KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba
amewaasa Watanzania kutofanya makosa kwa kumchagua Mgombea Urais wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kuwa Rais wa
Tanzania na badala yake wamchague Dk John Magufuli ambaye ni kiongozi
makini anayejali shida za wananchi.
Akizindua kampeni za Jimbo la Mtera Kijiji cha Nagulo Kata ya
Mpwayungu, Makamba alisema Dk Magufuli ni kiongozi anayekerwa na
matatizo ya watu na kuyatatua.
Makamba alidai kuwa mgombea wa Chadema anadai kukerwa na matatizo ya
watu, lakini wakati akiwa Waziri wa Ardhi alipora Ranchi ya Mzeli na
kuifanya yake na familia yake.
Alisema hakuna zawadi nzuri, itakayoonyesha shukrani kwa Rais Jakaya
Kikwete kwa mema aliyoyafanya katika uongozi wake, zaidi ya kuchagua
viongozi wanaotokana na CCM kuanzia nafasi ya urais, ubunge na udiwani.
“Livingstone Lusinde nimemlea mwenyewe, najua utendaji wake wa kazi
na jimbo la Mtera limesikika na kupata umaarufu kwa sababu yake, hivyo
ni vyema mkamchagua tena ili aendeleze na kumaliza yale aliyoyaanza,”
alisema.
Kwa upande wake, Lusinde aliwataka viongozi wa dini waiombee nchi ili
uchaguzi ufanyike kwa amani na kutoa mwito kwa viongozi wote dini
nchini kuomba ili uchaguzi umalizike kwa amani na Rais bora apatikane.
Created by Gazeti la Habari leo
Sunday, 20 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment