Tuesday, 13 October 2015

Tagged Under:

Kampuni za pombe AB InBev na SABMiller kuungana

By: Unknown On: 05:33
  • Share The Gag
  • Vinywaji vya pombe
    Kampuni mbili kubwa zinazozalisha pombe duniani zinatarajiwa kuungana baada ya SABMiller kukubali kiwango zaidi cha fedha cha kuinunua kutoka kwa mpizani wake mkubwa Anheuser-Busch InBev.
    SABMiller ilikubali kwa kanuni thamani ya hisa za pauni 44 kila moja baada ya majaribio manne kutoka kwa AB InBev.
    Bidhaa za AB InBev ni Budweiser,Stella Artois na Corona,huku SAB Miller ikiwa inazalisha Peroni na Grolsc.
    Iwapo mpango huo wenye thamani ya pauni bilioni 70 utafanikiwa,kampuni hiyo mpya itamiliki asilimia 30 ya vinywaji vyote vya pombe duniani.
    SABMiller ina wafanyikazi 70,000 katika zaidi ya mataifa 80 na mauzo ya dola bilioni 26.
    Vinywaji vya pombe AB InBev ina wafanyikazi 155,000 pamoja na mapato ya hadi dola bilioni 47.
    AB InBev ilijaribu kwa mara kadhaa kuungana na SAB Miller kwa kwango cha pauni 38,pauni 40,pauni 42.15 na pauni 43.50 kwa kila hisa,lakini viwango hivyo vilikataliwa na SAB Miller ambayo inasema kuwa hawaithamini kampuni hiyo.
    Katika taarifa ,bodi za kampuni hizo mbili zilisema hatimaye zimeafikiana kwa kanuni kupitia masharti kadhaa ya kuungana.
    Kampuni hizo mbili bado hazijaweka rasmi masharti ya muungano huo,lakini hatua hiyo inamaanisha kwamba zimeongeza mda wa ununuzi.

    Created by BBC Swahili

    0 comments:

    Post a Comment