IGP Ernest Mangu.
WATU watano wa familia moja akiwemo mtoto wa miezi tisa, wameuawa kwa
kukatwa mapanga kutokana na ugomvi unaodaiwa kua wa mgogoro wa ardhi
katika kijiji cha Kisesa katika Kata ya Bugarama, wilayani Maswa, Mkoani
Simiyu.
Kamanda wa Polisi Mkoa Simiyu, Gemini Mushy amethibitisha, akisema
waliokufa papo hapo ni baba wa familia, George Charles (30), Siku John
(23) ambaye alikuwa mke wa George na watoto wao Nchambi George(7), Tuma
George (5) na Amos George mwenye umri wa miezi 9 wote waliuawa kwa
kukatwa mapanga sehemu zao za shingoni na watu wasiofahamika.
Alisema wauaji hao waliivamia familia hiyo saa 9:00 usiku wa Septemba
28 mwaka huu na kuwatendea unyama ambao chanzo kikisadikiwa kuwa ni
mgogoro wa ardhi kati ya marehemu na baba yake wa kambo ambaye alinunua
kipande cha ardhi alipokuwa akiishi marehemu.
Kamanda Mushy alisema kuwa katika tukio hilo jeshi hilo
linawashikilia watu watatu kuhusiana na mauaji hayo ambao ni Migata
Lusalago (50), Jihelya Migata (30) na Sollo Kengele (31) wote wakazi wa
kijiji hicho huku likiendelea kuwatafuta wahusika wengine ili wafikishwe
mahakamani.
Wakati huohuo, John Gagarini anaripoti kutoka Kibaha kuwa, watu
wawili wamekufa na wengine 33 wamejeruhiwa baada ya baada ya basi la
Ngorika kugongana uso kwa na basi dogo la abiria.
Akithibitisha jana, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Jafary Mohammed
alisema basi la Ngorika lilikuwa linaelekea Arusha kutoka Dar es Salaam.
Alisema ajali hiyo ilitokea eneo la Misugusugu wilayani Kibaha majira
ya saa 1:30 .
Created by Gazeti la HabariLeo.
Tuesday, 29 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment