GEORGIA, Marekani
ALIYEKUWA mpenzi wa marehemu Kristina Brown, Nick Gordon, amekana kuhusika na kifo cha aliyekuwa mpenzi wake mtoto wa Bobby Brown na marehemu Whitney Houston, Kristina Brown.
Kristina
alifariki Julai 26 baada ya kuanguka akiwa bafuni Januari 31 mwaka huu
na Gordon kuhusishwa na kifo hicho kutokana na kuwa na marehemu mara ya
mwisho kabla ya kupatwa na ugonjwa huo.
Vipimo
vilivyopimwa vya mwanadada huyo vimeonyesha aliwekewa sumu kwenye
kinywaji chake na Gordon ndiye anayetuhumiwa kuhusika na tukio hilo.
Juzi Gordon alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa hilo, lakini alikana kuhusika na kifo hicho.
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Gordon ana wakati mgumu na familia ya Kristina kwa kuwa inaonekana kuendelea kumfuatilia zaidi.
Created by Gazeti la Mwananchi
0 comments:
Post a Comment