Staa wa Filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema kuwa sababu ya
kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mwanamuziki Baraka Da Prince ni
kuhitaji penzi la kweli na si vinginevyo.
Akipiga stori na Ijumaa, Nisha alisema kuwa watu wamekuwa
wakimsengenya kwa kudai kuwa eti yeye kuwa na Baraka ni sawa na
‘kumbemenda’ lakini akajitetea kwamba penzi la siku hizi haliangalii
umri, kikubwa ni penzi la kweli.
“Unaweza kuwa na mtu mzima mwenzako na msielewane lakini ukawa na
‘serengeti boy’ mkaelewana hivyo mimi sioni tatizo kuwa naye na
ninampenda hatari,” alisema Nisha.
Chanzo: GPL
Saturday, 10 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment