Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
MGOMBEA
Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ali Mohammed
Shein, amesema amedhamiria kuipaisha Zanzibar kwa kuwa uwezo huo anao.
Amesema
kwamba, pamoja na majukumu mengi aliyonayo, kazi hiyo ataifanya katika
miaka mitano ijayo kama atafanikiwa kuendelea kukiongoza kisiwa hicho.
Kutokana
na hali hiyo, amewatahadharisha Wazanzibari wasiwachague wagombea
waongo ambao mara zote wamekuwa wakisema uongo majukwani kwa lengo la
kupata madaraka.
Dk.
Shein ambaye anatetea nafasi yake ya urais wa Zanzibar, alitoa kauli
hiyo jana alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi katika uwanja wa
Galagala uliopo Mjini Magharibi, Unguja.
“Kwa
kweli bado nina nia ya kweli dhati ya kuwatumikia Wazanzibari kwa sababu
uwezo huo bado ninao. Nawaomba sana vijana msidaganywe na wanasiasa
wasiokuwa waaminifu kwani hakuna rais atakayekuja kutoa ajira kwa kila
mzanzibari kwani hilo nimeliona baada ya kuizunguka dunia hii.
“Kwa
kuwa bado nina uwezo, nimelazimika kuja na mambo mbalimbali
yatakayoipaisha Zanzibar kiuchumi ikiwamo ujenzi wa kiwanda cha samaki,
uwekezaji katika sekta ya uvuvi na ujenzi wa kiwanda cha maziwa.
“Yote
hayo ni mambo ya msingi kwa sababu yatasaidia kuzalisha ajira na pia
yatawawezesha wananchi kuweza kukabiliana na gharama za maisha,”
alisema.
Katika
kuhakikisha Zanzibar inasonga mbele kiuchumi, Dk. Shein alisema
Serikali yake hivi karibuni itazindua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume utakaokuwa chachu ya maendeleo kisiwani humo.
Kuhusu
suala la wazee, alisema kuanzia mwakani, kila mzee aliyefikisha umri wa
miaka 70, atakuwa akipewa pesheni ya Sh 20,000 kila mwezi.
Created by Gazeti la Mwananchi
Monday, 28 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment