Ilipoishia sehemu ya Tano ( kama hukuisoma bofya hapa).
Eddy
alimwacha Dorice Solemba, akilia na moyo nje ya darasa. Na alipoingia
darasani Eddy alifuatwa na Doreen kwenye kiti chake, na alitaka
kumwambia kitu muhimu....
Endelea...
Doreen
alizidi kujilegeza sana kwa Eddy ili amteke kimawazo na kiakili
sawasawa. Alirembua macho kama aliyekula kungu huku akimtazama Eddy..
Hakika kwa urembo aliokuwa nao Doreen na vituko alivofanya alizidi kuziteka hisia za Eddy haswa. Mtoto wa kiume alijikuta anaishiwa pozi, uvumilivu ukamshinda akajikuta anakohoa kidogo ili asafishe koo na kuweza kusema la moyoni.
Hakika kwa urembo aliokuwa nao Doreen na vituko alivofanya alizidi kuziteka hisia za Eddy haswa. Mtoto wa kiume alijikuta anaishiwa pozi, uvumilivu ukamshinda akajikuta anakohoa kidogo ili asafishe koo na kuweza kusema la moyoni.
"Eddy!" Doreen aliita kwa sauti ya mvuto sana.
"Naam"
"niambie basi.."
"ah!..
Doreen kama nilivosema awali wewe in mzuri sana hivyo basi .... nataka
uwe mpenzi wangu.. please! naomba unielewe!" Eddy aliongea kwa sauti ya
chini ili majirani wasiweze kusikia.
"Eddy!
we ni shemeji yangu siwezi kumsaliti rafiki yangu Dorice!" Doreen
alijifanya kukataa ingawa moyoni mwake alifurahia ushindi wa kumpata
Eddy ilhali warembo wore shuleni pale waliikosa nafasi ile isipokuwa
Dorice.
"Doreen! plz naomba nikubalie nakupenda sana "
"Na Dorice je?"
"habari za Dorice achana nazo me nimeachana nae, nakupenda wewe"
"mi sitaki Eddy!" sauti aliyoitoa Doreen ilionesha kabisa alikuwa anataka Ila alivunga tu.
"Nikubalie
Dori.. nakupenda Doreen.. usinitese!" Eddy alisema huku machozi
yakimlengalenga kwani hakutaka kumkosa Doreen. Ama kweli dawa za Doreen
alizotafuna kabla ya kumfuata Eddy zilifanya kazi vizuri sana.
"Okey! nakubali kuwa na wewe!"
"Oh
my God kweli Doreen unanipenda? asante sana!" Eddy aliachia tabasamu
mwanana na alitamani hata kumkumbatia Ila aliogopa kufanya vile kwani
walikuwa darasani.
"Nakupenda Eddy Ila kuna sharti moja muhimu inabidi ufate ili uwe na Mimi..."
"sharti gani tena?" Eddy alishtuka
"upo tayari?"
"ehm.. ah ndio coz I love u.. ntafanya"
"good.. nafurahi sana"
"Niambie basi mpenzi.." alisema Eddy akitabasamu.
"usijali nitakuambia baadae..."
Alisema
Doreen huku akiinuka kitini na kuondoka zake. Eddy alikuwa na furaha
sana hakuweza hata kusoma zaidi ya kumfikiria Doreen na kila Mara
aliachia tabasamu.
==>Endelea Nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>
==>Endelea Nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment