NA CHRISTOPHER MSEKENA
KUNDI la Navy Kenzo linaloundwa na wapenzi, Emmanuel Mkono ‘Nahreel’
na Aika Mareale ‘Aika’ limekuwa gumzo nchini Nigeria kutokana na wimbo
wao wa ‘Game’ waliomshirikisha Vanessa Mdee kupigwa mara kwa mara katika
redio na televisheni za huko.
Nahreel alisema amekuwa akipokea simu kutoka kwa watangazaji wa vituo
mbalimbali vya redio na runinga vya nchini humo kwa ajili ya mahojiano,
huku wengine wakimpongeza kwa wimbo huo unaofanya vizuri nchini humo.
“Wanadai ‘audio’ na video ya wimbo wetu unafanya vizuri nchini mwao,
ndiyo maana upo katika chati za juu katika vituo vya redio na runinga
nchini humo, tunashukuru na tutazidi kuandaa kazi nzuri kama
inavyoendelea kujitokeza kwa kuvuka malengo ya tulivyojipangia
kimafanikio ya kazi zetu,’’ alieleza Nahreel.
Created by Gazeti la Mwananchi
Wednesday, 16 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment