Afya ya mwanamuziki
maarufu wa miondoko ya kufokafoka nchini Angola na mwanaharakati Luaty
Beirao,ambaye alikuwa kwenye mgomo wa kutokula kwa siku 23 imekuwa
mbaya.Mke wake ameeleza.
Beirao alikamatwa na Watu wengine 14
mwezi Juni wakishutumiwa kupanga mipango ya kumuondoa Rais aliyekaa
madarakani kwa muda mrefu Eduardo dos Santos.''nina wasiwasi kuhusu afya yake na kitakachomkuta hapo baadae'' mke wa mwanamuziki huyo, Monica Almeida aliiambia BBC.
Takriban watu 20 walikamatwa siku ya jumatatu mjini Luanda walipokuwa wakidai wanaharakati hao waachiwe huru.
Polisi walizingira kundi lao walipokusanyika katika kanisa wakiwa wamebeba mishumaa.Walishinikiza kuachwa huru kwa watu hao ambao wamekuwa wakishikiliwa kwa miezi mitatu sasa bila kufunguliwa mashtaka, ambapo ni kinyume cha Sheria nchini humo.
Mwanamuziki huyu amekuwa akiikosoa Serikali akitoa wito kutaka mgawanyo wa haki wa utajiri wa mafuta nchini humo.
Created by BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment