Video Queen wa Bongo ambaye pia aliwahi kushiriki Miss Tanzania 2011,
Husna Maulid amewatangazia kichapo kwa mastaa wawili wa Bongo Muvi,
Jacqueline Wolper na Elizabeth Michael ‘Lulu’ endapo watathubutu tena
kumsogelea mpenzi wake wa sasa (jina kalificha).
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Husna ambaye pia amejikita kwenye
ujasiriamali alisema kuwa, wakati f’lani yeye na Lulu walizinguana kwa
sababu ya mwanaume aliyekuwa akifahamika kwa jina la Seki, akawa mpole,
wakati mwingine akazinguana na Wolper kwa mwanaume Mkongo aitwaye Radjab
Mwami, kwake pia akazidiwa nguvu, akakaa pembeni, sasa amemnasa
mwanaume huyo na hataki ugomvi na mtu.
“Nimekuwa mvumilivu sana kipindi cha nyuma lakini sasa hivi
atakayethubutu kuniwangia nitamshushia kichapo, maneno haya yawafikie
hao watu,” alisema Husna.
Ijumaa lilimtafuta Wolper kuzungumzia mkwara huo alipopatikana alisema:
“Mimi nafikiri Husna bado ni mtoto, yaani hajakua kwa maana angekuwa ni
mtu mzima na akili zake asingeongea mambo hayo.”
Lulu hakupatikana kupitia simu yake ya mkononi.
Chanzo:GPL
Saturday, 10 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment