Mbeya. Serikali imekubali kupunguza viwango vya
kodi kwa wafanyabiashara na kuiondoa kwa wale wenye mauzo yasiyozidi Sh4
milioni kwa mwaka.
Meneja wa Mamlaka ya Kodi Tanzania
(TRA) Mkoa wa Mbeya, Arnold Maimu, alisema Serikali kupitia kwa Kamishna
Mkuu wa Mamlaka hiyo, ilimaliza mgogoro na wafanyabiashara kuhusiana na
viwango vya kulipa kodi.
Maimu alisema ushirikiano
wanaotoa wafanyabiashara kwa sasa umeleta mafanikio katika kukusanya
kodi. Mwenyekiti wa wafanyabiashara, Charles Syonga, alisema Serikali
ilisikiliza kero zao na sasa mambo ni shwari.
Alisema hivi sasa wanawahamasisha wafanyabiashara wote kulipa kodi TRA baada ya kuridhishwa na makubaliano hayo.
Syonga
alisema wafanyabiashara wenye mauzo hadi Sh7.5 milioni sasa, watalipa
kodi ya Sh150,000 kwa mwaka badala ya Sh200,000 iliyopangwa awali.
Ofisa
Elimu kwa Walipakodi kutoka TRA Mkoa wa Mbeya, Kissa Kyejo, alisema
Serikali pia ilikubaliana na wafanyabiashara kwamba watakoingizwa kwenye
utaratibu wa VAT ni wenye mauzo yanayoanzia Sh100 milioni badala ya
wale wa Sh40 milioni.
Awali wafanyabishara mkoani hapa
walikuwa na mgogoro na TRA kuhusiana na kutakiwa kulipa kodi kwa viwango
vilivyowekwa na Serikali.
Created by Gazeti la Mwananchi
Created by Gazeti la Mwananchi
0 comments:
Post a Comment