Papa Francis kuongoza misa Cuba
Maelfu ya
waumini wa kanisa katoliki wanahudhuria misa mjini Havana hii leo
ambayo itaongozwa na kiongozi wa kanisa katoliki papa Francis ambaye
anafanya ziara nchini humo kwa mara ya kwanza.
Papa Francis amezitaka Marekani na Cuba kuendelea kuboresha uhusiano kati yao.
Papa Francis amezitaka Marekani na Cuba kuendelea kuboresha uhusiano kati yao
Akiongea
kwenye uwanja wa ndege wa Havana anapoanza ziara nchini Cuba na
Marekani, papa Francis alipongeza uhusiano ambao umeshuhudiwa kati ya
nchi hizo.
Rais wa Cuba Raul Castro amemshukuru papa Francis kwa jitihada zake kurejesha uhusiano kati ya Cuba na Marekani.
Akijibu
hayo rais wa Cuba Raul Castro amemshukuru papa kwa wajibu wake katika
kusaidia kurejesha uhusiano kati ya Cuba na Marekani.
Hii ndiyo
ziara ya kwanza anayofanya papa Francis nchini Cuba baada ya kulakiwa
na umati uliokuwa ukipeperusha bendera za Cuba wakati msafara wake
ulikuwa ukipita katika mitaa ya mji wa Havana.BBC
0 comments:
Post a Comment