Mgombea Urais wa CC, Dk John Magufuli. |
YAKIWA yamebaki majimbo ya 69 kabla ya kutangazwa kwa matokeo yote ya urais, Watanzania wanaonekana kumpa kazi mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli (pichani) kuwaongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo baada ya kura nyingi kuelekezwa kwake.
Mpaka jana Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliyo chini ya Jaji mstaafu Damian Lubuva, imetangaza majimbo 196, ambapo mgombea wa CCM, Dk Magufuli anaongoza katika majimbo 156 huku mpinzani wake wa karibu, mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa akipata majimbo 39.
Kwa mujibu wa kura zilizotangazwa na NEC, Dk Magufuli amejikusanyia kura 6,026,197 dhidi ya kura 4,251,282 za Lowassa huku tofauti kati ya wagombea hao ikiwa ni kura 1,774,915. Majimbo yaliyotangazwa jana jioni ni Ilala, Bububu, Tabora Mjini, Dodoma Mjini, Segerea, Geita Mjini, Rufiji, Kibiti, Mbarali, Bariadi, Temeke, Ubungo, Busokelo, Kwela, Morogoro Kusini, Karagwe, Muheza, Arumeru Mashariki, Nyamagana, Mtwara Mjini, Bukoba Vijijini, Songwe, Nchemba, Buchosa, Kilwa Kaskazini, Kibakwe, Kilwa Kusini, Morogoro Kusini Mashariki, Hanang, Morogoro Mjini na Kigamboni.
Akizungumza jana, Jaji Lubuva alisema, “Tumeshatangaza majimbo 195, yaliyobaki tutamalizia kesho (leo) kabla ya keshokutwa kutoa cheti kwa mshindi.” Mawakala waridhia Katika hatua nyingine, mawakala wa vyama vya vinne kati ya vinane vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu, wameridhishwa na mwenendo na matokeo yanayotolewa na Tume na kuahidi kushirikiana na mgombea atakayeshinda kiti cha urais.
Wakala wa Tanzania Labour Party (TLP), Dominata Rwechungura, alisema chama hicho kimeridhika na mwendo wa utoaji wa matokeo unaofanywa na tume na kwamba wanaopinga matokeo hayo wana ajenda ya siri ya kuiingiza nchi katika mchafuko. “Watu na viongozi waache kuamini matokeo yao ya kwenye mitandao, matokeo ya tume ndiyo halali na yanatoka kwenye vituo. Sisi tumeridhika nayo, hao wanaopinga wana ajenda ya siri,” alisema Rwechungura.
Naye Wakala wa National for Reconstruction Alliance (NRA), Salum Joseph, aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kulinda amani na kuwaonya vijana kuwa makini ili wasitumike na wanasiasa kwa ajili ya maslahi yao binafsi. Alimtaka kiongozi atakayechaguliwa kuwatumikia wananchi na kulisogeza taifa mbele ili liwe lenye mafanikio. Kwa upande wake, Wakala wa UPDP, Felix Makuwa aliipongeza Tume kwa kazi nzuri waliyoifanya na kutangaza matokeo kwa muda waliopanga, huku akisistiza kuwa ni lazima Watanzania tulinde amani na kuondokana na kauli za uchochezi zinazotolewa na viongozi wa vyama vya siasa.
Doni Mnyamani ambaye ni Wakala wa NDC, alisema chama chake kimeridhika na mwenendo wa utoaji wa matokeo licha ya kutofanya vizuri na kuwa pamoja na kuwapo mapungufu ni ya kibinadamu. Tume kutolumbana Aidha, siku moja baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kuishutumu NEC kuwa inashiriki katika uchakachuaji wa matokeo ya urais yanayoendelea kutangazwa, Lubuva alikanusha huku akieleza kuwa Tume hiyo haiko tayari kuendelea kulumbana na vyama au wagombea.
Alisema matokeo yanayotangazwa ndiyo yaliyopokelewa kutoka kwenye majimbo husika na ambayo yameshahakikiwa na kukubaliwa na mawakala waliopo katika majimbo husika na kwamba Chadema ina wakala kila kituo ambaye aliyakubali matokeo hayo. “Tunachosema ni hukumu ya wananchi wenyewe, upotoshwaji unaofanywa haukubaliki na ni mbaya. NEC inatangaza kilichotoka kwenye majimbo na haiongezi hata nukta,” alisema.
Jimbo la Ushetu Mghwira kura 397, Magufuli kura 51,034 na Lowassa kura 21,585. Jimbo la Tunduma Mghwira kura 153, Magufuli kura 19,446, na Lowassa kura 32,219. Jimbo la Sumbawanga Mjini Mghwira kura 350, Magufuli kura 43,542, na Lowassa kura 34,201. Jimbo la Musoma Mjini Mghwira kura 135, Magufuli kura 33,658, na Lowassa kura 25,352. Jimbo la Magu Mghwira kura 434, Magufuli kura 69,961, na Lowassa kura 30,070.
Jimbo la Geita Mghwira kura 377, Magufuli kura 45,472 na Lowassa kura 18,640. Jimbo la Busega Mghwira kura 458, Magufuli kura 47,049, na Lowassa kura 19,765. Jimbo la Shinyanga Mjini Mghwira kura 144, Magufuli kura 41,692, na Lowassa kura 25,465. Jimbo la Same Mashariki Mghwira kura 203, Magufuli kura 18,520, na Lowassa kura 17,874. Jimbo la Rorya Mghwira kura 438, Magufuli kura 54,892, na Lowassa kura 36,569.
Jimbo la Nyasa Mghwira kura 386, Magufuli kura 30,609, na Lowassa kura 14,062. Jimbo la Mufindi Kaskazini Mghwira kura 294, Magufuli kura 26,412, na Lowassa kura 8,085. Jimbo la Mtwara Vijijini Mghwira kura 392, Magufuli kura 25,938, na Lowassa kura 24,518. Jimbo la Msalala Mghwira kura 346, Magufuli kura 44,213, na Lowassa kura 16,942. Jimbo la Mpanda Mjini Mghwira kura 239, Magufuli kura 32,770, na Lowassa kura 16,569.
Jimbo la Moshi Vijijini Mghwira kura 429, Magufuli kura 25,017, na Lowassa kura 54,823. Jimbo la Mikumi Mghwira kura 390, Magufuli kura 35,192, na Lowassa kura 26,841. Jimbo la Mbinga Vijijini Mghwira kura 949, Magufuli kura 55,895, na Lowassa kura 12,213 Jimbo la Mbarali Mghwira kura 1,169, Magufuli kura 55,933, na Lowassa kura 45,374. Jimbo la Lushoto Mghwira kura 266, Magufuli kura 28,058, na Lowassa kura 8,673.
Jimbo la Lupa Mghwira kura 402, Magufuli kura 37,684, na Lowassa kura 20,175. Jimbo la Ludewa Mghwira kura 324, Magufuli kura 35,364, na Lowassa kura 11,715. Jimbo la Liwale Mghwira kura 138, Magufuli kura 19,967, na Lowassa kura 23,176. Jimbo la Kishapu Mghwira kura 661, Magufuli kura 65,173, na Lowassa kura 17,177. Jimbo la Kilosa Mghwira kura 551, Magufuli kura 55,839, na Lowassa kura 24,276.
Jimbo la Kilombero Mghwira kura 232, Magufuli kura 49,478, na Lowassa kura 49,166. Jimbo la Kilolo Mghwira kura 477, Magufuli kura 52,517, na Lowassa kura 25,424. Jimbo la Kavuu Mghwira kura 157, Magufuli kura 21,483, na Lowassa kura 8,083. Jimbo la Kasulu Mjini Mghwira kura 2,226, Magufuli kura 32,297, Lowassa kura 15,762. Jimbo la Kalambo Mghwira kura 555, Magufuli kura 38,165, na Lowassa kura 29,501.
Jimbo la Kahama Mjini Mghwira kura 346, Magufuli kura 58,728, na Lowassa kura 27,501 Jimbo la Ismani Mghwira kura 127, Magufuli kura 26,766, na Lowassa kura 15,303. Jimbo la Iringa Mjini Mghwira kura 224, Magufuli kura 36,584, na Lowassa kura 38,860. Jimbo la Hai Mghwira kura 263, Magufuli kura 29,341, na Lowassa kura 49,125. Jimbo la Gairo Mghwira kura 475, Magufuli kura 44,659, na Lowassa kura 6,925 Jimbo la Chato Mghwira kura 538, Magufuli kura 83,820, na Lowassa kura 27,936.
Jimbo la Mahonda Mghwira kura 9, Magufuli kura 4,760, na Lowassa kura 1,449 Jimbo la Sumve Mghwira kura 189, Magufuli kura 32,079, na Lowassa kura 11,203 Jimbo la Mbogwe Mghwira kura 478, Magufuli kura 44,558, na Lowassa kura 12,040. Jimbo la Kalenga Mghwira kura 376, Magufuli kura 40,896, na Lowassa kura 16,890. Jimbo la Rombo Mghwira kura 592, Magufuli kura 21,908, na Lowassa kura 57,715. Jimbo la Mlalo Mghwira kura 555, Magufuli kura 33,996, na Lowassa kura 8,938.
Jimbo la Tarime Mjini Mghwira kura 177, Magufuli kura 18,009, na Lowassa kura 15,992. Jimbo la Busanda Mghwira kura 575, Magufuli kura 73,834, na Lowassa kura 35,373. Jimbo la Mlimba Mghwira kura 328, Magufuli kura 39,555, na Lowassa kura 35,944. JImbo la Bukoba Mjini Mghwira kura 92, Magufuli kura 27,620, na Lowassa kura 25,898. Jimbo la Sengerema Mghwira kura 307, Magufuli kura 69,392, na Lowassa kura 28,335.
Jimbo la Bukombe Mghwira kura 487, Magufuli kura 50,063, na Lowassa kura 28,106 Jimbo la Mvomero Mghwira kura 156, Magufuli kura 68,179, na Lowassa kura 33,468. Jimbo la Tanga Mjini Mghwira kura 401, Magufuli kura 65,340, na Lowassa kura 56,939 Majimbo yaliyotangazwa juzi usiku ni: Jimbo la Mfenesini Mghwira kura 23, Magufuli kura 4,496, na Lowassa kura 3,047. Jimbo la Rungwe Mghwira kura 605, Magufuli kura 47,862, na Lowassa kura 41,534. Jimbo la Arumeru Mghwira kura 524, Magufuli kura 27,658, na Lowassa kura 105,720.
Jimbo la Pangani Mghwira kura 80, Magufuli kura 14,041, Lowassa kura 10,151. Jimbo la Korogwe Vijiji Mghwira kura 511, Magufuli kura 51,984, Lowassa kura 19,050. Jimbo la Kijito Upele Mghwira kura 50, Magufuli kura 8,075, Lowassa kura 5,639. Jimbo la Chaani Mghwira kura 24, Magufuli kura 4,689, na Lowassa kura 2,585. Jimbo la Kiembesamaki Mghwira kura 22, Magufuli kura 6,618, na Lowassa kura 5,610.
Jimbo la Manyoni Magharibi Mghwira kura 233, Magufuli 24,675, na Lowassa kura 9,901. Jimbo la Iramba Magharibi Mghwira kura 572, Magufuli kura 50,322, na Lowassa kura 11,714. Jimbo la Dimani Mghwira kura 22, Magufuli kura 5,292, Lowassa kura 1,8618. Jimbo la Nzega Mghwira kura 84, Magufuli kura 18,843, Lowassa kura 10,155. Jimbo la Igunga Mghwira kura 232, Magufuli kura 36,796, na Lowassa kura 18,600.
Jimbo la Urambo Mashariki Mghwira kura 373, Magufuli kura 36,458, Lowassa kura 22,385. Jimbo la Babati Vijijini Mghwira kura 409, Magufuli 67,183, Lowassa kura 42,334. Jimbo la Kiteto Mghwira kura 172, Magufuli kura 41,862, Lowassa 31,269. Jimbo la Bukene Mghwira kura 456, Magufuli kura 36,229, Lowassa kura 11,380. Jimbo la Sikonge Mghwira kura 568, Magufuli kura 36,729, Lowassa kura 16,164. Jimbo la Kaliua Mghwira kura 1,342, Magufuli kura 28,599, Lowassa kura 19,724.
Jimbo la Bulyankulu Mghwira kura 565, Magufuli kura 35,329, Lowassa kura 7,568. Jimbo la Kyela Mghwira kura 261, Magufuli kura 44,451, Lowassa kura 37,563. Jimbo la Manonga Mghwira kura 270, Magufuli 32,013, Lowassa 14,343. Jimbo la Ukerewe Mgwira kura 655, Magufuli 55,091, Lowassa 47,667.
Jimbo la Mpwapwa Mghwira kura 280, Magufuli kura 37, 480, Lowassa kura 8,230. Jimbo la Longido Mghwira kura 118, Magufuli 14,621, Lowassa 25,361. Jimbo la Kondoa Mjini Mghwira kura 117, Magufuli kura 15, 113, Lowassa kura 7,102.
Created by Gazeti la HabariLeo
0 comments:
Post a Comment