(East Africa Book of Records), Dk Paul Bamutaze (kushoto). Tuzo
hiyo ina lengo la kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kutatua
migogoro mbalimbali Afrika ya Mashariki. Kulia ni Mk
TANZANIA imetajwa kuwa kinara katika nchi za Afrika Mashariki kwa
kutunza amani na utulivu tangu ipate uhuru, huku Rais Jakaya Kikwete
akiibuka kiongozi bora katika ukanda huo kwa kujitolea kuleta amani
katika Bara la Afrika na kutunza amani hiyo nchini mwake.
Kwa hali hiyo, Rais Kikwete ametunukiwa tuzo mbili na Taasisi ya East
Africa Book of Records ya nchini Uganda, moja ikiwa ni kwa ajili ya
Tanzania ambayo imefanikiwa kutunza amani pamoja na utulivu tangu uhuru
na nyingine ni ya Rais Kikwete mwenyewe kutokana na juhudi zake za
kupigania amani nchini mwake na eneo lote la ukanda wa mashariki mwa
Afrika.
Kutokana na tuzo hizo, sasa Rais Kikwete ameacha kumbukumbu katika
vitabu vya nchi za Afrika Mashariki, kama mtu na kiongozi maarufu
aliyetoa mchango mkubwa katika kuleta amani kwenye nchi za ukanda huu.
Akikabidhi tuzo hizo jana Ikulu, Dar es Salaam, Kiongozi wa taasisi
hiyo Dk Paul Bamutaze alisema wametoa tuzo hizo baada ya kuangalia
mchango wa Rais Kikwete katika kuleta amani katika baadhi ya nchi barani
Afrika, akitoa mfano namna kiongozi huyo alivyoleta amani mwaka 2008
nchini Kenya, kufuatia machafuko baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.
“Tuzo ya kwanza tunaitoa kwa Tanzania kama nchi kwani ndio nchi pekee
katika eneo la Afrika Mashariki ambayo imedumisha amani na utulivu
tangu kupata uhuru na ndio imekuwa inasaidia kutatua migogoro mbalimbali
kwa majirani zake na inaendeshwa kwa utawala wa sheria,” alisema Dk
Bamutaze.
Alisema tuzo ya pili wanamkabidhi Rais Kikwete kutokana na kuwa
kiongozi bora, ambaye amedumisha amani nchini mwake, lakini pia
ameshiriki kutatua migororo mbalimbali. Alisema licha ya Kenya, lakini
ni Rais Kikwete ambaye ameshiriki kuleta amani nchini Burundi na
kurejesha serikali iliyokuwepo madarakani baada ya kuwepo jaribio la
uasi.
Rais Kikwete pia amesaidia kuleta amani katika nchi za Sudan Kusini,
Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya Jeshi la
Tanzania kuwasambaratisha kundi la waasi la M23.
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa taasisi hiyo, Adam Buyinza alisema
katika utafiti ambao wameufanya, wamegundua kuwa Tanzania imedumu kuwa
na amani kutokana na kuongozwa na CCM ambacho kina sera zinazoeleweka.
Kwa upande wake, Rais Kikwete alisema kwamba misingi ya amani na
utulivu uliopo nchini umewekewa misingi yake na Mwalimu Julius Nyerere,
ambaye uongozi wake haukubagua watu kwa misingi ya kidini, rangi na
kabila au eneo ambako anatoka mtu.
Alisema tuzo hiyo aliyoipokea sio yake peke yake, bali ni ya wananchi
wa Tanzania pamoja na wasaidizi wake ambao yeye kama nahodha wa meli
wamesaidiana kuhakikisha kuwa meli yao inaenda vizuri hata pale
panapotokea mawimbi wanasaidiana kukiendesha chombo hicho.
Rais Kikwete alisema kuwepo kwa amani nchini, kumetokana na watu wake
kuamini kwenye majadiliano badala ya kupigana na alisema hata pale
ilipotokea tofauti kati ya Serikali na vyama vya upinzani, walikaa meza
moja wakazungumza na pale ilipotokea tofauti kati ya Waislamu na
Wakristo pia walitatua migogoro yao kwa mazungumzo.
“Kwa mfano kulitokea ugomvi wa nani ana uhalali wa kuchinja, haya
mambo walitaka mimi niingilie kati, lakini jamii yenyewe walikaa na
kujadiliana kwamba yametoka wapi na nani ameyachochea, walipokaa
waligundua kwamba hakuna faida kwani mambo hayo wamejiwekea jamii
husika,” alisema Rais Kikwete.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe,
alisema kwamba tuzo hizo alizotunukiwa Rais Kikwete ni kitu kikubwa kwa
Rais anayeondoka madarakani
Created by Habari leo
Wednesday, 9 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment