NA FREDY AZZAH, MWANGA
MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward
Lowassa, ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumaliza utata wa wapi
wanafunzi wa vyuo vikuu watapigia kura kwa vile hiyo ni haki yao ya
msingi.
Kwa sasa kuna utata kama wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wengi wako
likizo wataruhusiwa kupigia kura popote walipo au mpaka warudi
vyuoni walikojiandikishia.
“Naomba NEC itafakari upya suala hili, ihakikishe wanafunzi wanapiga
kura kwa kuwa ni haki yao ya msingi na wao ni sehemu ya Watanzania,”
alisema Lowassa.
Lowassa aliyasema hayo jana mkoani Kilimanjaro katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Kwasakwasa, Same.
Pia alizungumzia kukatika katika umeme nchini akisema haamini kama sababu zinazotolewa zina mashiko.
Watanzania hivi sasa wako njia panda kutokana na kukatika au kuwapo mgao wa umeme.
Katika serikali yangu sitavumilia watumishi wazembe katika shirika la
umeme, haiwezekani mpaka leo tatizo la umeme nchini liendelee, nikiingia
siwezi kulivumilia tatizo hili,” alisema Lowassa.
Baada ya mkutano huo wa kampeni, Lowassa alikwenda kuzulu kaburi la
mmoja wa waasisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), marehemu Peter Kisumo
aliyefariki dunia Agosti mwaka huu. Wakati huo alizuiwa na polisi
kushiriki mazishi yake.
Lowassa alifika eneo la Usangi na kupokewa na Daniel Mchangila ambaye ni kaka wa marehemu Kisumo.
“Yaliyopita yamepita, tunashukuru leo umekuja na sisi tangu asubuhi tuko hapa tunakusubiri.
Lowassa alisema anamshukuru Mungu kwa kutimiza azma yake ya kuhani kaburi la mwanasiasa huyo.
Mbatia na TBL Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia, alisema serikali
imeuza hisa za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) zenye thamani ya Sh bilioni
176 na fedha hizo kuzipeleka kwenye kampeni za CCM jambo ambalo ni
kinyume cha taratibu.
Alisema kwa sasa wanataka pia kuuza hisa za Benki ya NMB na Kampuni ya Sigara (TCC).
Created by Gazeti la Mtanzamia.
Wednesday, 7 October 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment