Tuesday, 13 October 2015

Tagged Under:

HRW lawalaumu wapiganaji wa Kikurdi

By: Unknown On: 05:13
  • Share The Gag
  • Human Rights Watch
    Shirika la kibinadamu la Human Rights Watch limewalaumu wapiganaji Wakurdi wa Syria wa Kaskazini Mashariki kwa kufanya kampeni ya makusudi kuwatimua manyumbani watu wenye asili ya Kiarabu kutoka maeneo ambayo wameyakomboa kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State.
    Amnesty wanasema kuwa katika maeneo mengine vijiji vizima vimeharibiwa kabisa.
    Kama ilivyo Kaskazini mwa Iraq, Ni Wakurdi wa Syria Kaskazini waliojitokeza kama wafuasi waaminifu zaidi kwa muungano wa wanajeshi wanaoongozwa na Marekani wanaokabiliana na wapiganaji wa Islamic State.
    Wamarekani waliwasaidia kwa kulipua makombora katika eneo la Kombani, na mwishoni mwa wiki iliyopita, muungano huohuo unaoongozwa na Marekani ulianza kudondosha risasi kwa wapiganaji wa kundi hilo la Wakurdi lijulikanalo kama YPG Kaskazini Mashariki mwa Syria.
    Image copyright Reuters
    Human Rights Watch Lakini Amnesty International wamesema kuwa Wakurdi wametekeleza uhalifu wa kivita kwa kubomoa nyumba za watu, na kuwalazimisha raia, wengi wao wakiwa Waarabu kutoka katika maeneo ambayo yamekombolewa na Wakurdi.
    Katika kijiji cha Husseiniya, Amnesty wanasema mijengo 14 ndiyo iliyobakia imesimama kati ya mijengo 225.
    Amnesty walinukuu wakaazi wa vijiji vya Waarabu wakisema kuwa walionywa kuwa wangepigwa risasi kama wangeendelea kukaa mahali hapo.
    Inadaiwa Wakurdi pia walisema wangewataja Waarabu hao kama magaidi ili walipuliwe kwa ndege za kivita na Wamarekani.
    Amnesty walionya Uingereza na mataifa wanayoungana nayo dhidi ya kupuuza uhalifu wa kivita unaotekelezwa na washirika wao katika vita dhidi ya Islamic State.
    Wapiganaji Wakurdi, YPG, na chama chake asili PYD wamekanusha mara kwa mara kuwa wamekuwa wakiwatimua watu kutoka makaazi yao ingawa walikiri kuwa kumetokea kile walichotaja kama makosa madogomadogo.
    Created by BBC Swahili

    0 comments:

    Post a Comment