KOLETHA Raymond, ambaye ni muigizaji wa muda mrefu, amesema kwa sasa
amechoshwa na upweke huku akiweka wazi kuwa yuko tayari kuingia kwenye
uhusiano endapo atapata mwanaume mwenye sifa stahiki.
‘Akidondosha silabi’ na Amani, Koletha
alisema kwa muda mrefu sasa amekuwa peke yake huku pombe ikigeuka faraja
pekee ya moyo wake, kutoka na kukosa mapenzi ya dhati kwa wanaume.
“Nimeishi peke yangu kwa muda mrefu sana japo kipindi cha nyuma
wanaume waliniliza mno, lakini kwa sasa nimechoshwa na upweke huu,
nikipata mwanaume mwenye sifa ninazohitaji niko tayari kuingia tena
kwenye uhusiano,” alisema Koletha.
Chanzo: GPL
Tuesday, 13 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment