Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa.
MGOMBEA Ubunge jimbo la Iringa Mjini kupitia Chadema, Mchungaji Peter
Msigwa na wenzake watatu, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa
wa Iringa wakituhumiwa kushambulia na kujeruhi askari polisi wawili.
Katika mashitaka hayo, Msigwa ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la
Iringa Mjini na Waziri kivuli katika Wizara ya Maliasili na Utalii
katika bunge lililopita, alifikishwa na wenzake watatu shitaka
linalowakabili washitakiwa 10 kwa makosa hayo Mwendesha Mashitaka wa
Serikali, Blandina Manyanda aliwataja washitakiwa wengine waliofikishwa
mahakamani hapo mbele ya Hakimu Makazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa
Iringa, David Ngunyale, ku wa ni Edwine Sambala(66), Joseph Mgima (56)
na Josephat Chengula (36).
Manyanda alisema kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo Septemba
28 mwaka huu, ambapo watuhumiwa hao kwa pamoja walifanya makosa hayo kwa
kufanya kosa la uvunjifu wa amani katika eneo Sambala Kata ya
Gangilonga na kuwasababishia usumbufu kwa watumiaji wa barabara ya
Iringa Dodoma.
Created by Gazeti la HabariLeo.
Thursday, 8 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment