Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, amewataka waumini kuliombea Taifa.
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limetangaza kuwa mgeni
rasmi katika maadhimisho ya sherehe za Idd El Hajj leo yanayofanyika
kitaifa mkoani Mara ni Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal.
Bakwata ilieleza jana kuwa sherehe hizo zitafanyika katika mji wa
Musoma na Idd itaswaliwa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo, saa
mbili asubuhi na Baraza la Idd saa nane mchana.
Sikukuu ya Idd el Hajj au Idd el-Adha inaadhimishwa baada ya
kukamilika kwa ibada ya Hija, moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu
ambapo kwa sasa mahujaji wako katika ibada hiyo nchini Saudi Arabia.
Mjini Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
Baraza la Idd, litakalofanyika Mkokotoni mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Katiba na Sheria wa
Zanzibar, Abubakar Khamis Bakary, swala ya Idd inatazamiwa kufanyika
kitaifa katika Msikiti wa Mkokotoni na Baraza la Idd kufanyika katika
Chuo cha Amali, Mkokotoni Unguja.
“Maandalizi ya swala ya Eid na Baraza la Eid yamekamilika ambapo
kitaifa utafanyika katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkokotoni,” alisema
Bakary.
Created by Gazeti la Mwananchi
Thursday, 24 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment