika fani mbalimbali nchini zinaendelea
kushika chati, baada ya mtoto wa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb
Abdul ‘Diamond’, Lattifah Abdul ‘Tiffah’ kufanyiwa sherehe kubwa jana.
Sherehe hiyo ilifanyika nyumbani kwa msanii huyo Tegeta kama baadhi
ya mastaa waliowawahi kuwafanyia sherehe watoto wao walipozaliwa
akiwemo, Zamaradi Mketema, Aunt Ezekiel, Mboni Masimba, Hbaba, Flora
Mvungi na wengine wengi.
Wazazi wake wameweza kumficha sura kwa muda wote ambao alikuwa
hajatimiza siku arobaini licha ya kufichwa sura ameweza kupata dili ya
kuwa balozi wa maduka mawili makubwa, moja ni duka la nguo za watoto
Msasani City Mall baby shop pamoja na Super Market iliyopo Pugu ‘Pugu
Mall’.
Created by Gazeti la Mtanzaia
Monday, 21 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment