Kinana
NA SARAH MOSSI, LINDI
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
amesema chama hicho kina uwezo wa kuzuia mafuriko hata kwa kidole,
achilia mbali mikono.
Nape ambaye ni mgombea ubunge Jimbo la Mtama mkoani Lindi, alisema
hayo jana katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Nyangao na
kuhudhuriwa na mgombea mwenza wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan.
Katika mkutano huo, Nape aliwabeza wanachama waliowania nafasi ya
urais kupitia CCM na ubunge, kisha wakatemwa na baadae wakaamua kuhama.
“Mimi sizuii mafuriko kwa mkono, uwezo wangu ni kuzuia mafuriko hata kwa kidole,” alisema Nape.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, jimbo lake litaongoza kwa kutoa
kura nyingi za urais.“Ni aibu jimbo analotoka katibu mwenezi taifa,
lishindwe kutoa kura za kutosha za urais,” alisema.
hatua nyingine, aliitaka Serikali kukirejesha mikononi kiwanda cha
kubangua korosho kilichopo ili kiwape ajira vijana wengi ambao hawana
ajira jimboni humo.
“Wanatunyonya, wakati mwalimu anaondoka kusini kulikuwa na viwanda
vya korosho wakaviua, tunaomba turudishiwe kiwanda chetu cha kubangua
korosho vijana wetu hawana kazi,” alisema.
Nape alilalamikia tatizo la maji linalowakabili wananchi wa jimbo
hilo na kusema waliowaagusha ni Benki ya Dunia ambayo imeshindwa kutoka
fedha za maendeleo kwa wakati.
Akijibu hoja hiyo, Samia alisema mfumo wa stakabadhi ghalani
ulianzishwa kwa nia njema na Serikali, lakini watendaji wa vyama vya
ushirika waliukoroga.
“Tunataka mkulima wa korosho alipwe fedha zake anapopeleka mazao
sokoni na si bonsai…Serikali ya awamu ya tano itaongeza thamani ya bei
ya korosho na ufuta, tutajenga viwanda vya ushirika mtakaounda wenyewe
ili mpaki vizuri bidhaa zenu,” alisisitiza Samia.
Akizungumzia mfumo wa stakabadhi ghalani alisema Serikali
itahakikisha inakarabati mfumo huo na kusisita haitowavumilia watendaji
wa vyama vya ushirika wazembe.
Akijibu ombi la Mtama kuwa wilaya, Samia aliwaomba viongozi kufuata utaratibu wa kisheria na kuahidi kulisimamia jambo hilo
cREATED BY gAZETI LA mWANANCHI
Wednesday, 16 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment