MCHEKESHAJI wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja
Mkandamizaji’, amewataka wanaomtuhumu kwamba anatumia tiketi ya
uchungaji kama njia ya kujiingizia kipato wajaribu kazi hiyo wataona
malipo yake.
Aliongeza kuwa uchungaji ni wito na siyo kazi, pia uchekeshaji ni
ajira yake, hivyo hawezi kuacha uchekeshaji kwa sababu ya uchungaji kwa
kuwa hakiuki miiko ya uchungaji.
“Eti wanasema uchungaji na siasa wapi na wapi, mbona kuna chama cha
siasa kimojawapo mgombea wao wa urais ameletwa na mchungaji lakini
kwangu ndiyo siyo sawa? Anayedhani uchungaji ni dili, ajaribu aone kama
hajatoka majipu kama Ayubu,” alieleza Masanja, alipokuwa katika moja ya
mikutano ya kampeni ya kisiasa alipoalikwa na Chama Cha Mapinduzi
Created by Gazeti la Mtanzania
Thursday, 24 September 2015
Tagged Under:
http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2015/09/masanja-300x300.png
By:
Unknown
On: 02:40
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment