Kila mtu sasa hivi yuko katika kuhesabu siku zilizobaki kufikia
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Huku tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ikikesha
mchana kutwa pale Bwawani kutoa na kupokea fomu za wagombea, bado tume
hii inayokazi kubwa ya kutoa daftari la wapiga kura.
Hadi leo hii haijajulikana ni Wazanzibar wangapi ndio watakaopiga
kura. Kimaana ndani ya daftari hili wamo waliokufa, waliohama,
waliojiandikisha mara mbili, nakadhalika.
Ikumbukwe ujanja wa kubadili mipaka ya Shehia, Wadi na Majimbo
umeleta athari kubwa kwa wananchi. Wengi hawajui wapi watapiga kura.
Mfumo uliotumika wakuwa na majimbo 54 kwa Uwakilishi na majimbo 50 kwa
Ubunge ndio kabisa mkorogovyogo. Huku mipaka yenyewe ikiwa haijulikani
mengine ikiwa imepandiana, mengine imepinzana.
Ndani ya siku 47 hizi kuna mengi yanahitajika kufanyika. Isionekane
ni mipaka au vituo vya kupigia kura, laaa hasha, kuna suala zima la
uchapishaji wa karatasi za kura. Hizi lazima ziendane a idadi ya wapiga
kura katika kituo, shehia, au jimbo husika. Leo hii ikiwa hujuwi nani
yuko jimbo gani, au mipaka ya jimbo imepitia wapi, vipi utaweza
kuchapisha karatasi za kura.
Kinyume chake unapokwenda kuchapisha karatasi za kura ni kwamba
tayari unawajuwa wapiga kura wa kila eneo. hivyo basi ipo haja ya
daftari kamili la wapiga likatolewa.
N ivyema Tume ya Uchaguzi kujipanga mapema kadri iwezekanavyo kukamilisha kazi hii kabla ya kuaparaganyika na nyengine
Created by Gazeti la Majira
Wednesday, 9 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment