Dar es Salaam. Baadhi ya wasomi na wanaharakati
wamekemea kauli ya mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli ambaye amekuwa
akiwaonya wanaotaka mabadiliko ya haraka nchini akiwakumbusha
yaliyojitokeza nchini Libya.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti leo wasomi hao wameiita kauli hiyo ni ya vitisho kwa wananchi,
kwa kuwa mabadiliko wanayotaka ni ya kidemokrasia na siyo vita.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Sikika, Irenei Kiria, amesema wananchi
wamejiandaa kwa ajili ya kupiga kura na siyo vita kama wachache
wanavyofikiri.
“Mabadiliko yanayozungumzwa na wengi ni
ya kidemokrasia na siyo vita, hivyo Dk Magufuli hapaswi kutolea mfano wa
Libya, tumejiandaa tangu 2010” alisema.
Amesisitiza : “
Ukweli ni kwamba kuna watu wamekuwa wanataja vita hapa nchini tangu
mwaka 1995 hao wanatamani kuleta machafuko wamethubutu kufananisha na
Rwanda au Burundi, wakati nchi hii ni tofauti kwani CCM imekuwa
madarakani kwa 50 na amani ipo,” amesema Kiria.
Mkurugenzi
wa Kituo Cha Haki za Binadamu (LHRC), Hellen Kijo-Bisimba amesema
wakati wa kampeni si wa kutoa kauli za vitisho bali, wananchi
wanachohitaji ni kusikiliza sera za vyama husika ambavyo vitawawezesha
kufanya uamuzi wa kuvichagua.
Akiwa mikoa ya Morogoro
na Tanga, Dk Magufuli amekuwa akitoa kauli za kuwaonya wanaotaka
mabadiliko kuwa wakumbuke yaliyotokea Libya ambapo nchi hiyo imezama
kwenye machafuko baada ya kuondolewa aliyekuwa kiongozi wan chi hiyo
marehemu Muamar GadhafiCreated by Gazeti la Mwananchi
0 comments:
Post a Comment