Mufti Mkuu wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubery
MUFTI Mkuu wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubery amewataka wagombea wa
nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kuacha
kutumia nyumba za ibada kuomba kura.
Amewataka pia Waislamu kutomchagua kiongozi kutokana na udini wake,
kabila lake na wala aina yoyote ya sera zenye kuweza kuhatarisha amani
ya taifa.
Mufti huyo alisema hayo juzi usiku katika hotuba yake aliyoitoa
wakati wa swala ya kumkaribisha baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa
huo.
Hafla hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA) ilihudhuriwa pia na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili,
Ali Hassan Mwinyi pamoja na idadi kubwa ya waislamu.
Katika hotuba yake hiyo kabla ya kumkaribisha Mwinyi, Mufti alisema
kuwa Tanzania ni nchi ambayo imekuwa ikisifiwa kwa amani kila kukicha na
kuna kila sababu ya kuendeleza amani hiyo. Alisema kuwa Watanzania
wanaweza kuipoteza amani hiyo wasipokuwa makini na masuala yanayohusu
ubaguzi wa kidini kwani amani hiyo inaweza kupotea.
“Najua mwaka huu tunachagua viongozi kuanzia Madiwani, Wabunge na
Rais pia, hivyo ningependa kuwataka wale wote ambao wanatumia nyumba za
ibada kama misikiti na kwingineko kuomba kura kwa kisingizio cha udini
kuacha tabia hiyo,” alisema Mufti.
Alisema kuwa sio kitu kizuri kutumia nyumba za ibada kuombea kura kwa
mtazamo wa kiubaguzi wa kidini kwa kuwa inaweza kuleta mpasuko wenye
kuathiri amani.
Aliongeza kuwa Watanzania wanatakiwa kumchagua kiongozi ambaye
anapenda maendeleo, mfanyakazi na mwenye hofu ya Mungu ili kuwaunganisha
watanzania wote kuwa kitu kimoja.
“Kura ni haki yako ndugu Mwislamu wala usidanganywe kuwa kuna
uwezekano kuwa kupiga kura sio sehemu ya uislamu ila mfahamu kuwa ni
moja kati ya haki zenu za msingi kabisa”.
Aliwataka pia Waislamu nchi nzima kutumia baraza hilo kama
kiunganishi chao kuwa kuwa baraza hilo lipo kwa kwa ajili yao. Kwa
upande wake Rais mstaafu Mwinyi alisema kuwa Tanzania imekuwa ikisifiwa
kwa amani na huu sio wakati wa kuipoteza ila ni wakati wa kuiendeleza
kwa mustakabali wa taifa.
Aliwataka vijana kuepuka kutumiwa hovyo na watu kwa lengo la kuvuruga
amani na badala yake wawe mstari wa mbele katika kuidumisha
created by Gazeti la Mtanzania
Sunday, 13 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment