NEW YORK, MAREKANI
NYOTA wa filamu nchini Marekani, Will Smith, anatarajia kurudi kwenye muziki baada ya kukaa kimya kwa zaidi ya miaka 10.
Msanii huyo alikuwa kimya mara baada ya kuachia albamu yake ya ‘Lost and Found’, aliyoiachia 2005 na kuingia
kwenye filamu na sasa amerudi katika muziki.
Tayari msanii huyo amemaliza baadhi ya video zake katika nyimbo alizotumia lugha ya Kiingereza na Kihispania.
“Nimekaa nje ya muziki kwa muda mrefu, lakini kwa sasa nimeamua kurudi tena kwa kuwa ni fani yangu, kuna
kazi ambazo ziko tayari nimezifanya na Kanye West tangu Februari
mwaka huu, lakini bado sijaziachia, naamini huu ni muda sahihi wa
kufanya hivyo,” alisema Smith.
Chanzo Mtanzania
Tuesday, 6 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment