Mgombea Uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli akihutubia wakazi wa
Geita mjini kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho uliofanyika kwenye
viwanja vya Karangalala mjini humo jana.
SIKU moja baada ya matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza
kuonesha kuwa anapaa katika urais, mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Dk John Magufuli ametamba kupata ushindi wa ‘tsunami’.
Akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa kampeni mjini Geita
jana jioni, Dk Magufuli alisema hana shaka kuwa atapata ushindi mkubwa
kwa sababu amejionea hali ya kukubalika miongoni mwa Watanzania katika
mikoa 15 aliyopita tangu aanze kampeni Agosti 23, mwaka huu.
“Nitapata ushindi wa tsunami kwa sababu watu wanataka kuendelea na
Tanzania yao. Huu ni mkoa wangu wa 15, nimeanzia Katavi, nimeona jinsi
watu wanavyotaka mabadiliko, watu wamejitokeza kila mahali kunilaki na
kunihakikishia ushindi.
“Ndio maana niliamua kutembea kwa gari, kutembea katika barabara
mbovu, kwani uwezo wa kutembea na helikopta ninao, ningeweza kuja hapa
kwa helikopta, lakini niliamua kutembea ili kujionea hali halisi, ili
nikifika Ikulu nikumbuke shida za Watanzania na nikafanye kazi ya
kuwatumikia,” alisema Dk Magufuli.
Awali, mgombea huyo alipokewa kwa kishindo mkoani Geita liliko Jimbo
la Chato aliloliongoza kwa miaka 20. Licha ya maelfu ya watu
waliojitokeza kwenye mkutano wake mjini Geita, vile vile katika maeneo
mbalimbali ya wilaya za Bukombe, Chato na Geita, hali ilikuwa hivyo.
Akiwa mjini Geita, Polisi walipata kazi ya kusimamia usalama kutokana
na msongamano wa watu uliokuwa uwanjani hapo hali ambayo kuna wakati
ilitokea tafrani iliyosababisha sehemu ya umati kwenye Uwanja wa
Kalangalala, kukimbia ovyo bila kufahamu chanzo.
Katika maeneo mengine hususan kwenye mikutano iliyofanyika kwa
nyakati tofauti Katoro (Geita) na Lunzewe (Bukombe), zilisikika sauti
zilizopazwa zikisema yeye ndiye rais. Akihutubia mjini Geita, Magufuli
aliwataka wananchi wawazomee mafisadi kwa kusema haooo, nao wakaitikia
kwa kusema ‘haooo’.
Aidha, alisema wakati mwingine watu wanaichukia serikali kwa sababu
ya watu wachache. Kuhusu huduma mbaya hospitalini, Magufuli alisisitiza
kwa kusema atahakikisha dawa zinapatikana hospitalini na wakati huo huo
watumishi wa afya watapata maslahi ya kutosha.
Akiwa mjini Katoro katika Jimbo la Busanda, alisema hachukii utajiri
isipokuwa anachukia ufisadi ambao umechangia baadhi ya huduma
kutopatikana ipasavyo. “Sichukii utajiri, lakini nachukia ufisadi,”
alisema mgombea huyo na kufafanua kwamba ufisadi ndiyo umekuwa
ukisababisha hata dawa zikosekane katika hospitali badala yake, wananchi
wanaambiwa wakanunue kwenye maduka binafsi.
Magufuli ambaye amekuwa akiahidi kutatua kero mbalimbali ikiwamo
kukomesha ushuru kwa wajasiriamali wadogo wakiwamo mama lishe,
wafanyabiashara ndogondogo na waendesha bodaboda, anasema anafahamu
mianya ya kuziba kuhakikisha fedha hizo zinanufaisha wengi.
Akiwa kwenye mkutano huo wa jana mjini Katoro uliohudhuriwa na maelfu
ya watu, alisisitiza kuwa serikali yake itajenga mazingira yakusaidia
wanyonge. Magufuli ambaye alisisitiza kuwapenda watu wote wakiwamo
wafanyabiashara, wafanyakazi, wakulima, hata hivyo alisema, kwake jambo
la msingi ni kazi tu.
Alisema ni lazima kutengeneza mazingira ya kusaidia wanyonge. Alisema
umasikini upo asilimia 28 na malengo yake ni kuhakikisha unapungua kwa
kiwango kikubwa. Alisema akiwa serikalini miaka 20, amejifunza mengi.
Alisisitiza kuwa lazima hata zao la pamba liwe juu. Kuhusu viwanda
mkoani Geita, alisema ipo haja ya kuvifufua ikiwamo vya kukamua juisi
ili kutoa soko kwa zao la nanasi na atahakikisha manufaa wanayopata
wachimbaji wakubwa, yanapatikana pia kwa wachimbaji wadogo.
Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM inasema watawapa wachimbaji wadogo
teknolojia mpya, vifaa vya uchimbaji pamoja na kuendelea kuwarudishia
maeneo ya uchimbaji. Alisema katika uongozi wa sasa wa Rais Jakaya
Kikwete, yamerudishwa maeneo 25
Created by Gazeti la HabariLeo
Thursday, 24 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment