Wednesday, 7 October 2015

Tagged Under:

Kazi Imeanza!!! Kijana Mmoja Akamatwa kwa Kusambaza Ujumbe kuwa Mkuu wa Majeshi Jen. Mwamunyange kalishwa Sumu na Kufa

By: Unknown On: 08:02
  • Share The Gag
  • Kijana mmoja ambaye ni mwanafunzi kutoka taasisi moja ya Elimu ya Juu amekamatwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutunga na kusambaza ujumbe katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa Mkuu wa Majeshi hapa nchini, Jenerali Davis Mwamunyange amelishwa chakula chenye sumu na kufariki dunia.

    Taarifa hizo potofu na zisizo na ukweli wowote zilitolewa Septemba 25 mwaka huu na kukanushwa na Jeshi siku chache baadaye.
     
    Jeshi hilo limesema kijana huyo alikiri kuhusika na utunzi wa taarifa hiyo na ingawaje alipewa fursa ya kujitokeza na kuomba msamaha kwa umma, mtuhumiwa alikaidi, ndipo hatua ya kumkamata ilipofuatia.
    Credit; Mpekuzi

    0 comments:

    Post a Comment