Mzindakaya
alisema, CCM ni chama chenye heshima kubwa duniani na chenye Ilani ya
Uchaguzi bora, yenye heshima. Alisisitiza kuwa rais bora wa awamu ya
tano atatoka katika chama hicho.
Alisema
hayo juzi akiwawakilisha wazee wa mkoa wa Rukwa kwenye mkutano wa
kampeni ya kuwanadi wagombea urais, ubunge na udiwani kwa tiketi ya CCM
uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Ndua, Manispaa ya
Sumbawanga.
Mkutano
huo wa kampeni ulihudhuriwa na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa na
Halmashauri Kuu, Mizengo Pinda ambaye pia ni Waziri Mkuu. Wengine ni
pamoja na viongozi waandamizi wa CCM mkoa na wilaya.
“Sisi
wazee wa mkoa huu tunasema chama cha siasa chenye heshima kubwa duniani
ni CCM ambapo bila wasiwasi ndiko atakakotoka rais wa awamu ya tano
ambaye ni Dk John Magufuli …Tunawaasa viongozi wa CCM na wagombea
wasihangaike kugombana na wale waliohama CCM mkifanya hivyo mtakosea
sana,” alisisitiza .
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment