Monday, 21 September 2015

Tagged Under:

Hemed: Nitatoa albamu hata kama hazilipi

By: Unknown On: 05:27
  • Share The Gag


  • NA CHRISTOPHER MSEKENA
    MWIGIZAJI Hemed Suleiman ‘PHD’ anatarajia kuachia albamu aliyoiita Virgo mapema mwakani tofauti na wasanii wengine wanaodai albamu hazilipi.
    Albamu hiyo itakuwa ya kwanza tangu alipoingia katika muziki na anatarajia kuachia wimbo wa ‘Itabaki story’ ili kuwapa mashabiki wake alichokiandaa katika albamu hiyo.
    “Itabaki story’ ni wimbo ambao upo ndani ya albamu hiyo pia nitaachia nyimbo nyingine mbili kama utambulisho wa albamu yangu ya kwanza toka nimeanza muziki,” alisema Hemed akidai albamu hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo 10.
    Created by Gazeti la Mtanzania

    0 comments:

    Post a Comment