IGP Ernest Mangu.
WATU watano wa familia moja akiwemo mtoto wa miezi tisa, wameuawa kwa
kukatwa mapanga kutokana na ugomvi unaodaiwa kua wa mgogoro wa ardhi
katika kijiji cha Kisesa katika Kata ya Bugarama, wilayani Maswa, Mkoani
Simiyu.
Kamanda wa Polisi Mkoa Simiyu, Gemini Mushy amethibitisha, akisema
waliokufa papo hapo ni baba wa familia, George Charles (30), Siku John
(23) ambaye alikuwa mke wa George na watoto wao Nchambi George(7), Tuma
George (5) na Amos George mwenye umri wa miezi 9 wote waliuawa kwa
kukatwa mapanga sehemu zao za shingoni na watu wasiofahamika.
Alisema wauaji hao waliivamia familia hiyo saa 9:00 usiku wa Septemba
28 mwaka huu na kuwatendea unyama ambao chanzo kikisadikiwa kuwa ni
mgogoro wa ardhi kati ya marehemu na baba yake wa kambo ambaye alinunua
kipande cha ardhi alipokuwa akiishi marehemu.
Kamanda Mushy alisema kuwa katika tukio hilo jeshi hilo
linawashikilia watu watatu kuhusiana na mauaji hayo ambao ni Migata
Lusalago (50), Jihelya Migata (30) na Sollo Kengele (31) wote wakazi wa
kijiji hicho huku likiendelea kuwatafuta wahusika wengine ili wafikishwe
mahakamani.
Wakati huohuo, John Gagarini anaripoti kutoka Kibaha kuwa, watu
wawili wamekufa na wengine 33 wamejeruhiwa baada ya baada ya basi la
Ngorika kugongana uso kwa na basi dogo la abiria.
Akithibitisha jana, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Jafary Mohammed
alisema basi la Ngorika lilikuwa linaelekea Arusha kutoka Dar es Salaam.
Alisema ajali hiyo ilitokea eneo la Misugusugu wilayani Kibaha majira
ya saa 1:30 .
Created by Gazeti la HabariLeo.
Tuesday, 29 September 2015
Mahujaji 18 waliopotea Makka watambuliwa
By:
Unknown
On: 23:23
SIKU moja baada ya Serikali kutangaza kuwa mahujaji 50 wa Tanzania
waliokuwa katika Mji Mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia, hawajulikani
walipo tangu kutokea kwa tukio la kukanyagana na kusababisha vifo vya
watu 769, imesema imepokea majina 18 ya watu ambao hawajulikani walipo.
Katika tukio lililotokea eneo la Mina, nje kidogo ya Makka, Alhamisi iliyopita ambayo ilikuwa ya maadhimisho ya Sikukuu ya Idd el Haji, mahujaji watano wa Tanzania waliripotiwa kufa, na wengine kujeruhiwa.
Taarifa ya Serikali kwa vyombo vya habari jana, iliwataja mahujaji wa Tanzania ambao hawajaonekana kuwa ni Abdul Iddi Hussein, Awadh Saleh Magram, Burhani Nzori Matata, Yussuf Ismail Yusuf, Saleh Mussa Said, Adam Abdul Adam na Archelaus Antory Rutayulungwa.
Wengine ni Farida Khatun Abdulghani, Rashida Adam Abdul, Hamida Ilyas Ibrahim, Rehema Ausi Rubaga, Faiza Ahmed Omar, Khadija Abdulkhalik Said, Shabinabanu Ismail Dinmohamed, Salama Rajabu Mwamba, Johari Mkesafiri Mwijage, Alwiya Sharrif Salehe Abdallah na Hafsa Sharrif Saleh Abdallah Aidha, ilisema mbali ya taarifa za kupatikana kwa majina hayo, Wizara imepokea taarifa ya kutambuliwa kwa mwili wa mmoja wa Tanzania anayeitwa Hadija Shekali Mohammed wa kikundi cha Ahlu Daawa.
“Serikali ya Saudi Arabia imetoa picha za maiti za mahujaji waliokufa Makkah ambao wamehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti kwa ajili ya utambuzi. Hivyo, Ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission pamoja na vikundi vya mahujaji unaendelea na zoezi la kuzihakiki picha hizo ili kubaini kama zinalingana na sura za mahujaji wetu waliopotea.
“Pia Mamlaka ya Serikali ya Saudi Arabia imesema kuwa imechukua alama za vidole za mahujaji waliokufa ili wazilinganishe na zile walizozichukua Uwanja wa Ndege wakati mahujaji hao wakiingia nchini humo.
Wizara inaamini kuwa taarifa za alama za vidole zitakapotolewa zitasaidia sana kuwatambua mahujaji wetu,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Waanza kurejea Wakati huohuo, kundi la mahujaji 90 kati ya zaidi ya 3,000 waliokwenda Makka kuhiji kwa lengo la kutimiza moja ya nguzo kuu za Uislamu, wanatarajiwa kuwasili nchini leo alfajiri.
Idadi hiyo ya mahujaji ni wale ambao walipelekwa huko kupitia Taasisi ya Haji Caravan, wakati wengine wanatarajiwa kurejea nchini kesho na keshokutwa. Juzi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kupitia Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma, ilieleza kuwa mahujaji wa Tanzania ambao wapo salama, walimaliza ibada yao ya Hija Jumamosi iliyopita na juzi walitarajiwa kuanza safari ya kurejea nyumbani.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya mtandao akiwa Saudia, aliyekuwa Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage ambaye alishiriki ibada hiyo, alisema msafara huo wa watu 90 wa Taasisi ya Haji Caravan utafika leo alfajiri. “Sisi ambao tuko salama tutarejea nchini kesho (leo) alfariji. Tuko 90, ni wa taasisi moja, Haji Caravan. Lakini wengine watarudi Alhamisi na Ijumaa,” alieleza Rage.

NEC yavitoa hofu vyama wizi wa kura
By:
Unknown
On: 23:19
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jji Mstaafu, Damian Lubuva akizungumza na wanahabari juu ya mambo yahusuyo tume hiyo
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitoa wasiwasi vyama vya siasa kuwa hakutakuwepo na wizi na udanganyifu wa kura katika matokeo ya uchagauzi wa rais, wabunge na madiwani, utakaofanyika nchini kote Oktoba 25, mwaka huu.
Aidha, NEC imesema ipo tayari kushirikiana na wataalamu wa vyama hivyo kubaini vyanzo vya wizi wa kura, iwapo tatizo hilo litajitokeza na hivyo kuhakikisha haki inatendeka kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji mstaafu Damian Lubuva wakati wa mkutano wake na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu, aliokutana nao kupata ushauri na maoni ya taasisi hizo kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Alisema hadi kufikia sasa, vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo vimefanyika kampeni za kistaarabu. Lakini, alisema katika siku za hivi karibuni, baadhi ya vyama vimekuwa vikitoa kauli na matamshi yaliyovuka mipaka. Alisema NEC inavionya vyama hivyo kuacha mara moja tabia hiyo.
“Vipo baadhi ya vyama vya siasa na wagombea wao wamekuwa wakitumia muda mwingi kutoa lugha zisizofaa baada ya kunadi sera ya vyama vyao, vyama hivyo tumekutana navyo na kuwataka kuacha mara moja kampeni za aina hiyo,” alisema Jaji Lubuva.
Jaji Lubuva alisema Julai 27 mwaka huu, vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu, vilisaini mkataba wa maadili ya uchaguzi huo, hivyo ni wajibu wa vyama hivyo kuzingatia viapo walivyotoa katika maktaba huo.
Akifafanua, Jaji Lubuva alisema iwapo chama chochote hakina hoja ya kuzungumza na wananchi ni vyema kikawa kimya hadi siku ya uchaguzi Oktoba 25 mwaka huu. Aidha, Jaji Lubuva alivitaka vyama vya siasa kuacha tabia ya kuingilia masuala ya utawala ya tume hiyo, kwani kufanya hivyo vyama hivyo vitakuwa vikifanya kazi za tume hiyo na hivyo kuingilia masuala ya ndani ya kiutendaji ya taasisi hiyo.
Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi huo, Jaji Lubuva alisema mahitaji yote ya msingi ya uchaguzi huo tayari yamepokewa na NEC, ikiwemo karatasi, wino, na masanduku ya kura, ambapo baadhi yake yameanza kusafirishwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Akisisitiza juu ya kuamini utendaji wa tume, alisema haioni sababu ya vyama hivyo kuwa na wasiwasi na tume na kutaka kubaki vituoni kwa madai ya kulinda kura. Alisema matokeo ya uchaguzi mkuu, yatatangazwa kwa mujibu wa sheria na taratibu na mapema iwezekanavyo, tofauti na siku saba sheria inavyotaka, huku kukiwa na waangalizi 140 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) na wengine wa nje.
Waangalizi wa ndani watakuwa 75. Wapigakura wanatakiwa kurejea nyumbani mara tu baada ya kupiga kura na hawatakiwi kuendelea kukaa vituoni kwa madai kulinda kura. Aidha, alisema Tume imepokea taarifa ya vifo vya wagombea watano wa nafasi za udiwani na vifo vya wagombea wawili wa nafasi ya ubunge, ambapo uchaguzi katika maeneo hayo umeahirisha hadi Novemba 22 mwaka huu.
Alisema katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu, NEC imefanya uteuzi wa wagombea nane wa urais, wagombea 1,218 wa ubunge, kati yao wanaume wakiwa 985 na wanawake 233. Kwa upande wa udiwani ni 10,879, kati yao wanaume ni 10,191 na wanawake 679.
Akizungumzia walemavu wasioona, alisema watatumia kifaa maalumu cha ‘Tactile Ballot Folder’kupigakura, ambacho kitamwezesha mlemavu huyo kupiga kura yake mwenyewe bila kusaidiwa na mtu mwingine, hivyo kutimiza lengo la usiri wa kura kwa mpigakura.
Kuhusu daftari la kudumu la wapiga kura, Jaji Lubuva alisema katika kipindi cha siku 10 zijazo kuanzia sasa, Tume hiyo inatarajia kusambaza daftari la kudumu katika mikoa yote nchini na wananchi watatakiwa kuhakiki majina yao katika kipindi cha siku 8.

Msigwa, wengine 62 mbaroni
By:
Unknown
On: 23:16
Mbunge wa Iringa Mjini anayemaliza muda wake, Mchungaji Peter Msigwa.
WATU 62, akiwemo Mbunge wa Iringa Mjini aliyemaliza muda wake, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhusika kufanya fujo na kufunga barabara mjini hapa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi alitoa taarifa hiyo jana mkoani hapa kwa waandishi wa habari na kusema waliokamatwa, wanasadikiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Akieleza sababu za kumkamata Msigwa ambaye ni mgombea wa Jimbo la Iringa Mjini, Kamanda alisema yeye hakuwepo eneo la tukio, isipokuwa anatuhumiwa kutoa hamasa kosa lifanyike. “Katika kutenda makosa, hakuwapo pale katika eneo, lakini wakosaji wakuu wako katika makundi manne.
Kuna anayetenda makosa kwa mkono wake, kuna yule anayewezesha, kuna anayesaidia, hata mshauri au kutoa hamasa kwa watu kutenda makosa. Yeye ndiye huyo wa la nne,” alisema.
Akielezea tukio, Kamanda alisema juzi saa 12 jioni wafuasi hao walikuwa kwenye barabara inayotoka Iringa mjini kwenda eneo la Kihesa, wakiwa wamezuia barabara na kucheza katikati ya barabara.
Alisema akiwa katika mkutano wa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli, zilipatikana taarifa kwamba waendesha bodaboda zaidi ya 150, walikuwa wamekusanyika katika hoteli ya Sambala.
“Tukafuatilia kuona kwa nini wamejikusanya; tukafuatilia tukaona wako kwenye kikao chao cha ndani. Hatuna usumbufu na watu wanaofanya vikao vyao vya ndani kwani ni haki yao,” alisema Kamanda Mungi. Hata hivyo, alisema mkutano wao ulipoisha, wale watu walitoka na kuingia barabarani na kuanza kucheza wakizuia watu na magari kupita.
Alisema alimwagiza mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) akawaondoe watu hao barabarani. Kwa mujibu wa kamanda, Mkuu wa FFU alipotaka kuwaondoa kwa amani, walikaidi na alipojaribu kutumia nguvu, walianza kumrushia mawe na kukimbilia kwenye hoteli waliyokuwa wakifanyia mkutano.
Alisema FFU waliingia kwenye hoteli hiyo na kukamata baadhi; tukio ambalo lilisababisha wengine kuumia kutokana na kuruka ukuta na wengine kuanguka. Akitoa taarifa hizo jana mchana, Kamanda alisema walitarajia kufikisha watuhumiwa hao mahakamani wakati wowote.
Kamanda alionya vyama vya siasa na viongozi wake kuepuka vitendo vinavyoashiria kuhatarisha usalama. Alisema katika kipindi hiki cha nusu ya kampeni kuelekea siku ya uchaguzi, upo mhemko mkubwa wa kisiasa ikilinganishwa na siku za mwanzoni.
“Sasa hivi tuko karibu nusu ya muda wa kampeni. Kipindi cha awali, kimekwenda vizuri. Kwa mfano katika Mkoa wa Iringa, Kuanzia tarehe ishirini na mbili hadi tarehe thelathini mwezi wa nane hakuna kosa hata moja lililotendeka pale kuhusiana na kampeni,” alisema kamanda.
Alisema Septemba mosi hadi Septemba 5, yaliripotiwa makosa sita. Septemba 5 hadi 19, kulikuwa na makosa 17 ambayo kati ya hayo, ambayo kati yake, 15 yalitokea Iringa mjini na yaliyobaki ni ya Kilolo. Alisema kadri inavyoelekea katika uchaguzi, watu wanapata mihemko na kusahau kanuni ya maadili ya uchaguzi.
Aliwaomba viongozi wa siasa kuzingatia maadili, wawaelekeze na kuwaelimisha wafuasi wao wayafuate. “Tusipofanya hivyo, amani itavurugika. Sisi polisi Iringa hatutakuwa na huruma na chama chochote, mtu yeyote ambaye anaonesha dalili zozote za kuvuruga amani katika mkoa wetu wa Iringa,” alisema.
Alisisitiza, “sisi amani ni kipaumbele cha kwanza, mengine yote yatafuata. Yeyote anayetishia amani Iringa, anatishia kazi ya polisi, hatutamvumilia.” CCM yasikitishwa Naye Emmanuel Ghula, anaripoti kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeelezea kusikitishwa na kitendo cha wafuasi wa vyama vinavyounda Ukawa kupiga mawe, kurusha chupa na kuharibu ofisi za chama hicho mkoani Tanga juzi wakati wa kampeni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba, wafuasi wa vyama vinavyounda Ukawa ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, walisababisha uharibifu mkubwa katika ofisi za chama hicho mkoani Tanga wakati wa kampeni.
“Tunasikitika sana kwa wenzetu kukosa ustaarabu katika kampeni zao kwani mikutano yote ya CCM imekuwa ikifanyika katika hali ya amani, utulivu na ustaraabu,” alisema. Makamba alisema kampeni zimekuwa zikienda vizuri, lakini vijana wa vyama vinavyounda Ukawa wamekuwa wakisababisha uvunjifu wa amani katika mikutano ya CCM, lakini CCM wao wamekuwa wakiendesha kampeni zao kistaraabu.
Alisema ni lazima watanzania waelewe kuwa uchaguzi utapita na taifa litabaki, hivyo ni vyema wananchi wote hasa viongozi wa vyama vya siasa kuendesha kampeni zao kistaarabu pasipo kusababisha vurugu.
Creted by Gazeti la HabariLeo.

Mshikemshike
By:
Unknown
On: 02:36
* Tume ya Uchaguzi yakana tuhuma za Freeman Mbowe
* Dk. Magufuli asema CCM haiwezi kung’oka kama jino
* Lowassa aonya asema kuyakataa mabadiliko ni kujiandalia tabu
Na Waandishi Wetu
WAKATI zikiwa zimebaki siku 26 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, kampeni za wagombea urais zinaonekana kushika kasi katika mikoa mbalimbali nchini.
Wakati vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vikisema mwisho wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) umewadia, mgombea wa chama hicho Dk. John Magufuli amesema CCM haiwezi kung’oka madarakani kama jino.
Naye Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliibua tuhuma dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akisema kitendo cha wakurugenzi wa tume hiyo kuhamishwa ni mkakati wa kutaka kuibeba CCM.
Hata hivyo tume hiyo ya uchaguzi imekanusha madai hayo na kusema hakuna mtumishi wake aliyehamishwa kwa ajili ya kutaka kuhujumu uchaguzi wa mwaka huu.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Luvuba alisema hadi sasa hakuna mkurugenzi yeyote aliyehamishwa tofauti na mabadiliko yaliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete katika nafasi ya Mkurugenzi wa Uchaguzi kwa kumteua Julius Malaba kuwa jaji.
“Nakwambia ndugu yangu, Mbowe na Chadema waache kutapatapa…wanaingilia utendaji kazi wa tume na Serikali, nawaomba wasiendelee kupotosha umma.
“Hii si mara ya kwanza kuibuka na madai haya, wanazungumzia wizi wa kura kila siku, waiachie tume ifanye kazi zake, hakuna wizi wa kura wowote ule tunaongozwa na sheria za nchini,”alisema Jaji Lubuva.
“Nipo njiani natoka Arusha, nimekutana na wanasheria wa nchi jana (juzi) na pale alikuwapo kiongozi mmoja wa Chadema akawa anazungumzia malalamiko haya haya…nikamwambia ndugu yangu mbona hakuna kitu kama hicho.
“Pamoja na kulalamika hivyo, wenzake wa vyama NCCR-Mageuzi,CUF walikuwapo, jamani hatuna haya mambo, nawaomba tena wasiendelee kupotosha umma… si si mata ya kwanza kutoa madai haya,”alisema Jaji Lubuva.
Kuhusu madai ya Mbowe kwamba kuna kura feki ambazo zimeanza kusambazwa mikoani, Jaji Lubuva alisema hakuna kitu kama hicho.
“Kila siku nawasikia wanasema wanataka kulinda kura, huku ni kutapatapa tu…sasa sikia wanasema kuira zimepelekwa mikoani hakuna kitu hiki…nasema kwa kujiamini hakipo,”alisema.
Kauli ya Jaji Lubuva, imekuja muda mfupi baada ya Mbowe ambaye pia ni mgombea ubunge Jimbo la Hai, kuibua tuhuma hizo katika mkutano wa hadhara mkoani Kilimanjaro.
Katika madai yake, Mbowe alisema wakurugenzi wote katika tume ya uchaguzi wameondolewa na kuwekwa maofisa wengine kutoka taasisi za kijeshi kwa lengo la kutaka kuhujumu uchaguzi.
Mbowe
Akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Himo Polisi mkoani Kilimanjaro katika Jimbo la Vunjo, Mbowe alisema mbali na kubadilisha viongozi hao, lengo ni kuiba kura na tayari Serikali imeanza kutawanya kura kwenye mikoa mbalimbali nchini.
“Mtu mwenye wajibu wa kisheria wa kusimama uchaguzi ni NEC baada ya CCM kuona Lowassa (mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa), anashinda wameamua kuandaa mazingira ya kuchakachua tume yenyewe.
“Mkurugenzi wa Uchaguzi, Malaba (Julius) walianza kumwondoa yeye mwezi mmoja uliopita wakaleta mwingine, wiki mbili zilizopita wakurugenzi wote wamewang’oa na kuwaingiza wengine wa mwisho kuondolewa alikuwa mkurugenzi wa idara ya Tehama, inayoshughulika na daftari la kudumu la wapiga kura.
“Wameanza mkakati mwingine wa kutengeneza kura bandia na tayari zimepelekwa mkoani Kilimanjaro,” alisema Mbowe.
Hata hivyo, Mbowe alisema hakuna mkakati wowote ovu utakaopangwa na CCM bila wao kuujua kwa sababu kila wanachokipanga asubuhi, wao wanakipata mchana.
Alisema mabadiliko ambayo Ukawa unayapigania, yanamgusa kila Mtanzania bila kujali dini yake wala kabila lake hivyo ni vigumu mtu kujaribu kuyahujumu.
Alisema vingozi kama mgombea ubunge Jimbo la Vunjo, James Mbatia (NCC-Mageuzi), wana mchango mkubwa na kazi ya kuendelea kufanya kwa ngazi ya taifa ili kuhakikisha mabadiliko hayo yanatokea.
“Tumekuja hapa viongozi wote kwa sababu ya kazi kubwa anayofanya Mbatia kitaifa, mabadiliko tunayozungumza si kwa faida ya yake wala Lowassa ( Edward) ni kwa faida ya Watanzania wote,” alisema Mbowe.
“Nyie ni kati ya watu wachache mliyepata mgombea ambaye hata taifa linamhitaji, huu ni mwaka wa mabadiliko, mimi nilikuwa CCM, Lowassa na viongozi wengine wametoka ili kuleta mabadiliko, katika mfumo wa vyama vingi kama chama hakijatekeleza walichoahidi lazima kitoke madarakani,” alisema.
Msemaji wa JWTZ
Naye Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Ngamela Lubinga alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema hayana ukweli wowote.
“Siwezi kukupa majibu siko sehemu nzuri, lakini madai haya yalishatolewa ufafanuzi na tume yenyewe kupitia Elius Malima,”alisema Kanali Lubinga.
Lowassa naye anena
Kwa upande wake, mgombea urais wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa alisema ameamua kuwania nafasi hiyo kwa sababu anauchukia umasikini na CCM imeshindwa kulitatua kwa miaka 50.
“Miaka 50 ya CCM ni shida, nagombea urais kwa sababu nachukia umasikini, umasikini ni ujinga, siutaki, nitaanza na eneo la elimu,” alisema.
Akiwa Kahe, Lowassa alisema endapo wananchi watashindwa kufanya mabadiliko na kurudi kwenye maisha ya zamani itakuwa tabu kubwa.
Mbatia
Kwa upande wake,mgombea ubunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) pamoja na mambo mengine alizungumzia mdahalo wa wagombea urais.
“Mdahalo wanaoutaka CCM na lowassa si saizi yake, Dk. Magufuli aje kwangu nimtoe jasho, namwambia hata kama ni leo jioni aje kwangu nimtoe jasho. Yeye ni saizi yangu si saizi ya Lowassa,” alisema.
Akiwa Kahe, Mbatia aliwataka wananchi kutumia haki yao ya kupiga kura, kwani hiyo ni haki ya kila mwenye sifa za kufanya hivyo.
“Kama una haki ya kupiga kura, uwezo wa kupiga kura, usipopiga kura, huna haki ya kulalamika,” alisema Mbatia.
Katika hatua nyingine, Mbatia aliawaambia wananchi wa Kahe kuwa wakimchagua kuwa mbunge, ndani ya siku 14 atahakikisha hospitali ya kata hiyo inapata umeme.
Alisema suala hilo halihitaji kulisemea bungeni ama kuisubiri serikali ifanye hivyo bali ni jambo la kufanywa na mbunge pekee.
Dk. Magufuli
Naye Dk. Magufuli alibeza kauli za wapinzani akisema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakiwezi kung’oka madarakani kama jino.
Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake wa kampeni wilayani Mbarali mkoani Mbeya jana.
Alisema anashangazwa na watu wanaotaka CCM ing’oke madarakani na kueleza kuwa chama hicho hakiwezi kung’oka kirahisi, kwani kina mizizi kuanzia ngazi ya kijiji.
“Eti kuna watu wanapitapita mitaani wanasema CCM imechoka, lazima ing’oke madarakani.
“Ehee wakae wakijua CCM haiwezi kung’oka kama jino…ndivyo walivyoamua Watanzania wakae wakijua,” alisema.
Kuhusu mgogoro wa shamba la Kapunga kati ya mwekezaji na wananchi, Dk. Magufuli ameahidi kulirudisha shamba hilo kwa wananchi iwapo atachaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano.
Alisema suala hilo ni kipaumbele chake cha kwanza kama akishinda urais na kuingia madarakani.
Alisema anatambua namna wananchi wanavyohangaika kwa kukosa mahali pa kuendeshea shughuli za kilimo, wakati mwekezaji kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wamemega ardhi ya wananchi.
Alisema katika ubinafsishaji wa shamba hilo, mwekezaji alitakiwa kupewa ekari 5,000 na badala yake amepewa ekari 7,000 kinyume cha utaratibu.
Alisema mgogoro huo umechukua muda mrefu, kwani aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Modestus Kilufi alishindwa kuwasilisha hati za mashamba hayo serikalini ili hatua stahiki zichukuliwe.
Baada ya kushindwa kura za maoni, Kilufi alijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambako alikaa kwa siku tano, kisha kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo na kuteuliwa kugombea ubunge wa Mbarali.
Alisema hayuko tayari kuongoza nchi na kuona wananchi wake wakikosa eneo la kuendeshea kilimo kwa ajili ya masilahi ya mwekezaji.
“Natambua Igurusi na Mbarali, mmekuwa na kilio kikubwa kuhusu shamba la mpunga la Kapunga, mwekezaji badala ya kupewa ekari 5,000 amepewa zaidi ya ekari 7,000.
“Tena katika ekari hizi, zipo 1,800 ambazo ni mali ya wananchi, ninasema kama mtanichagua nitatumia sheria namba 4 ya ardhi na sheria namba 5 ya vijiji zote za mwaka 1999, nitafuta hati za shamba hili na kurudisha kwenu wananchi.
“…unapokuwa rais wa nchi kwa mujibu wa sheria, ardhi yote inakuwa chini yako, nami nasema hapa nitaifuta hati hii mchana kweupe kikubwa ninawaomba mnichague,” alisema Dk. Magufuli.
Kuhusu askari wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA) katika Bonde la Ihefu kuwapiga wananchi na kuwafukuza, Dk. Magufuli alisema suala hilo halitatokea katika uongozi wake.
Created by Gazeti la Mwananchi.

Chekechea, shule za msingi waletewa shindano
By:
Unknown
On: 02:34
NA ASIFIWE GEORGE
SHINDANO jipya la ‘Graph Game’ litakalochezwa kwa kutumia simu za mkononi kwa lengo la kuleta tija na mabadiliko na maendeleo katika jamii kwa vizazi vijavyo limezinduliwa nchini.
Shindano hilo litakalowashirikisha watoto kuanzia chekechea hadi shule ya msingi, mwisho wa usajili wake ni Oktoba 22 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya simu ya Tigo, Diego Gutierez, ambao ndio waandaaji wa shindano hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya Reach for Change, alisema lengo la shindano hilo ni kuwasaidia na kuinua vipaji kwa vijana wenye mawazo bunifu yanayolenga kuboresha maisha ya watoto.
Naye Mkurugenzi wa Reach for Change, Peter Nyanda, alisema shindano hilo pia litasaidia kupata wajasiriamali watakaowapatia dola 20 kwa ajili ya kutengeneza miradi yao.

Christina: Ninawasiliana na Lil Wayne japo tumeachana
By:
Unknown
On: 02:31
ALIYEKUWA mpenzi wa msanii wa hip hop nchini Marekani, Lil Wayne,
Christina Milian, amesema bado ana mawasiliano mazuri na mpenzi wake wa
zamani. Wawili hao walikuwa na uhusiano tangu mwaka jana, lakini Agosti
waliachana. “
Mimi na Lil Wayne bado tunawasiliana lakini hatuna uhusiano wa kimapenzi tena kama ilivyo miezi michache iliyopita, kwa sasa tumekuwa na urafiki mkubwa na watu wanadhani kama tuna uhusiano mpya,” alisema Christina. Wawili hao wanatarajia kufanya video ya wimbo mpya wa mrembo huyo aliomshirikisha Lil Wayne.

Nana wa Diamond wamdatisha Swizz Beatz
By:
Unknown
On: 02:29
NA CHRISTOPHER MSEKENA
RAPA na prodyuza wa muziki duniani, Kasseem Dean maarufu kwa jina la
Swizz Beat, ameonekana kuvutiwa na nyimbo mbili za msanii, Diamond
Platnumz.
Staa huyo anayeishi Marekani ameweka vipande vya video katika kurasa zake za mitandao ya kijamii ikimuonyesha akisikiliza na kucheza nyimbo za Diamond ‘Nataka Kulewa’ na ‘Nana’ huku akiandika ujumbe kwamba anafurahia midundo ya Afrika.
Hii siyo mara ya kwanza kwa prodyuza huyo wa muziki kusikiliza nyimbo za Afrika, ameshaonekana akisikiliza na kucheza wimbo wa msanii wa Nigeria, Wizkid huku ujumbe wake ukiwa ni kwamba anapenda midundo ya Afrika ndiyo maana anasikiliza.

NEC yajikanganya
By:
Unknown
On: 02:27
*Mkurugenzi Tehama aondolewa
* Maofisa watoa kauli tofauti
NA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM
MKURUGENZI wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Sisti Cariah ameondolewa kwenye nafasi hiyo, imefahamika.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya NEC ambazo MTANZANIA ilizipata juzi na jana zimeeleza kuwa mkurugenzi huyo ambaye ni mtu muhimu katika Tume ameondolewa katika siku za karibuni huku kukiwa hakuna taarifa ya wapi alikohamishiwa serikalini.
Chanzo hicho cha ndani ya tume kimesema mkurugenzi huyo ameondolewa siku tano zilizopita huku zikiwa zimesalia siku 25 tu kufikia Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 wakati idara hiyo ya Tehama ikiwa ndiyo ina orodha nzima ya Watanzania wanaotarajiwa kupiga kura.
“Ni kweli mkurugenzi huyo wa Tehama ameondolewa na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa msaidizi wake (bila kumtaja) na nafasi nyingine zinaendelea kusukwa upya.
Hadi jana tovuti ya Tume hiyo hadi ilikuwa ikionyesha kuwapo mkurugenzi mmoja tu ambaye ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima, huku ukiwapo unaosomeka kwamba kurugenzi nyingine zinaendelea kusukwa upya.
Tume hiyo ina kurugenzi saba ambazo ni Elimu ya mpiga kura na habari, Uchaguzi, Ununuzi, Uhasibu, Ukaguzi, Utawala na Tehama.
MTANZANIA lilipomtafuta Mkuu wa Kitengo cha Habari wa NEC, Clarence Nanyaro kupata ufafanuzi wa suala hilo alisema:
“Ndugu yangu hakuna mkuu yeyote wa idara aliyehamishwa hadi sasa lakini ngoja nifuatilie zaidi nitakupa jibu zuri kwa kutumia simu ya mezani.”
Baada ya dakika chache alipiga simu lakini aliendelea kusisitiza kwamba anaamini idara hizo hazijafanyiwa marekebisho.
Hata hivyo alisema hazisimamiwi na wakurugenzi bali zinasimamiwa na wakuu wa idara.
“Watu wengi wamekuwa wakiwaita wakuu wa idara hizo kama wakurugenzi jambo ambalo si sahihi na hata hivyo wote bado wapo,” alisema Nanyaro na kuongeza:
“Sina taarifa za kuhamishwa Dk. Cariah kwa kuwa hadi jana (juzi) alikuwa kazini akiwajibika hadi saa nne usiku tulipoachana.
Alipoulizwa kuhusu tovuti ya NEC kuwa na ujumbe unaoonyesha kufanyika marekebisho ya wakuu wa kurugenzi zote saba, alisema suala hilo aulizwe Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima kwa kuwa ndiye mwenye mamlaka ya kuzungumzia wafanyakazi wa Tume.
MTANZANIA lilipomtaka asaidie kupata jibu hilo kutoka kwa bosi wake huyo alisema kwamba wakati huo mkurugenzi huo alikuwa kwenye mkutano na wawakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU). Aliahidi kutoa jibu baadaye kama angeonana na Kailima na kukata simu.
Baadaye Nanyaro alipiga tena simu na kusema kwamba taarifa zilizokuwa zikielezea mabadiliko ya viongozi wa kurugenzi za Tume zilitokana na viongozi hao saba kutowasilisha picha zao kwa ajili ya kuziingiza taarifa hizo kwenye tovuti.
“Napenda kusema wakurugenzi wote saba wapo kazini; katika Idara ya elimu ya mpiga kura na habari, Uchaguzi, Ununuzi, Uhasibu, Ukaguzi na Utawala akiwamo Dk. Cariah wa Tehama ambaye alikuwa kazini hadi juzi na alitoka muda wa saa nne usiku,” alisema Nanyaro.
Kauli ya Jaji Lubuva
Wakati Nanyaro akisema hivyo, juzi Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, alipoulizwa na Mtanzania alikiri kuwa Mkurugenzi huyo wa Tehama, Dk. Cariah, amehamishwa.
Hata hivyo dakika chache baadaye Jaji Lubuva alipiga simu kwa mhariri wa gazeti hili akikanusha taarifa yake hiyo ya awali akisema hakuna mkurugenzi yeyote aliyehamishwa katika Tume yake tofauti na mabadiliko yaliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete katika nafasi ya mkurugenzi wa uchaguzi iliyokuwa inashikiliwa na Julius Malaba ambaye aliteuliwa kuwa jaji hivi karibuni.
“Nakwambia ndugu yangu, Mbowe na Chadema waache kutapatapa, wanaingilia utendaji wa Tume na serikali nawaomba wasiendelee kupotosha umma, ” alisema Jaji Lubuva.
Alichosema Mbowe
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Himo Polisi mkoani Kilimanjaro juzi, Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Freeman Mbowe aliituhumu Serikali kwa kile alichokiita uchakachuaji wa NEC kwa kubadilisha wakurugenzi wote na kuweka wapya kutoka idara nyeti za usalama.
Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) alidai viongozi hao wa Tume wameondolewa na serikali lengo likiwa ni kuiba kura.
“Mtu mwenye wajibu wa sheria wa kusimamia uchaguzi ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi, baada ya CCM kuona Lowassa (Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa), anashinda wameamua kuandaa mazingira ya kuchakachua Tume yenyewe.
“Walianza kumuondoa Mkurugenzi wa Tume Malaba (Julius) mwezi mmoja uliopita katika mazingira ya kutatanisha wakaleta mwingine, wiki mbili zilizopita…. wakurugenzi wote wamewang’oa na kuwaingiza wengine.
“Tume kwa sasa siyo huru huku Serikali ya CCM pia ikiingiza wanajeshi kwenye tume hiyo. Namuuliza Mkuu wa Majeshi atueleze hao wanajeshi huko wameenda kufanya nini?” aliuliza Mbowe
Mbowe alisema pia kuwa CCM imeanza mkakati mwingine wa kutengeneza kura bandia na tayari zimepelekwa mkoani Kilimanjaro, Mamlaka ya Barabara (Tanroads) ambayo iko chini ya Magufuli ndiyo inasambaza kura hizo,” alidai Mbowe.
Mwenyekiti mwenza huyo wa Ukawa alisema hakuna mkakati wowote ovu utakaopangwa na CCM bila Umoja huo kuujua kwa sababu kila inachokipanga asubuhi wao wanakipata mchana.
“Mnaopanga nao mchana, usiku tunakuwa nao. Kikwete wewe ni rais wa nchi usifikiri una usalama sana kama utaharibu uchaguzi wa nchi hii. Watanzania ndiyo wataamua, Kikwete na familia yako hamtatuchagulia mtu, tumia majeshi, tumia vyote unavyotaka, tutapiga kura na kuzilinda kwa gharama yoyote… nimesema haya nitoe onyo kwa CCM,” alisema Mbowe.
Akiwa kwenye mkutano wa kampeni katika Kata ya Kahe kwenye Viwanja vya Shule ya Oria, Mbowe alisema kila mtu atakayejaribu kuzuia mabadiliko na kuwa wakala wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu ya masilahi binafsi, mafuriko yatamkumba.
“Mabadiliko tunayozungumzia hapa yako kwa vyama vyote, mtu yeyote atakayekuwa wakala wa kuitetea CCM kwa sababu ya ubinafsi mafuriko lazima yamkumbe, tuna kila sababu ya kupigania mabadiliko,” alisema Mbowe.
Alisema mabadiliko ambayo Ukawa unayapigania yanamgusa kila Mtanzania bila kujali dini yake wala kabila lake hivyo ni vigumu mtu kuyahujumu.

Msajili anapobainisha hofu ya kuibiwa kura kwenye uchaguzi.
By:
Unknown
On: 02:24
Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Fransis Mutungi.
WATANZANIA wametakiwa kujiandaa kisaikolojia kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi mkuu ujao bila hofu kwa kuwa kura zao zitakuwa salama. Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na gazeti hili jijini Mwanza hivi karibuni, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi anasema wapiga kura hawapaswi kuwa na hofu kwa kuwa uchaguzi utafanyika kwa usalama.
“Yamezuka maneno kutoka kwa watu wasioitakia mema nchi wakiwatisha wananchi kuwa kura zao zitaibiwa, nitumie fursa hii kuwaeleza Watanzania kuwa kamwe kura zao hazitaporwa, zitakuwa salama”, anasema Jaji Mutungi.
Anafafanua kuwa Uchaguzi Mkuu unafanyika kwa kuzingatia sheria ambapo Tume ya Uchaguzi (NEC) imepewa dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sheria za uchaguzi na kuhakikisha unafanyika kwa kuzingatia haki ili kutimiza demokrasia. “Pia Jeshi la Polisi limepewa dhamana ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na lina jukumu la kulinda kura,” anasema. Anawataka kuondoa hofu na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi na NEC wana jukumu zito na la kisheria la kulinda kura hadi matokeo ya uchaguzi yatakapotangazwa. “
Tusitake kuwaaminisha Watanzania kuwa vyama visivyoweka vikosi vyao vya ulinzi vitaibiwa kura”, anasema Mutungi. Anasema kwa siku za hivi karibuni baadhi ya vyama vya siasa viliamua kujiundia vikundi vyao vya ulinzi kwa lengo la kujilinda, ambapo anakiri baadhi ya vikundi hivyo hivyo vipo kwa mujibu wa kanuni na taratibu za vyama vyao, lakini vimeonesha mwelekeo wa ukiukwaji wa Katiba ya nchi.
Anasema hii ni baada ya vyama hivyo, kuamua kutoa mafunzo makubwa mazito kwenye vikundi vyao hivyo vya ulinzi mithili ya yale yanayotolewa kwenye majeshi ya ulinzi katika nchi yetu. Mutungi anasema ingawa baadhi ya vikundi vya vyama hivyo vipo kwa mujibu wa Katiba za vyama vyao vinapofundishwa mafunzo ya kijeshi vinakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 147 inayoeleza kuwa mamlaka pekee yenye uwezo wa kuanzisha vikosi vya ulinzi ni Serikali.
“Hakuna Chama cha siasa, wala mtu yeyote wala kikundi chochote chenye mamlaka hayo, isipokuwa Serikali peke yake”, Jaji Mutungi anasisitiza. Anasema ukweli bado unabaki kwamba hata kama kuna taasisi au kikundi cha watu au chama kitakachoanzisha kikosi chenye mwelekeo wa kijeshi, kikundi hicho bado kitakuwa ni batili hata kama ilani na sera za baadhi ya vyama vya siasa zinaelekeza kufanyika kwa mafunzo hayo.
Anasema ofisi yake ilishaanza kulishughulikia suala hilo, ambapo anasema ilishatolea ufafanuzi wa hoja hiyo kwa vyama vyote vya siasa nchini. Amewataka Watanzania na viongozi wa vyama vya siasa nchini kutolifanyia mzaha jambo hilo la uundaji wa vikundi hivyo vya ulinzi wa kuwa vinaweza kutumika vibaya na kuvuruga amani ya nchi. Amevitaka vyama vya siasa kujifunza kutoka nchi jirani za Kongo DRC na Burundi kutokana na machafuko waliyoyapata baada ya kuunda vikundi vya aina hiyo.
“Nchi jirani kama Congo zilipata machafuko kwa sababu ya vikundi vya kijeshi ambavyo awali vilipuuziwa katika nchi hizo na baadaye zilisababisha matatizo makubwa”, anasema Jaji Mutungi. Anavitaka baadhi ya vyama vya siasa kuacha kuhubiri sera zao huku vikitishia kuwepo kwa umwagaji damu kwa vitisho hivyo itasababisha wananchi wengi wasijitokeze kupiga kura Oktoba 25 mwaka huu.
“Vyama vinavyojikita kwenye lugha za vitisho wakati huu wa kampeni, ikiwemo hoja ya umwagaji wa damu, kama njia ya kupeleka vitisho kwa wananchi itasababisha wasijitokeze kupiga kura”, Mutungi anaeleza. Anasema Tanzania imekuwa na tatizo la wananchi wake kutoelewa kwa mapana mambo mengi ya demokrasia na siasa kutokana na elimu ya uraia nchini kutowekewa mkazo.
“Hii tumeiona katika kipindi hiki, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaendesha kampeni siziso za kistaarabu, huku baadhi yao kwa sababu ya kutokuwa na elimu ya uraia, wanaamini ndizo zinazohitajika”, anaeleza. Ili kuondokana na tatizo hilo Jaji Mutungi anapendekeza elimu ya uraia kutolewa mashuleni kuanzia madarasa ya chini ya shule za msingi na sekondari ili kuanza kuwajengea watoto uzalendo wa kuipenda na kuifahamu vizuri nchi yao.
Anasema elimu hiyo ikiboreshwa na ikafundishwa kwa vijana wa Kitanzania itasaidia kuwajengea uwezo vijana wa Kitanzania kuifahamu vyema nchi yao na wakati mwingine kuwa tayari kuitetea kwenye mambo ambayo yanaweza kuhatarisha amani. Anaiomba Serikali ihakikishe kuwa inaboresha mitaala hiyo ili kujenga uelewa kwa wananchi kwa kuimarisha demokrasia na kufanya siasa za kistaraabu kwa kuzingatia utamaduni wa Mtanzania, uelewa mpana wa demokrasia na ujenzi wa uzalendo wa nchi.
“Watoto wetu leo hii wanaishia kuangalia picha za nchi za Magharibi runingani, ni rahisi mtoto kukuambia Rais wa Marekani anaitwa nani kuliko kumuelezea Rais wa nchi yake, hii ni kwa sababu elimu yetu ya uraia bado haijawekewa mkazo wa kutosha”, anaeleza. Anasema elimu ya uraia itakayotolewa izingatie mazingira na utamaduni halisi wa Mtanzania ikiwa ni pamoja na kuwajenga vijana wa kitanzania kwenye maadili ya kuthamini utu na tabia njema.
Mutungi amewataka wananchi, vyama vya siasa, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wanasiasa kutambua kuwa wana jukumu kubwa la kuidumisha na kuienzi amani iliyopo nchini ili uchaguzi wa mwaka huu uwe wa huru na haki. “Tusikubali kuingia kwenye mitego ambayo inasababisha machafuko ya kisiasa kama ambavyo tumeona kwenye nchi nyingine ambazo sasa zinatumia gharama kubwa kurudisha amani…. sisi kazi yetu ni kuimarisha na kuboresha amani tuliyo nayo maana ndiyo msingi wa mambo yote, ikitoweka hata uchaguzi wa mwaka huu hautafanyika,” anasema Mutungi.
Anasema makundi hayo yakiicha amani itoweke yatambue kuwa haiwezi kununuliwa sehemu yoyote ile duniani bali baadaye hutafutwa kwa gharama kubwa kwa kutumia fedha za walipa kodi kujenga miundombinu itakayokuwa imeharibiwa kwa sababu ya kutoweka kwa amani. “Mtu anaweza kununua chakula lakini hawezi kununua hamu ya kula chakula, hivyo ndivyo ilivyo kwenye suala la amani pia”, anasema.
Anawataka Watanzania kutokubali kulishwa sumu za jazba ili wavuruge amani nchini, bali wahakikishe kuwa amani iliyopo hapa nchini inalindwa na kuenziwa. Anasema baadhi ya watu hapa nchini wamekuwa wakitumia kuwepo kwa migogoro wakiifananisha na kuvunjika kwa amani, ambapo anasema migogoro ni sehemu ya kawaida ya binadamu.
“Kuwepo kwa migogoro ndani ya ndoa haimaanishi sasa ndoa haipo, migogoro imekuwepo na ndoa zimeendelea kudumu”, anasema na kuongeza kuwa jukumu la kutafuta amani sio la Msajili wa vyama vya siasa peke yake bali ni la kila mtu katika jamii, Polisi, NEC na wananchi. Anasema wananchi nao wana nafasi kubwa ya kulinda amani wakati wa uchaguzi kutokana na wao kuwa na kura ya maamuzi ya kuwachagua viongozi wanaowataka wao.
“Leo hii Watanzania wakisema chama kinachofanya fujo hatukipi kura, hakuna chama au mwanasiasa atakayefanya fujo”, anasema. Anawataka wandishi wa habari na vyombo vyao wafanye kwa kuzingatia weledi na maadili ya utendaji kazi wao, lakini visijihusishe kwa namna yoyote katika kukuza migogoro nchini hasa wakati huu wa uchaguzi mkuu.
“Migogoro ikitokea vyombo vya habari visichochee bali viandike taarifa za kuhamasisha amani ili wananchi wapate fursa ya kushiriki kwenye shughuli za uzalishaji”, Mutungi anasisitiza. Anasema ofisi yake itaendelea kufanya kazi kwa usawa ikitoa elimu kwa vyama vyote vya siasa ili kila chama kiweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Mwakyembe: Lowassa ndiye Richmond
By:
Unknown
On: 02:22
Dk Harison Mwakyembe akihutubia wananchi mkutano wa hadhara. |
MJUMBE wa timu ya kampeni ya CCM, Dk Harrison Mwakyembe, amesema sakata la kashfa ya Richmond, haliwezi kuachwa kuzungumzwa na wanaCCM kwa kuwa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa ameanza kusingizia watu wengine kuhusika na kashfa hiyo, jambo ambalo alisema haliwezi kuachwa lipotee bila kujibiwa.
Aliyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Ubungo jana, mkutano uliokwenda sambamba na kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Dk Didas Massaburi. “Unaposema kuna wakubwa juu waliamuru Mkataba wa Richmond usivunjwe maana yake unamsema Rais wa nchi.
Katika suala lile hakuna rais wala nani, mhusika mkuu ni Lowassa na alifanya hivyo kwa uroho tu wa kutaka kujipatia fedha na upo ushahidi wa maboksi mawili. “Tulimpa masharti mawili; Kwanza ajipime kutokana na ushahidi uliopatikana wa yeye kushiriki. Pili ilikuwa ni kwa Bunge kuthibitisha ushiriki wake endapo angegoma.
Alichofanya ni kuamua kujiuzulu ili kukwepa aibu. Sasa katika hili rais anatokea wapi au anaposema alionewa ni katika lipi?” Alihoji. Akizungumzia kutofuatana na Dk Magufuli katika mikutano yake kuzungumzia kashfa ya Richmond na kuachia makada wengine kuzungumzia suala hilo, Dk Mwakyembe alisema ni kutokana na wajumbe 32 wa Kamati ya Kampeni kuwa na majukumu katika maeneo mbalimbali nchini.
“Wale wajumbe 32 tumegawanyika katika maeneo mbalimbali, na kila mtu anaonana na wananchi kwa njia na staili tofauti lakini lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa CCM inaibuka na ushindi wa kishindo. Hata kama wajumbe wote 32 tukifuatana na Dk Magufuli hatuwezi kuzungumza wote kutokana na muda,” alisema.
Akimnadi Dk Masaburi, Dk Mwakyembe ambaye pia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Kyela na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alisema mgombea huyo wa ubunge katika Jimbo la Ubungo kupitia CCM ni aina ya wachapakazi ambao wanahitajika katika uongozi ujao wa Dk Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo.
“Jimbo la Ubungo ni jimbo la kimkakati kutokana na umuhimu wake. Kwanza ni Jimbo la viwanda, pili ni lango la Jiji na hivyo ni sura ya Dar es Salaam, lakini tatu ni Jimbo la Elimu ya Juu kutokana na kuwepo kwa Chuo Kikuu na Chuo cha Usafirishaji. Dk Masaburi ni aina ya mbunge anayehitajika kuliongoza ili kulifanya Taifa kulitendea haki,” alisema.
Created by Gazeti la HabariLeo.
Serikali kufuta sheria kandamizi
By:
Unknown
On: 02:19
Raisi Jakaya Kikwete akiwasilisha hotuba kuhusu Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa
Mwanamke katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,
jijini New York, Marekani jana.
TANZANIA imeahidi kuchukua hatua tano muhimu za kutetea na kuendeleza haki za wanawake kati ya sasa na mwaka 2030, ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko makubwa ya kufuta sheria zinazokandamiza wanawake.
Badala yake itatunga sheria za kuleta usawa wa kijinsia, yote katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG) mapya kwa manufaa ya wanawake wa Tanzania. Miongoni mwa hatua hizo itakuwa ni pamoja na kufuta ama kufanya mabadiliko ambayo yanaendeleza vitendo vya kiutamaduni ambavyo vinaendeleza ubaguzi wa wanawake kama vile Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971, Sheria ya Urithi na kutunga Sheria ya kukomesha ukatili dhidi ya wanawake.
Msimamo huo wa Tanzania umeelezwa mwishoni mwa wiki na Rais Jakaya Kikwete alipozungumza katika Mkutano wa Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Akinamama: Dhamira ya Kuchukua Hatua uliohudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali duniani kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York, Marekani.
Rais Kikwete ameuambia mkutano huo ulioitishwa kwa pamoja na China, Denmark, Mexico na Kenya kuwa hatua ya pili ambayo Tanzania inakusudia kuchukua ni kuridhia makubaliano yote ya kimataifa kuhusu haki za akinamama hasa Makubaliano ya Kimataifa Juu ya Kukomesha Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW).
Hatua nyingine ambazo Rais Kikwete amesema Tanzania itachukua katika miaka 15 ijayo ili kuhakikisha usawa wa kijinsia pamoja na kuendeleza na kuunga mkono upatikanaji wa rasilimali fedha.
Rasilimali hizo zinazolenga kuongeza usawa wa kijinsia kwa mujibu wa Ajenda ya Kugharimia Maendeleo ya Addis Ababa, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha zinatolewa pesa za kutekeleza mipango ya kitaifa na ya Serikali za Mitaa za kukomesha ukatili dhidi ya wanawake.
Itahakikisha pia utekelezaji wa uwakilishi wa uongozi wa asilimia 50 kwa 50 kati ya wanawake na wanaume katika nafasi zote za maamuzi kwenye ngazi zote.
Created by Gazeti la HabariLeo

Magufuli kuondoa kauli za ‘njoo kesho’ serikalini
By:
Unknown
On: 02:17
Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli.
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli ameendelea kueleza msimamo wake wa kutaka Tanzania yenye viwanda kwa kusisitiza kuwa hatakubali kuwepo kwa urasimu kwa watu wanaotaka kuwekeza nchini.
Amekemea pia utaratibu wa baadhi ya watumishi serikalini kuwazungusha watu wanaotaka kuwekeza kwa kauli za ‘njoo kesho’ akisema, katika uongozi wake, hataruhusu vitendo hivyo.
Akihutubia umati wa wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Samora, mjini Iringa, Magufuli alisema atakapoingia madarakani, atataka kuona kiwanda cha usagishaji cha NMC cha mjini Iringa kinafanya kazi mara moja.
“Nataka serikali ya wachapakazi,” alisema na kumuita mwekezaji mzalendo wa kiwanda cha ASAS, Salim Abri, huku akisisitiza kwamba, nchi inahitaji wawekezaji wanaotengeneza ajira kama huyo.
Akizungumzia mafanikio ya serikali yake, Magufuli alimsuta Mchungaji Peter Msigwa (Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chadema aliyemaliza muda wake) kutokubali kusema ukweli juu ya mafanikio yaliyopo Iringa.
“Lakini leo mchungaji, tena mchungaji wa bwana, mchungaji wa kondoo anasema hakuna chochote,” alisema Magufuli na kutaja maeneo kadhaa yanayodhihirisha maendeleo ya nchi ikiwamo, huduma za mawasiliano, barabara na ujenzi wa nyumba bora.
Alihoji wanaodai hakuna chochote kilichofanyika, wanashindwa kuona hata suala la amani kuwa pia ni sehemu mafanikio? “Shukurani ya punda ni mateke,” alisema. Magufuli aliendelea kusisitiza msimamo wake juu ya uwajibikaji na kusema, kwenye kazi hatokuwa na blabla.
Akizungumzia maslahi ya wafanyakazi, mgombea huyo wa urais alisema, lengo ni kuhakikisha kila anayefanya kazi vizuri, anafaidi badala ya kuwapo tofauti kubwa ya mishahara. Alisema ndiyo maana imeundwa tume ya kupitia mishahara ili wafanyakazi wanaofanya vizuri wanufaike na siyo kuhangaika na mwisho wa siku, kuichukia serikali yao.
Alisema utaratibu wa watu wachache wanaopata fedha za rushwa na kudhulumu watu wa chini, kuharibu eneo moja na kuhamishiwa lingine, hataukubali katika serikali yake kama ataingia madarakani.
Mgombea urais huyo alisisitiza kwamba anataka kuleta mabadiliko ikiwa ni pamoja na kutekeleza ilani ya chama inayotaka zitengenezwe ajira asilimia 40. Kwa upande wake, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia mkutano huo, alisema Watanzania hawataki Rais wa majaribio Nape ambaye alisema CCM siyo chama kinachoongozwa na malaika, alikiri kuwa kina upungufu wake lakini pia kina mambo mengi mazuri

Mahujaji 50 kutoka Tanzania wapotea
By:
Unknown
On: 02:15
Mufti wa Tanzania, Shekhe Abubakar Zuberi Ally. |
WAKATI Waislamu kote duniani wakiwa katika simanzi kuu kutokana na vifo vya mahujaji zaidi ya 700 katika mji mtakatifu wa Makka, Saudia Arabia, imethibitika kuwa zaidi ya mahujaji 50 wa Tanzania, hawajulikani walipo.
Aidha, idadi ya mahujaji wa Tanzania waliokufa katika tukio la kukanyangana katika mji huo mtakatifu, imefikia watano, baada ya mtu mmoja zaidi kuthibitika kufa na mwingine kupatikana akiwa majeruhi.
Kutokana na ongezeko hilo la vifo, idadi ya Watanzania waliokufa wakiwa katika ibada ya Hijja, moja ya nguzo kuu ya Kiislamu, sasa imefikia watu watano. Hayo yamethibitishwa jana na Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakari Zuberi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoituma akiwa Makka.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa “Bakwata kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia, tumepata taarifa kwamba maiti mmoja amepatikana, ametambulika kwa jina la Shafi Khamisi Ali. Pia Nasra Nassor Abdallah amepatikana akiwa amepata majeraha. Mwenyezi Mungu atawapa tahfif Insha Allah.
“Kadhalika tumepokea taarifa ya kutopatikana kwa Watanzania 50 ambao walikuwapo Makka wakati wa tukio hilo. Kati yao 30 walisafiri kupitia taasisi ya Ahlu Daawa, taasisi ya Khidma watu 17 na TCDO watu watatu.”
Taarifa ya Mufti Zuberi imekuja ikiwa ni mwendelezo wa taarifa juu ya tukio la kuhuzunisha, lililotokea wiki iliyopita huko Mina, Saudi Arabia, ambako mahujaji zaidi ya 700 walikufa na wengine kujeruhiwa wakati wakielekea kwenye Jamaraat, ambapo palitokea msongamano mkubwa.
Alisema anatambua uwepo wa mkanganyiko wa taarifa, ambazo zinazidisha taharuki kwa ndugu na jamaa wa mahujaji. Hata hivyo, aliwaomba Waislamu kuwa na moyo wa subira, kwani juhudi za kuwatafuta mahujaji wengine zinaendelea.
Aliwaombea dua wale waliotangulia mbele ya haki na Mwenyezi Mungu, apokee ibada zao, awasamehe madhambi yao na awakusanye katika kundi la waja wema peponi. “Kutokana na mtihani huu kwetu sote, nawaombea dua wafiwa Mola awape subra na ustahmilivu na kuwaombea wagonjwa wapate tahfif.
Pia nawaomba Waislamu wote Tanzania kuwaombea dua waathirika wa mtihani huu. “Mwisho nichukue fursa hii kuwaomba wale wote wenye nafasi ya kuwafariji na kuwasaidia wanafamilia, ambao katika ajali hii wameondokewa na nguzo katika familia hizo wafanye hivyo.
Tuwasaidie wanafamilia hawa kwa hali na mali katika wakati huu mzito sana kwao ili tuwapunguzie majonzi na unyonge walionao,” ilisema taarifa hiyo ya Mufti. Mufti aliushukuru Ubalozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia.
Alisema wanaendelea kushirikiana na ubalozi huo na vyombo vya serikali ya Saudi Arabia. Alisema maofisa wa Bakwata waliopo Makka, wanaendelea kufuatilia habari na taarifa za mahujaji wa Tanzania kwa umakini mkubwa.
Tukio hilo limetajwa kuwa baya zaidi kutokea wakati wa Hijja katika kipindi cha miaka 25 iliyopita. Iran imepoteza zaidi ya mahujaji 140. Idadi ya mahujaji wengine waliokufa na nchi wanazotoka kwenye mabano ni 87 (Morocco), 55 (Misri), 20 (Cameroon), 19 (Niger), 18 (India), 18 (Pakistan), 11 ( Chad), 8 (Somalia), 5 (Senegal).
Nchi za Algeria, Uturuki na Tanzania kila mmoja imepoteza mahujaji wanne, ingawa jana kiliripotiwa kifo cha mahujaji mwingine wa Tanzania, hivyo kufanya waliokufa kufikia watano. Nchi za Indonesia, Kenya na Nigeria kila moja imepoteza mahujaji watatu wakati Uholanzi, Burundi na Burkina Faso kila mmoja imepoteza mtu mmoja.
Wakati huo huo, taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, jijini Dar es Salaam jana, ilisema idadi ya watu wa mataifa mbalimbali duniani waliokufa huko Makka, imeongezeka na kufikia 769 na majeruhi wamefikia 934.
Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia Ubalozi wa Tanzania mjini Riyadh, Saudi Arabia, ilisema tukio hilo la Makka, lilitokea Septemba 24 mwaka huu na lilitokana na mkanyagano (stampede) wa mahujaji.
“Wizara kupitia Ubalozi huo inaendelea kufuatilia hatma ya mahujaji wa Tanzania waliopotea katika tukio hilo la ajali ambapo hadi sasa mahujaji wa Tanzania wapatao 50 bado hawajaonekana.
Vikundi wanavyotoka mahujaji hao na idadi yao ni kama ifuatavyo Ahlu Daawa- mahujaji 30, Khidma Islamiyamahujaji 16 na TCDO- mahujaji 4,” ilieleza taarifa hiyo ya Wizara. Vile vile juhudi za Ubalozi wa Tanzania kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission na viongozi wa vikundi vilivyopoteza mahujaji wao, zimefanikiwa kuutambua mwili wa hujaji mmoja aliyefariki dunia, anayejulikana kwa jina la Shafi Khamis Ali kutoka kikundi cha Ahlu Daawa.
Kutambuliwa kwa mwili wa hujaji huyo, kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania, waliofariki dunia katika tukio hilo kufikia watano. Pia, Wizara kupitia Ubalozi wake, imepokea taarifa ya kupatikana kwa hujaji mwingine, anayeitwa Nasra Abdullah akiwa hai, naye kutoka kikundi hicho cha Ahlu Daawa.
“Mahujaji wengine wa Tanzania wapo salama, ambapo tarehe 26 Septemba 2015 walimaliza Ibada ya Hijja na tarehe 28 Septemba 2015 wameanza safari ya kurejea nyumbani. Wizara inaendelea kuwaomba wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati serikali ikiendelea kufuatilia” ilisema taarifa hiyo ya Wizara.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Afya wa Saudi Arabia, Khalid al-Falih, amekaririwa na mashirika ya kimataifa, akisema kuwa Serikali ya Saudi Arabia itachunguza vifo vya mahujaji hao zaidi ya 700 vilivyotokea Makka.
Waziri huyo alieleza kuwa uchunguzi utafanyika, kubaini chanzo cha vifo hivyo, ambavyo havijawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 25. “Uchunguzi utafanyika juu ya tukio la kufa mahujaji katika mji wa Mina.
Tunadhani baadhi ya mahujaji walianza kutembea bila kupata maelekezo kutoka kwa wahusika maalumu wa kuwaongoza. Uchunguzi utakuwa wa haraka na tutatoa matokea yake mapema,” alieleza Waziri huyo wa Saudi Arabia.
Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saud Arabia ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike kuhusu tukio hilo na kwamba baada ya kupata matokeo ya uchunguzi huo, atatoa maamuzi stahiki. Pia, mfalme Salman ameagiza taratibu za Hijja, ziangaliwe upya.
Awali, ilibainika kuwa mahujaji 717 wamepoteza maisha na wengine 800 walijeruhiwa katika tukio hilo la Makka, wakati watu zaidi ya 2,000,000 walipokuwa wakiswali Ibada ya Hijja. Makundi makubwa mawili ya mahujaji, yaligongana yalipokutana wakati yakielekea “kumtupia mawe shetani”, kilometa chache nje ya Makka.
Created by Gazeti la HabariLeo.
Kombani aagwa Dar
By:
Unknown
On: 02:13
Ndugu wa karibu na watoto wa aliyekuwa waziri wa nchi, ofisiya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani wakitoa
heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa ibada ya kumuaga
iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Dae es salaam.
MAKAMU wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal jana aliongoza mamia ya Watanzania waliojitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani.
Mwili wa Kombani uliagwa katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam huku idadi kubwa ya watu wakiwemo Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, viongozi wa vyama vya siasa na wabunge wakihudhuria.
Jeneza lenye mwili wa marehemu liliwasili katika viwanja hivyo majira ya saa 5:00 asubuhi, likiwa limebebwa na askari wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliokuwa wamevalia suti nadhifu huku wakisindikizwa na Mawaziri na Manaibu Mawaziri hadi kwenye jukwaa.
Akitoa salamu za Serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenista Mhagama alisema, serikali imepata pigo kubwa kutokana na kifo cha Kombani kwani alikuwa ni kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo ya taifa kupitia wajibu wake na majukumu aliyopewa na serikali.
Alisema pengo aliloacha Kombani haliwezi kuzibika kirahisi kwani mchango wake ulikuwa ukihitajika kwa ajili ya kuendeleza harakati za kuleta maendeleo ya taifa. “Alijitahidi kuwapigania wananchi wa jimbo lake, hakuna ubishi alifanya kazi kubwa kwa wananchi wa jimbo lake.
Amefanya mageuzi makubwa katika sekta ya utumishi na atakumbukwa daima,” alisema Mhagama. Awali akizungumza, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema, Kombani aliwasaidia kuunda muundo mpya wa utumishi wa Bunge ambapo alisema, Agosti 16, mwaka huu walipitia muundo huo kwa mara ya mwisho ambapo Kombani alishiriki.
Alisema wakiwa katika kikao hicho Kombani alitoka nje na baada ya muda alipewa taarifa kuwa anajisikia vibaya. “...Kwa kuwa nilikuwa Mwenyekiti wa kile kikao nikapewa taarifa kuwa Waziri anajisikia vibaya nikawa nimeshangaa kwa sababu tulikuwa naye yuko vizuri, nikawa nimetoka kwenda kumuona,” alisema.
Alisema wakati wakiwa hapo Katibu wa Bunge alimwambia kuwa Waziri anataka apelekwe kwa daktari wake ambapo alipelekwa kwa daktari huyo katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni. Aliwataka waliohudhuria tukio hilo kuchukulia kifo cha Kombani kama somo la kutenda mema kama ilivyokuwa kwa Waziri huyo.
Akitoa salamu za uliokuwa Umoja wa Wabunge Wanawake, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angellah Kairuki alisema, bado mchango wa waziri huyo ulikuwa ukihitaji kwani alikuwa ni mshauri mzuri katika mambo mbalimbali ya umoja huo pamoja na Bunge kwa ujumla.
Alisema umoja huo ulipokea kifo chake kwa mshtuko mkubwa kwani hawakutegemea kama wangempoteza mapema kiasi hicho na hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi ambapo pia alikuwa anatetea jimbo lake la Ulanga Mashariki.
Mwili huo jana ulisafirishwa kwenda mkoani Morogoro kwa ajili ya maziko ambapo kwa mujibu wa ratiba ya maziko, leo mwili huo unatarajiwa kuwasili katika uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya sala kabla ya kwenda kuhifadhiwa katika nyumba yake ya milele.
Katika sala hiyo itakayofanyika uwanjani hapo, inatarajiwa kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Rais Dk Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Bunge Makinda na viongozi mbalimbali.
Kombani alifariki Septemba 24, mwaka huu katika Hospitali ya Apollo nchini India na anatarajiwa kuzikwa shambani kwake, Lukobe, nje kidogo ya mji wa Morogoro.

Monday, 28 September 2015
Dk. Shein aahidi kuipaisha zaidi Zanzibar
By:
Unknown
On: 23:54
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
MGOMBEA
Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ali Mohammed
Shein, amesema amedhamiria kuipaisha Zanzibar kwa kuwa uwezo huo anao.
Amesema kwamba, pamoja na majukumu mengi aliyonayo, kazi hiyo ataifanya katika miaka mitano ijayo kama atafanikiwa kuendelea kukiongoza kisiwa hicho.
Kutokana na hali hiyo, amewatahadharisha Wazanzibari wasiwachague wagombea waongo ambao mara zote wamekuwa wakisema uongo majukwani kwa lengo la kupata madaraka.
Dk. Shein ambaye anatetea nafasi yake ya urais wa Zanzibar, alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi katika uwanja wa Galagala uliopo Mjini Magharibi, Unguja.
“Kwa kweli bado nina nia ya kweli dhati ya kuwatumikia Wazanzibari kwa sababu uwezo huo bado ninao. Nawaomba sana vijana msidaganywe na wanasiasa wasiokuwa waaminifu kwani hakuna rais atakayekuja kutoa ajira kwa kila mzanzibari kwani hilo nimeliona baada ya kuizunguka dunia hii.
“Kwa kuwa bado nina uwezo, nimelazimika kuja na mambo mbalimbali yatakayoipaisha Zanzibar kiuchumi ikiwamo ujenzi wa kiwanda cha samaki, uwekezaji katika sekta ya uvuvi na ujenzi wa kiwanda cha maziwa.
“Yote hayo ni mambo ya msingi kwa sababu yatasaidia kuzalisha ajira na pia yatawawezesha wananchi kuweza kukabiliana na gharama za maisha,” alisema.
Katika kuhakikisha Zanzibar inasonga mbele kiuchumi, Dk. Shein alisema Serikali yake hivi karibuni itazindua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume utakaokuwa chachu ya maendeleo kisiwani humo.
Kuhusu suala la wazee, alisema kuanzia mwakani, kila mzee aliyefikisha umri wa miaka 70, atakuwa akipewa pesheni ya Sh 20,000 kila mwezi.
Created by Gazeti la Mwananchi

Mafuriko yamzidi nguvu Lowassa
By:
Unknown
On: 23:49
*Avunja mkutano Tanga kwa hofu watu kupoteza maisha
Fredy Azzah na Amina Omari, Tanga
WAKATI baadhi ya watu wakimshawishi kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Edward Lowassa, alisema hawezi kuzua mafuriko kwa mikono.
Lakini jana jijini Tanga mafuriko hayo (watu) yalitaka ‘kumsomba’ kutoka na maelfu ya watu kufurika katika uwanja Tangamano kwa ajili ya kumsikiliza.
Baada ya kuona watu wanazidi kuongezeka, huku wengi wakianguka na kupoteza fahamu, Lowassa alitangaza kuuvunja mkutaano huo kwa hofu ya watu kukanyagana na kupotea maisha.
Hali ya kuwapo watu wengi katika mkutano huo ilianza kuonekana mapema, kwani wananchi walianza kufurika uwanjani hapo kuanzia saa 3:00 asubuhi, licha ya kutangaziwa wafike saa 5:00 asubuhi na mkutano ungeanza saa 8:00 mchana.
Ilipofika saa 5:00 uwanja huo tayari ulikuwa umefurika, hali iliyofanya watu wengine kukaa kwenye majengo yaliyo pembeni ya uwanja huo na wengine kupanda kwenye miti.
Ilipofika saa 7 mchana, barabara ya Taifa inayounganisha jiji hilo na vitongoji vyake, ilifungwa ili kuepusha ajali kutokana na watu wengi waliokuwa katika eneo hilo.
Lowassa kuvunja mkutano
Dalili za mkutano huo kuvunjika zilionekana pale, Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye alipopanda jukwaani.
Sumaye alitumia muda wake kueleza watu namna ya kusaidia wale wanaopoteza fahamu na watoto waliokuwa uwanjani hapo.
“Sisi Ukawa ni watu wa amani na utulivu, naomba msisukamane,” alisema.
Pamoja na kauli hiyo ambayo haikuzaa matunda, hali ilizidi kuwa mbaya ambapo alilazimika kumkaribisha Lowassa ili azungumze.
Kitendo cha Lowassa kukaribishwa kilionekana wazi kuzidisha mkanyagano mkubwa.
Lowassa, aliposimama wananchi walianza kushangilia kwa sauti, huku wakisukumana jambo lililosababisha watu kuendelea kupoteza fahamu.
Lowassa
Lowassa aliposimama alisema. “Hali iliyopo hapa si nzuri, tutapoteza maisha ya watu,” asante sana kwa mapokezi mliyonipa, nimekuja kutafuta kura sikujua kama wengi hivi.
“Leo mnanikumbusha Sumbawanga (Rukwa), Songea (Ruvuma) na Ujiji (Kigoma), sasa hapa tunaahirisha mkutano huu kwa sababu watu wanaweza kufa, kinamama na watoto watakufa,” alisema Lowassa.
Baada ya maelezo hayo, alijaribu kushuka jukwaani lakini watu walionekana wanakiu ya kutaka kumsikiliza.
Lowassa alikaa takribani dakika tano akisikiliza watu waliokuwa karibu na jukwaa na akachukua tena kipaza sauti na kuanza kuwatuliza.
Safari hii aliwaahidi kuwa, ndani ya miezi sita baada ya kuchaguliwa, atafufua bandari ya Tanga na reli ili kuinua uchumi wa wakazi hao.
Baada ya kusema hivyo, wananchi walio wengi walianza kutaja jina la Babu Seya, na Lowassa na kusema akipata nafasi ya kuwa rais, ataagiza vyombo vya sheria kuangalia upya suala hilo.
Wakati hayo yakiendelea, watu waliendelea kusogea karibu na jukwaa na kulizunguka huku wakisema wanataka ajira.
Baada ya kuzungumza na na kuwatangazia kuwa mkutano umefungwa hivyo waondoke, waliendelea kukaa kwenye eneo hilo hali iliyomfanya na yeye kukaa juu ya jukwaa kwa takribani dakika 10 akiwasikiliza.
Baada ya hapo, Lowassa alishuka jukwaani na kuondoka.
Hata baada ya kuondoka watu walibaki wakiwa wamekusanyika uwanjani hapo huku kukiwa na makundi ya vijana waliokuwa wakiimba ‘CCM mafisadi’ , ‘CCM imekufa, imezikwa’ .
Chopa
Ilipofika saa 8, umati huo ulitangaziwa kwamba helkopta inayotumiwa na Lowassa kwenye mikutano yake, haitatua kwenye eneo hilo kama ilivyokuwa imepangwa awali kutokana na uwanja huo kufurika watu.
Kutokana na hali hiyo, helkopta hiyo ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Tanga na kisha mgombea huyo kutumia gari kwenda uwanjani.
Kadri muda ulivyosonga, watu walikuwa wakizimia kutokana na kukosa hewa hali iliyosababisha na wingi wa watu.
Mmoja wa maofisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu waliokuwa uwanjani hapo, alisema watu waliopoteza fahamu walikuwa zaidi ya 50.
Mabomu ya machozi
Watu waliokuwa uwanjani hapo, walipokuwa wakitoka walijaa kwenye barabara ya Taifa na kufanya isitumike.
Hali hiyo ilidumu takribani dakika 20 hali iliyofanya polisi wapige mabomu ya machozi ili kuwatawanya.
Kabla ya mkutano huo, Lowassa alifanya mikutano Mombo wilayani Korogwe na Bumbuli wilayani Lushoto.

Magufuli: Watanzania wamekata tamaa
By:
Unknown
On: 23:44
*Asema haiwezekani wachache wale kuku kwa mrija
Na Bakari Kimwanga, Iringa
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema amejipanga kulipa deni kwa Watanzania kwa kuleta mabadiliko ya kweli.
Amesema pamoja na hali hiyo, anatambua namna wananchi walivyokata tamaa ikiwamo kushindwa kubadili maisha yao, kutokana na ubinafsi wa watu wachache ambao wameamua kujimilikisha rasilimali za nchi.
Dk. Magufuli, alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti jana, alipohutubia mikutano ya hadhara katika majimbo ya Kalenga, Kilolo na Iringa Mjini.
Alisema nchi haiwezi kuendelea kwa mfumo wa baadhi ya watu kujiona wao wapo daraja la kwanza, huku wananchi wa kawaida wakiendelea kuishi maisha ya kawaida.
Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali yake ya awamu ya tano itahakikisha inatoa fursa kwa Watanzania wote kunufaika na rasilimali za taifa.
Alisema Serikali yake, itakuwa ya watu waadilifu ambao watakuwa tayari kufanya kazi kwa masilahi ya watu.
“Ndugu zangu, mambo ni mengi ambayo nataka kuyafanya.. nataka kuleta maendeleo ya kweli na Tanzania mpya ambayo itawafanya wananchi wote wafurahie Serikali yao kuliko sasa.
“Ninajua kila zama na kitabu chake, Serikali ya Magufuli inakuja kufanyakazi, ikiwamo ya kuwafunga mafisadi…kwa hili simung’unyi maneno Watanzania nitalitekeleza kwa vitendo kikubwa ninawaomba mniamini kwa kunichagua.
“Ninajua Watanzania wanataka mabadiliko ambayo ni M4C yaani ‘Magufuli for Change’ na kwa lugha ya kawaida ni Magufuli kwa mabadiliko tena ya kweli,” alisema Dk. Magufuli.
Akizungumza namna atakavyoubadili mji wa Iringa, alisema anajua changamoto zilizopo katika mkoa huo, ikiwamo kero ya barabara hasa za ndani.
“Ninawashangaa watu wanasema eti CCM haijafanya kitu na wengine ni hapa hapa Iringa mjini tena mchungaji wa kondoo wa Mungu ambaye anazijua amri kumi za Mungu ikiwemo ya kutosema uongo.
“Tena amekuwa akitukana ovyo ndani na nje ya Bunge nataka kuwaambia mawaziri nao ni binadamu wana nyongo…nataka kuwauliza ikiwa kila siku unamtukana waziri hivi kweli anaweza kukupa fedha za maendeleo, nichagueni mimi na wabunge wa CCM,” alisema.
Alisema anahitaji ushindi wa asilimia 99 ili wapinzani waisome namba kupitia masanduku ya kura.
Dk. Magufuli ambaye ni maarufu kwa jina la ‘Tingatinga’ alisema anajua kazi kubwa anatakayokuwa nayo ikiwemo kulinda amani na umoja wa Watanzania.
“Ninataka kuwaambia mimi, nimekuwa waziri kwa miaka 20 sijawahi kukemewa wala kufukuzwa nawahakikishia Watanzania nitafanyakazi usiku na mchana kulinda amani ya nchi yetu,” alisema.
Alisema pamoja na yaliyotokea ya baadhi ya wana CCM kuhama, yeye yupo imara na huenda watu hao kuondoka kwao itakuwa salama kwa chama hicho ambacho tayari kilianza kuonekana hakifai mbele ya Watanzania.
Alisema Serikali yake itakuwa rafiki wa wafanyabishara na anaunga mkono kazi kubwa ya kukuza ajira inayofanywa na kada wa chama hicho Mkoa wa Iringa, Said Asas ambaye ameweza kuajiri vijana wa mkoa huo zaidi ya 400.
Abadili staili jukwaani
Katika kile kinachoonekana kubadili aina ya kuomba kura jukwaani, Dk. Magufuli kila alipokuwa anaitwa alikuwa akirukaruka jukwaani na kisha kuanza kuhutubia.
Akiwa wilayani Kilolo, baada ya kurukaruka jukwaani, alimpigisha ‘push up’ mgombea ubunge wa jimbo hilo, Venance Mwamoto huku akisema kufanya hivyo ni ishara ya wagombea wa CCM wako imara.
“CCM ipo imara pamoja na wagombea wake wote kuanzia urais, ubunge na udiwani, ndiyo maana tunaanza hivi ili Watanzania waone tuna kiu ya kweli ya kuwaletea maendeleo,” alisema.
Nape: CCM si malaika
Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema CCM inaongozwa na watu na si malaika ambao wapo sahihi kila wakati na kwa kila kitu.
“Tunajua Watanzania wanahitaji mabadiliko, tunaamini hakuna wa kuyaleta zaidi ya Dk. Magufuli ambaye ataongoza Serikali na chama chetu ili kiwe imara zaidi,” alisema.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, William Lukuvi, aliwataka Watanzania kutochagua rais wa mbwembwe, ispokuwa wachague rais kwa sifa zake hasa Dk. Magufuli.
Mwisho
Ajali yaua watano
Na Walter Mguluchuma, Katavi
WATU watano wamefariki dunia papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa wilayani Mlele Mkoa wa Katavi, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 9 alasiri katika Kijiji cha Matandalani.
Alisema ajali hiyo, ililihususha gari aina ya Noah lenye namba za usajili T451 DDP lililokuwa likiendeshwa na Justine Ndayele (24) mkazi wa Mkoa wa Kigoma.
Alisema gari hilo mali ya Adamu Omary, lilikuwa likitokea Mpanda mjini kwenda Kijiji cha Sitalike.
Aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Lunyalaja Nzugamrwa (50), Furaha Edward (35), Eva Mwanisawa (25), Maiko Jacob wote wakazi wa Kijiji cha Sitalike na Mwila Kifwewe (25) mkazi wa mtaa wa Kawajense mjini Mpanda.
Alisema miili ya marehemu hao, imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.
Kamanda Kidavashari, aliwataja majeruhi kuwa ni Felista Matunda (30) mkazi wa tarafa ya Inyonga,Thobias Kisila (65) mkazi wa Kijiji cha Sitalike, Velina Libaratu (9) mkazi wa Mpimbwe,Odila Lenatusi (19), Ndila Kameme (32) wote wakazi wa mtaa wa Nsemlwa.
Alisema majeruhi hao, wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda wakiendelea na matibabu.
Alisema jeshi hilo, linamshikilia dereva wa gari hilo na kwamba upelelezi wa tukio hilo utakapokamilika dereva huyo atafikishwa mahakamani.
Ceated by Gazeti la Mwananchi

Saturday, 26 September 2015
Kikwete ataja sababu za utalii kutokua haraka
By:
Unknown
On: 05:51
Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba wakati wa Mkutano Mkuu wa 10 wa mwaka wa Chama kinachojihusisha na Usafiri (ATA) uliofanyika jijini New York, Marekani jana. (Picha na Freddy Maro). |
RAIS Jakaya Kikwete ametaja changamoto zinazosababisha utalii wa Afrika usikue kwa haraka kuwa ni ukosefu wa miundombinu bora ya kitalii, utangazaji wa masoko ya utalii na matatizo ya usafiri wa anga kuingia na kutoka Afrika.
Alisema, pamoja na kuwa na vivutio vingi vya utalii, changamoto hizo zinalifanya bara hilo libaki nyuma katika kuvutia watalii wa kimataifa, hivyo kuendelea kuwa na mapato madogo yanayotokana na sekta hiyo.
Aidha, alisema kuwa Tanzania itaendelea kutenga eneo kubwa la ardhi yake kwa ajili ya hifadhi, pamoja na kudhibiti ujangili dhidi ya tembo. Alisema, kutokana na jitihada zinazofanywa kuukomesha, katika mwaka uliopita ujandili umepungua.
Aliyasema hayo jana alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa shughuli za miaka 10 ya Chama cha Usafiri cha Afrika (ATA) na miaka 10 ya Jukwaa la Rais kuhusu Utalii, kwenye Kituo cha Kimmel cha Chuo Kikuu cha New York jijini New York.
Rais Kikwete aliyeko Marekani kuhudhuria shughuli za mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) baada ya kumaliza kuendesha vikao vya jopo la watu mashuhuri duniani wanaotafuta njia inayoweza kutumiwa na dunia kukabiliana na magonjwa ya mlipuko alisema asilimia 36 ya eneo lote la nchi yake litatengwa kwa ajili ya shughuli za hifadhi.
Wakati huo huo, Rais Kikwete alisema ukweli kuhusu Afrika lazima uelezwe kwa usahihi na Waafrika wenyewe, ili picha inayojengwa kuwa tatizo lililo katika nchi moja ni tatizo la bara zima la Afrika ijulikane kuwa si sahihi.
Alisema, “Ni lazima itafutwe nia ya kulisahihisha jambo hilo kwa sababu Afrika ni bara lenye nchi 54 na si nchi moja na majimbo 54”. Kuhusu mapato ya utalii, alisema mwaka jana Afrika ilipokea watalii wa kimataifa milioni 56 ambalo ni ongezeko la asilimia mbili tu ya watalii wote wa kimataifa waliotembelea maeneo mbalimbali duniani na asilimia tano ya watalii wote waliotembelea dunia mwaka jana.”
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alishangiliwa wakati alipowaambia washiriki: “Napenda kuchukua nafasi hii pia kuwaaga marafiki zangu wote wa ATA kwa sababu hotuba hii ni ya mwisho kwangu nikiwa Rais wa nchi yangu...”. “Nitaondoka madarakani baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu nikiwa nimekamilisha vipindi viwili vya uongozi kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.”
Created by Gazeti la HabariLeo
HOTUBA - PAPA.
By:
Unknown
On: 05:48
Papa Francis akihutubia Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini
New York, Marekani jana mbele ya viongozi wa mataifa mbalimbali duniani
akiwemo Rais Jakaya Kikwete (wa tano kulia). (Picha na Freddy Maro).
Magufuli ajitabiria ushindi 95%
By:
Unknown
On: 05:46
Mgombea Urais wa CC, Dk John Magufuli.
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli, amejitabiria ushindi wa ‘tsunami’ wa asilimia 95 na siyo 65 kama ilivyotajwa katika utafiti wa Taasisi ya Twaweza.
Mbali na ushindi huo, Dk Magufuli aliyezungumza jana mjini Kahama, mkoani Shinyanga katika mkutano uliohudhuriwa na maelfu ya watu, pia alitabiri baadhi ya vyama vya upinzani kufa baada ya uchaguzi. Akihutubia mkutano huo ambao alikuwa akishangiliwa mara kwa mara na baadhi ya watu waliokuwa wakiimba ‘rais rais rais’, Dk Magufuli alisema anatarajia umati unaohudhuria mikutano yake ndiyo utakaompa ushindi.
“Wala sijashinda…wa kunifanya nishinde ni nyie,” alisema na kushuhudia umati mkubwa wa watu aliokutana nao katika mikoa mbalimbali aliyofanya kampeni. “Wala si asilimia 65 inayosemwa, bali utakuwa ni ushindi wa tsunami… na baadhi ya vyama vitakufa,” alisema na kutaja kuwa atashinda kwa asilimia 95.
Katika utafiti wa Twaweza uliotangazwa wiki hii, matokeo yalionesha kuwa Dk Magufuli ataibuka mshindi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 kwa kupata asilimia 65 ya kura na kufuatiwa kwa mbali na mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa ambaye ametajwa kupata asilimia 35. Akizungumzia ufisadi, Magufuli alisema, Serikali na hata chama tawala haviwezi kuwa na malaika pekee, bali wapo pia mafisadi wachache wakiwemo walioamua kuhama chama baada ya yeye kutangazwa kuwa mgombea urais.
Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika Kijiji cha Mwabomba, Jimbo la Ushetu na pia kwenye mkutano mjini Kahama, Magufuli alisema wapo ambao baada ya kupewa dhamana ya uongozi, wamekuwa wasaliti wa Serikali. “Hatuwezi kusema Serikali inaongozwa na malaika …wapo wabaya wachache. Hata kwenye CCM wapo. Ndio maana wengine walipoona nimeingia wakaanza kukimbia… na dalili ya mafisadi huwa ni kukimbia,” alisema.
Alisema walikimbia kwa sababu wanafahamu msimamo wake huwa anachukia mafisadi, anamtanguliza Mungu na yupo kwa ajili ya wanyonge. “Nipeni kura za kutosha niende nikashughulike na mafisadi,” alisema na kuendelea kusisitiza nia yake ya kuanzisha Mahakama ya Mafisadi. Alisema Tanzania imetoka kwenye mikono mizuri ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na imelelewa katika misingi ya umoja na amani.
Alisisitiza Serikali ya CCM siyo mbaya, bali wapo wachache hata ndani ya chama. Alisema ndiyo maana ameomba urais ili nchi iwe na neema. Alimfagilia Samuel Sitta (Waziri wa Uchukuzi) kuwa amesimama imara, hababaiki, hadanganyiki na kwamba hata alipogombea naye urais kwenye ngazi ya chama, alitambua kuwa wanaogombea ni wengi na wanaoitwa ni wachache. “Lakini wapo wenzetu wanapokosa nafasi…,yuko mmoja aligombea na Kikwete.
Wakati anagombea miaka ile ya nyuma, akasema yeye achaguliwe kwa sababu amefanya kazi nzuri katika Serikali ya Mkapa…,” alisema Magufuli. Aliendelea kusema akimlenga Frederick Sumaye, “Na sasa akagombea akasema yeye ndiye mwanzo wa mafanikio yote. Alipokosa akahama na sasa anasikika kwenye majukwaa akisema Serikali haijafanya kitu chochote.” “Wewe mtu ulikuwa humo humo CCM miaka kumi, ukagombea wakakuweka pembeni…leo unasimama na kusema hakuna mafanikio.
Kwa nini ulibaki sasa, ulikuwa unafanya nini,” alihoji na kushangiliwa na umati wa watu mjini hapa. Magufuli ambaye alikuwa akishangiliwa mara kwa mara na umati wa watu, aliwakumbusha wana Kahama mafanikio yaliyoletwa na Serikali ikiwamo kukua kwa mji na uwepo wa huduma za umeme, mtandao wa barabara na mawasiliano ya simu. “Kwa nini watu wanasahau mapema hivi?
Ni vyema mtu ukatambua yale mazuri yaliyofanywa…,” alisema na kutaja mafanikio ya ujenzi wa mtandao wa barabara nchi nzima. Alisema Wilaya ya Kahama haikuwa na shule za sekondari tofauti na sasa ambapo zipo kila mahali. Alisema watu wa Kanda ya Ziwa, hususani Kagera na Mwanza, ilikuwa ni kawaida kwenda Dar es Salaam wakipita Uganda na Kenya tofauti na sasa wanavyochagua mabasi ya kupanda.
“Haya yote hawayaoni…bado mtu anasimama kwenye majukwaa bila aibu anasema hakuna chochote kilichofanyika…shukurani ya punda huwa ni mateke,” alisema na kuongeza kuwa hata amani si chochote kwa hao wanaokosoa. Aliwataka wana Kahama kutambua mahali walikotoka, walipo na wanapokwenda wasije watu wakawapeleka pasipo. Alisema baadhi yao wanaotaka kuipeleka nchi wanakojua, hawana rekodi nzuri.
Alisisitiza kuwa katika uongozi wake atamtanguliza Mungu na atawatumikia Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao. Wachimbaji wadogo Akiwa eneo la Nyarugusu wilayani Geita, Magufuli aliahidi kufanyia kazi mgogoro uliopo kati ya wachimbaji wadogo wa eneo la Nyarugusu na Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kuhusu eneo la uchimbaji. Alisema wakati takribani maeneo 24 yamesharudishwa kwa wachimbaji wadogo, pia atahakikisha Serikali yake inatoa maeneo zaidi kwa wachimbaji wadogo.
Katika maeneo mengi ya Mkoa wa Geita na Shinyanga aliyotembelea jana, Magufuli aliendelea kusisitiza kwamba wachimbaji watakapovumbua madini eneo lolote, hawatanyang’anywa bali watapewa leseni za umiliki. Eneo linaloleta mgogoro katika eneo la Nyarugusu, ni ambalo Stamico kwa kushirikiana na mwekezaji kutoka Marekani wanadaiwa kushindwa kuliendeleza tangu mwaka 1983 na sasa wachimbaji wadogo wanataka wapewe.
Wamvaa Lembeli Wakati huo huo aliyekuwa Mbunge wa Kahama kwa tiketi ya CCM, James Lembeli ambaye alihamia Chadema, amerushiwa makombora na makada mbalimbali waliozungumza kwenye mikutano ya kampeni wilayani hapa. Mwenyekiti wa Wazazi, Bulembo alimtaja Lembeli na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mngeja kuwa ni watu wanaomnyonya mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Bulembo alisema, kwa mujibu wa wananchi wa Jimbo la Ushetu, wanasema Lembeli amekimbia kwa sababu hakutimiza matakwa yao. Lembeli na Kishimba (Jumannemgombea ubunge wa CCM) wapi na wapi?,” alihoji Bulembo. Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya Kampeni na Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga, Samuel Sitta, alisema Lembeli akiwa ndani ya CCM, alikuwa akijitambulisha kuwa ni mtu anayepambana na uovu lakini sasa yuko kundi moja na kundi alilokuwa akilipinga.
“Nasimama kwa masikitiko sana. Kulikuwa na ndugu yetu katika chama hiki anaitwa Lembeli; Alijitahidi sana kujitambulisha kama mtu anayepambana na maovu. Leo hii mtu aliyesema anapambana na maovu, yuko katika kundi moja na Mngeja, wanamsujudia mtu anayeitwa Lowassa; hii ni aibu sana,” alisema. Sitta aliendelea kusema, “Lowassa kwa sisi tunaomfahamu akiwa kijana, ni mtafutaji tu. Huyu haridhiki na utajiri wowote.
Alipogombea katika hatua za awali kwenye CCM alidhani ataitisha kwa kutumia fedha nyingi ili ateuliwe, lakini vigezo vya CCM si hivyo bali ni vya Chadema, ambavyo mtu akiwa na fedha anakuwa mwanachama namba moja. “ Alisema hao alioahidi mali wakae naye huko huko, CCM inachagua rais atakayejali Watanzania wa kawaida wakiwemo mama lishe, wenye bodaboda na wamachinga.
Sitta alisema mwezi mmoja tangu kampeni zianze, ahadi zilizomo kwenye ilani ya uchaguzi zinavyofafanuliwa na mgombea, ni tofauti na jinsi ilivyo kwa mgombea wa Chadema anayeungwa mkono na umoja wao wa Ukawa. Sitta alisema, kwenye udiwani, ubunge anataka kata na majimbo yote ya Shinyanga yachukuliwe na CCM. Alibeza wanaotumia helikopta nchi nzima na kusema hawawezi kuona matatizo ya wananchi.
“Leo hii mgombea wetu kasimama katika vijiji visivyopungua saba ambavyo vilikuwa njiani (wilayani Kahama), kwa sababu anatembea katika barabara,” alisema. Mgombea urais wa CCM, Magufuli hadi sasa, amefika kwenye vijiji zaidi ya 4,512 nchini. Mgombea huyo na mgombea mwenza, wamesafiri jumla ya kilometa 32,800 kuomba kura nchini.

Simba, Yanga ni kifo leo
By:
Unknown
On: 05:44
Kikosi cha Yanga. |
ILIKUWA miezi, mwezi, wiki, siku na sasa ni saa kabla ya vigogo vya soka Tanzania Bara vya Simba na Yanga kuchuana katika moja ya mechi za Ligi Kuu kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Tofauti na mara nyingi zinapokutana, leo timu hizo zinashuka dimbani zikiwa zinalingana kwa pointi wakati Yanga iko kileleni ikiwa inaongoza kwa tofauti ya mabao tu, huku kila moja ikiwa na pointi tisa.
Si Simba na Yanga tu zenye pointi tisa, Azam FC na Mtibwa Sugar, nazo zina idadi kama hiyo ya pointi na hivyo kufanya raundi ya nne kuwa na mvutano wa aina yake. Makocha wa pande zote mbili wametamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka hapa nchini na hata nje ya Tanzania.
Kocha wa Yanga, Hans van de Pluijm alisema kuwa mazoezi ya timu yake katika kisiwa cha Pemba yameisaidia timu hiyo kutokana na utulivu wa kisiwani humo. Pluijm anataka kuvunja mwiko wa timu hiyo kusumbuliwa na Simba katika kipindi cha hivi karibuni licha ya Yanga kuonekana bora zaidi, ukilinganisha na vijana hao wa Msimbazi.
Kocha wa Simba ambaye hii ni mechi yake ya kwanza dhidi ya Yanga, Muingereza Dylan Kerr ametamba kuwa lolote litakalokuwa, Yanga lazima wakae. Kerr, ambaye kikosi chake kilipiga kambi Unguja amesema kuwa amewapanga vizuri vijana wake ili kuhakikisha leo wanaoondoka na pointi zote tatu na kuwafurahisha wapenzi na mashabiki wao.
Mbali na makocha, wapenzi, mashabiki na wachezaji nao wamekuwa wakitambiana huku kila upande ukitamba kuwa wataibuka washindi na kuwalaza mapema wapinzani wao baada ya dakika 90.
Mshauri wa ufundi wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Abdallah Kibadeni alikaririwa hivi karibuni akisema kuwa, Yanga wataibuka washindi katika mchezo huo kutokana na ubora wa timu yao kwa sasa.
Kibadeni mbali na kuwahi kuwa mchezaji anayeshikilia rekodi ya kuwafunga Yanga hat-trick, pia aliwahi kuwa kocha wa timu hiyo mara kadhaa na ile ya Taifa. Simba ambao ni wenyeji katika mchezo huu wa leo, walishinda mechi zao tatu kwa kuzifunga African Sports 1-0 na Mgambo JKT 2-0 zote katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kabla ya kuifunga 3-1 Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa.
Licha ya kucheza kwenye uwanja inaotumia kama wa nyumbani, Yanga leo ni wageni na walishinda mechi zao tatu katika uwanja huo wakiwa wenyeji. Yanga waliwachapa 2-0 Coastal na baadae walishinda 3-0 dhidi ya Prisons kabla ya kukutana na JKT Ruvu kwa kuipiga 4-1.
Kwa upande wa mabao ya kufungwa, timu zote mbili zimefungwa bao moja na hivyo kuonesha ugumu wa safu zao za ushindi lakini kwa ushambuliaji, Yanga haina mpinzani baada ya kufunga mabao tisa wakati wenzao wamefunga mabao sita tu.
Simba wanaonekana kumtegemea sana Hamisi Kiiza aliyefunga mabao matano hadi sasa wakati Yanga ina wafungaji kama Amissi Tambwe na Donald Ngoma ambao kila mmoja amefunga mabao matatu.
Katika safu ya kiungo, Yanga inatarajiwa kuwa na akina Haruna Niyonzima, Thabani Kamosoko huku Simba huenda ikawategemea Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto na wengineo. Simba imepata pigo baada ya kocha wake wa mazoezi ya viungo, Dusan Marmcilovic kutimka siku chache kabla ya pambano hilo kwa madai ya kutoelewana na bosi wake.
Hata hivyo, uongozi wa Simba umedai kuwa kocha huyo aliondoka baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa miezi mitatu wa kuinoa timu hiyo. Viingilio vya mchezo huo ni Sh 7,000, wakati kiingilio cha juu ni Sh 30,000 kwa viti vya VIP A, Sh 20,000 kwa viti vya VIP B & C.
Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi wa kimataifa mwenye beji ya FIFA, Israel Nkongo (Dar es Salaam) akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Ferdinand Chacha (Mwanza), mwamuzi wa akiba Soud Lila (Dar es Salaam) wakati kamishna wa mchezo huo atakuwa Charles Mchau kutoka Kilimanjaro.
Michezo mingine ya Ligi Kuu leo ni Coastal Union dhidi ya Mwadui FC katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Maafande wa jeshi la Magereza (Tanzania Prisons) watawakaribisha maafande wa Mgambo Shooting katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mechi zingine ni JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Stand United katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, huku wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar watawakaribisha Majimaji ya Songea katika Uwanja wa Manungu wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Toto Africans katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Kesho Jumapili Azam FC watawakaribisha Mbeya City katika Uwanja wa Chamazi Complex, huku African Sports wakiwa wenyeji wa Ndanda FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga
Created by Gazeti la HabariLeo
Watanzania wanne waliokufa watajwa
By:
Unknown
On: 05:39
Mufti wa Tanzania, Shekhe Abubakar Zuberi Ally.
WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imethibitisha kutokea kwa vifo vya mahujaji Watanzania wanne, waliokufa wakati wakishiriki ibada ya Hijja, iliyofanyika Makka, Saudi Arabia juzi.
Taarifa ya wizara hiyo iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, umeeleza kuwa mahujaji hao walikufa kutokana na msongamano mkubwa wa watu uliotokea kwenye eneo la Mina.
Miongoni mwa waliokufa na kutambuliwa kwa mujibu wa taarifa hiyo ni Mwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi na Sefu Saidi Kitimla, huku taratibu zikiendelea kuchukuliwa kutambua mwili wa Mtanzania wa nne.
“Ubalozi unaendelea na jitihada za kupata jina la Mtanzania mwingine aliyekufa kwenye tukio hilo. Aidha, Serikali ya Saudia imeahidi kutoa taarifa kamili, ikiwemo idadi ya watu waliokufa na majeruhi na nchi wanazotoka mara itakapokamilika,” ilieleza taarifa hiyo.
Mbali na Watanzania hao wanne, taarifa hizo zimeeleza kuwa kuna mwingine aliyetokea nchini Tanzania na kufa katika tukio hilo, Fatuma Mohammed Jama, ambaye imebainika ni raia nchi jirani ya Kenya. “Mtu mwingine aliyekufa ni raia wa Kenya anayeishi nchini, ambaye ametambulika kwa jina la Fatuma Mohammed Jama,” imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini humo, kwa kushirikiana na taasisi zinazoshughulikia masuala ya Hijja za Tanzania, ikiwemo Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na mamlaka za Serikali ya Saudi Arabia, wanaendelea kufuatilia kwa karibu ili kujua endapo kuna vifo na majeruhi wengine kutoka Tanzania.
Kutokana na hali hiyo, Serikali imewaomba wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati Serikali ikiendelea kufuatilia.
Rambirambi za Rais Kikwete Kwa upande wake, Rais Jakaya Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz Al Saud kutokana na vifo vya zaidi ya mahujaji 700 vilivyotokea juzi.
“Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud, nimesikitishwa na taarifa ya vifo vya zaidi ya mahujaji 700 na wengine 800 kujeruhiwa Alhamisi Septemba 24 mwaka huu katika msongamano wa watu uliotokea nje ya mji mtakatifu wa Makka, wakati mahujaji hao wakikamilisha Hija yao.
“Kwa niaba ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania, natoa salamu zangu za rambirambi kwako, kwa Wasaudia na familia za mahujaji wote. “Familia yangu na Watanzania wanawaombea kwa Mungu marehemu wote ili roho zao zipumzike mahali pema peponi na kuwaombea subira kwa familia za mahujaji dunia nzima,” alieleza Rais Kikwete katika salamu zake kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mufti Akizungumzia hali hiyo katika taarifa yake iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakari Zuberi, aliye katika eneo la tukio Saudi Arabia, alisema majina ya Watanzania waliokufa katika tukio hilo, yamepatikana baada ya miili yao kukutwa na vitambulisho vyao.
Kwa mujibu wa Mufti Zuberi, mbali na taarifa za vifo vya Watanzania hao wanne na Mkenya mmoja, pia kulikuwa na taarifa za majeruhi ambao baadhi alionana nao baada ya kutoka hospitalini.
Pia alisema ameagiza maofisa wa Bakwata alioambatana nao huko, kufuatilia habari za mahujaji wa Kitanzania katika hospitali mbalimbali na sehemu za kuhifadhia maiti, ili apate uhakika wa usalama wa mahujaji kutoka Tanzania.
Mufti Zuberi amewaomba ndugu na jamaa wa mahujaji kuwa watulivu na kuwa na subira katika wakati huu mgumu, kwa kuwa Serikali ya Saudi Arabia inaendelea na kazi ya kutambua uraia wa kila mwili ili watoe taarifa na hivyo wakati wowote taarifa zaidi zitatolewa.
Wakati huo huo, Mroki Mroki anaripoti kuwa mashirika ya kimataifa yamemnukuu Waziri wa Afya wa Saudi Arabia, Khalid al- Falih, akisema kuwa vifo vya mahujaji zaidi ya 710 vilivyotokea huko Makka, vimetokana na mahujaji hao kutozingatia maelekezo ya mamlaka husika.
Taarifa iliyotolewa na kuchapishwa katika tovuti ya Waziri huyo, ilielezea kuwa uchunguzi utafanyika kubaini chanzo cha vifo vya mahujaji hao ambao havijawahi kwa zaidi ya miaka 25.
Mahujaji wapatao 717 wamepoteza maisha na mamia wengine wamejeruhiwa baada ya kukanyagana katika mji wa Mina, nje kidogo ya Makka, ambapo watu zaidi ya 2,000,000 wanaswali ibada ya hija.
Watu takriban 863 walijeruhiwa huku wengine wakikwama, wakati wa mkusanyiko huo mkubwa wa kila mwaka wa mahujaji kutoka sehemu mbalimbali duniani. “Uchunguzi utafanyika juu ya tukio la kufa mahujaji katika mji wa Mina.
Tunadhani baadhi ya mahujaji walianza kutembea bila kupata maelekezo kutoka kwa wahusika maalumu wa kuwaongoza. Uchunguzi utakuwa wa haraka na tutatoa matokeo yake mapema,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Falih alisema majeruhi watatibiwa katika hospitali zilizopo Makka na ikitokea ipo haja ya kuwapa rufaa majeruhi hao, basi watatibiwa katika hospitali mbalimbali nchini humo. Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saud Arabia ameagiza kuangaliwa upya kwa utaratibu wa Hija baada ya tukio hilo.
Katika tukio hilo, makundi makubwa mawili ya mahujaji yaligongana wakati yalipokutana Mina, yakielekea “kumrushia mawe shetani” kwenye nguzo saba zijulikanazo kama Jamarat, kilometa chache Mashariki mwa Makka. Ilielezwa kuwa matokeo ya uchunguzi huo, yatakabidhiwa kwa Mfalme Salman, ambaye atayatolea maamuzi stakihiki.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudia kupitia kwa msemaji wake, Meja Jenerali Mansour al-Turki alisema mvutano baina ya makundi hayo mawili makubwa na hali ya joto kali, vinaweza kuwa chanzo cha vifo hivyo.
Hujaji kutoka Kenya, Isaac Saleh alisema anaitupia lawama serikali ya Saudi Arabia kwa kushindwa kusimamia vyema mkusanyiko huo wa Hija hadi kusababisha vifo. “Naweza kuilaumu Serikali ya Saudia kwa tukio hili, na tayari watu watatu katika kundi langu wamepoteza maisha huku wengine hatujui walipo,”alidai Saleh.
Rahman Shareef, pia kutoka Kenya alisema, “Jamarat leo pako shwari. Nilikuwa na hofu hapo jana (juzi) lakini nashukuru nipo salama na naamini hata familia yangu inaniona niko salama.” Nchi za India, Indonesia, Pakistan na Netherland, zilithibitisha kuwa baadhi ya mahujaji wake wamekufa.
Uturuki iliarifu kuwa mahujaji wake 18 hawajulikani walipo. Navyo vyombo vya habari vya Morocco, vimeripoti kuwa mahujaji wake 87 ni miongoni mwa waliopoteza maisha.

Subscribe to:
Posts (Atom)