Ilipoishia sehemu ya tatu ( kama hukuisoma bofya hapa)
Dorice akamsogelea Doreen kwa hatua chache.
"Jana ulikuwa na nani pale kwenye mti usiku?" aliuliza Doreen huku akiuchezesha mguu wake wa kulia chini na mkono mmoja akiwa kaushika kiunoni.
"hukuniona au?" aliuliza Dorice kwa mshangao.
"jibu swali!"
"OK! nilikuwa na Eddy"
"nani yako Eddy?"
"Doreen unanitisha ujue?"
"kha! nakutisha nina mapembe hapa? nijibu swali langu"
"Eddy mpenzi wangu!"
"nimekupata sasa... tangu lini Eddy mpenzi wako hujui kama ni mume wangu mtarajiwa?"
"Ati nini....... Eddy ni. .."
"Jana ulikuwa na nani pale kwenye mti usiku?" aliuliza Doreen huku akiuchezesha mguu wake wa kulia chini na mkono mmoja akiwa kaushika kiunoni.
"hukuniona au?" aliuliza Dorice kwa mshangao.
"jibu swali!"
"OK! nilikuwa na Eddy"
"nani yako Eddy?"
"Doreen unanitisha ujue?"
"kha! nakutisha nina mapembe hapa? nijibu swali langu"
"Eddy mpenzi wangu!"
"nimekupata sasa... tangu lini Eddy mpenzi wako hujui kama ni mume wangu mtarajiwa?"
"Ati nini....... Eddy ni. .."
Sehemu ya nne
.... DORICE alishtuka sana kusikia Eddy ni mume mtarajiwa wa Doreen hakutaka kuyaamini maneno ya Doreen hata kidogo.
"hivi we Doreen umechanganyikiwa au upo timamu?" Dorice aliropoka kwa hasira.
"
nikuulize wewe, hivi upo timamu au mwendawazimu unavomng'ang'ania
mpenzi wangu Eddy? mpaka watu wanakushangaa! inaniuma sana Dorice usione
nimekukaushia!" Alisema Doreen kwa msisitizo wa hali ya juu. Maneno
ambayo yalizidi kumuumiza Dorice mpaka machozi yakaanza kumlengalenga
machoni mwake. Alimtazama Doreen kwa hasira huku akiumanisha meno yake
kwa ghadhabu, moyoni alitamani kumuadhibu vikali Doreen kwa kutaka
kulitia DOA penzi lake na Eddy lakini hakuwa na uwezo huo.
"Ama
kweli kikulacho ki nguoni mwako! sitaki kuamini kama rafiki yangu
kipenzi Leo unageuka adui yangu!"alisema Dorice huku akipiga hatua na
kutaka kuondoka mbele ya mbaya wake. Lakini ghafla Doreen akamvuta shati
na kumrudisha pale alipokuwa amesimama.
"we vipi? hebu niache niondoke?"
"nitakuachaje
sasa wakati unaniharibia penzi langu na Eddy?" alisema Doreen kwa
kujiamini sana huku akibetua midomo yake kwa dharau utadhani Eddy ni
mpenzi wake kweli kumbe hakuna lolote ni tamaa na wivu vinavyomsumbua.
"umefanikiwa
kuniumiza moyo wangu Doreen mpaka najuta kukufahamu.... haya Fanya
lolote utakalo tena ili kunyang'anya haki yangu ya mapenzi... do it!"
alisema Dorice kwa kwikwi kwani alishindwa kuzuia kilio chake kutokana
na maumivu makali aliyoyapata moyoni mwake kwani maneno ya Doreen
yalikuwa kama mkuki wenye sumu katikati ya moyo wake.
"hata Mimi najuta kukutana na mwanaharamu wewe, Kwa usalama wako achana na Eddy... sijui unanielewa?"
Dorice
hakusema chochote zaidi ya kumkazia macho ya hasira Doreen, bila kujua
kuwa kutazamana na Doreen kwa wakati ule ilikuwa ni kujikaanga kwa
mafuta yake mwenyewe kwani Doreen aliitumia nafasi ile vizuri sana.
Alijibadilisha
macho yakawa ya kutisha sana kisha kila alipomtazama Dorice machoni
alimhamishia vitu Fulani visivyoeleweka, kisha baada ya hapo Doreen
alimsogelea Dorice na kumzodoa lakini haikuwa kumzodoa kwa kawaida Bali
alimpaka vitu kama kamasi USO mzima na kumfanya Dorice atie kinyaa sana
bila yeye mwenyewe kujitambua.
"hebu
niondokee hapa mpuuzi wewe na ushukuru Mungu sijakufanya kitu kibaya"
alisema Doreen baada ya kuhakikisha amekamilisha kazi yake aliyokusudia
kwani sio siri Doreen alipania kumpata Eddy kwa vyovyote vile.
Dorice alitembea taratibu na kumfuata Eddy darasani huku akiendelea kulia.
==>Endelea nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>
==>Endelea nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>
Credit; Mpekuzi Blog
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
ReplyDeleteKAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.