David Kafulila |
BAADA ya mvutano, hatimaye matokeo ya jimbo la uchaguzi la Kigoma Kusini, wilayani Uvinza mkoa wa Kigoma yametangazwa ambapo mbunge aliyekuwa anatetea jimbo hilo, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), ameanguka.
Msimamizi wa jimbo hilo, Reuben Mfune alimtangaza jana Hasna Mwilima wa CCM kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo kwa kupata kura 34,453 huku Kafulila akipata kura 33,382.
Mgombea mwingine alikuwa ni Nashon Bidyanguze wa Tadea aliyepata kura 6,382. Juzi mchakato wa kuhesabu matokeo ya jimbo hilo ulisimama baada ya dosari kujitokeza huku Kafulila akipinga kura kuhesabiwa upya.
Kafulila alidai zimetokea dosari katika kujumlisha kura, hivyo aliamuru ujumlishaji ufanywe kwa kutumia fomu zilizokusanywa kutoka kwenye vituo ambazo wasimamizi wanazo na wagombea wanazo, lakini Mwilima wa CCM hakukubaliana na ushauri huo.
Created by Gazeti la habarileo
0 comments:
Post a Comment