Live! Hakuna siri tena kati ya staa wa Bongo Movies, Wastara Juma na
Mtangazaji wa Kipindi cha Action and Cut kinachorushwa kupitia
Televisheni ya Channel Ten, Bond Bin Sinan baada ya kuonesha mahaba niue
kwa kulishana keki kwa staili ya njiwa kwenye ‘bethidei’ ya mwigizaji
huyo.
Habari kutoka kwa shushushu wetu zilidadavua kwamba, mpango mzima
ulijiri kwenye bonge la pati ya kuzaliwa kwa Wastara iliyochukua nafasi
katika Hoteli ya Sun-Rise iliyopo Kigamboni jijini Dar.
Katika pati hiyo ya kimyakimya, Wastara aliwaalika baadhi ya ndugu na marafiki zake ambapo mtangazaji huyo alikuwa mgeni maalum.
Sosi wetu huyo alitanabaisha kuwa walipofika hotelini hapo, baada ya
watu kuanza kupata vinywaji ulifika muda wa keki ambapo Wastara
aliwalisha watoto wake na baadhi ya ndugu wa karibu kisha alimuita
mtangazaji huyo na kulishana naye keki kwa staili hiyo iliyogeuka gumzo.
“Unajua wale ni wapenzi lakini siku zote hawajawahi kuweka wazi
uhusiano wao hadharani lakini sasa naona Wastara ameamua kuweka kila
kitu wazi,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kumegewa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilizungumza na
Wastara ambapo alifunguka kuwa wageni wote aliowaalika aliwalisha keki
kwa staili hiyo kuonesha ni wapenzi wake wa kweli.
“Jamani wageni wangu wote niliowaalika niliwalisha kwa staili hiyo na
hao ndiyo wapenzi wangu wa ukweli kwa sababu hata watoto wangu na dada
zangu niliwalisha kwa mdomo pia,” alisema Wastara.
Chanzo: GPL
Tuesday, 6 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment